Kikosi kipya Taifa stars chatangazwa hakuna mchezaji wa Mbeya city

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
Kocha wa timu ya taifa stars Kim Poulsen ameteua wachezaji 32 kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya na atachuja wachezaji hao kupaki nao 20 watakaoenda kucheza michuano ya CECAFA nchini Kenya. Katika kikosi hicho akuna mchezaji wowote wa Mbeya City.

Makipa: aishi Manola(azam), Deo Munishi,ally mustafa(wote yanga), Ivo mapunda(gor mahia).

Mabeki: Agress moris, Ismail gambo na said morad(wote azam), Kelvin yondan,nadir haroub(wote yanga), michael pius(Ruvu shooting).

Viungo wakabaji: Erasto nyoni, Himdi mao, sure boy(wote azam), shomari kapombe(Ac Cannes), vicent barbanas(mtibwa), frank domayo,athuman iddy(wote yanga), said dilunga(ruvu shootin), willium lucian, jonas mkude(wote simba).

Viungo washambuliaji: Amri kiemba, haruna chanongo,ramadhan singano(wote simba), mrisho ngassa, simon msuva(wote yanga), farid mussa, joseph kimwaga(wote azam), mwinyi kazimoto(markhiya, Qatar).

Washambuliaji: mbwana sammata, thomas ulimwengu(wote Tp Mazembe), Elias maguli(ruvu shooting) na juma liuzio(mtibwa sugar)
 
Hivi Bertram Mwombeki sio Mtanzania?

mwombeki1.jpg
 
Huyu kocha huenda hajawahi kuhudhuria hata mechi moja ya ligi Mbeya city iliyocheza. Simba inachechemea kwenye ligi lakini imetoa wachezaji kibao, kicha inaelekea ana balance kwanza Simba na Yanga then anaangalia vigezo. Kocha alikuwa Maximo Tu...
 
Mbeya City hakuna mchezaji pale ni jihad tu...
 
Mpaka wachezaji wa Mbeya City waje wasajiliwe Yanga na Simba au Azam ndio wataonekana. Huyu Mzungu MPUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUZI kweli, keshaharibiwa na fitna za vilabu vya bongo
 
Jana nilisikia mahojihano ya aliyekuwa kocha wa Azam na leo nimekubali kauli zake ...Alisema mpira wa Afrika kwa ujumla haujali utaalamu kama mie kocha unaweza kushangaa hata mtunza maua anataka akupangie kikosi kiweje i.e kila mtu Tanzania anajifanya ni kocha... kwahiyo kutokuwepo Mbeya ndo timu mbovu? na wasipoitwa leo kwani soka linaisha leo,kwanini hatujiamini na kuwaamini watu wetu badala yake tunapenda sana short kati ? mbona wa timu zingine hawapo pia? basi tu kisa Mbeya haina mchezaji
 
Ndio, ni haki yao kuhoji. Iweje timu ya pili kwenye ligi ambayo wachezaji wote ni watanzania isiwe na mchezaji hata mmoja kwenye timu ya taifa?
Wewe mwenyewe hushangai?
 
tuwape Muda mBEYA cITY , KWANZA NI FURSA KWAO KUJIPANGA KWA UBINGWA, maana kikosi kitandelea kudumu kambini
 
Ndio, ni haki yao kuhoji. Iweje timu ya pili kwenye ligi ambayo wachezaji wote ni watanzania isiwe na mchezaji hata mmoja kwenye timu ya taifa?
Wewe mwenyewe hushangai?

Binafsi sishangai lakini pia haiko nafasi ya pili kama unavyoongozwa na hisia tu ...kwani Ruvu ni ya pili ama iko rank moja na Mtibwa? think big na msipoangalia mtaiangamiza hiyo timu yenu kwa ushabiki wa kijinga.
 
Kuwa wapili ktk ligi haimaanish una vigezo vyote na mashart ya kuitwa kikosin cha taifa na kuwa wapili bado xana kutabir matokeo kwa kua lig bado changa xana kwa sasa
 
Back
Top Bottom