Kikosi cha Yanga kilichofungwa na Simba ni sawa na kikosi kile kilichokuwa kinafungwa sana na mzee wa Kiminyio Madaraka Suleimani

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
SIMBA VS YANGA;KIKOSI CHA YANGA KILICHOFUNGWA NA SIMBA NI SAWA NA KIKOSI KILE KILICHOKUWA KINAFUNGWA SANA NA MZEE WA KIMINYIO MADARAKA SULEIMANI.

Leo 10:15hrs 17/04/20223

Mwaka 1994 timu ya Yanga ilikuwa na timu bora sana lakini kikosi hicho bora kililegezwa na mgogoro mkubwa wa Yanga asili na Yanga Kampuni,mgogoro huo ulisababisha timu ya Yanga kupigwa kipigo cha mbwa mwizi cha 4-1,Je wachezaji walileta mgomo baridi kutekeleza mgogoro huo sijui,ila tangu hapo Yanga iliendelea kufungwa kwa misimu miwili mfululizo hadi mwaka 1996 ilipozinduka tena,baada ya Kocha Tambwe Leya kukichukua kikosi cha pili cha Yanga na kukisuka kwa ajili ya ligi na kukiita kikosi hicho "Black Stars".

Kikosi cha kwa kwanza cha Yanga iliyokuwa bora kiliundwa na Makipa Steven Nemes na Riffat Said,mabeki Ngandou Ramadhani,Joseph Lazaro, Kenneth Mkapa, Willy Mtendamema,Costantine Kimanda, Willy Martin,Viungo wa kati walikuwa Method Mogella, Mwanamtwa Kihwelo, Said Mwamba Kizota, Sekilojo Chambua,Mawinga David Mjanja,Sanifu Lazaro, na Edibily Lunyamila, Wafunga mabao walikuwa Mohamed Hussein Mmachinga, James Tungaraza na Ally Yusuph Tigana, Unaweza kujionea kikosi bora cha Yanga kilichofungwa 4-1 na Simba mwaka 1994, baada ya kipigo hicho na Kocha Tambwe Leya kuanzisha timu nyingine ya Yanga kwa kukichukua na kukinoa kikosi cha pili cha Yanga, wachezaji wa timu ya kwanza wakaanza kuchukuliwa na timu kali za wakati huo zilizokuwa zinawatolea udenda, Kipa Riffat Said na Winga Edibily Lunyamila wakachukuliwa na timu ya Malindi ya Zanzibar, huku Steven Nemes na Said Mwamba Kizota wakichukuliwa na Simba Sports Club ya Msimbazi.

Kocha Tambwe akakiinua rasmi kikosi cha pili kuwa kikosi cha kwanza nacho kiliundwa na vijana wadogo wa wakati huo Anwar Awadh aliyepewa jukumu moja tu la kuweza kumkaba Mshambuliaji hatari Mzee wa Kiminyio Madaraka Suleiman,aliyekuwa akiifunga Yanga kila inapokutana na Simba,vijana wengine walikuwa ni Nonda Shaaban "Papii" aliyepikwa vyema na Kocha Tambwe Leya na baadae kuja kuwa mchezaji mkubwa wa dunia akiichezea timu ya Monaco, Rennes, Roma na Galatasaray,wengine ni Mzee Abdallah,Silvatus Ibrahim "Polisi" Maalim Saleh "Romario" baada ya vijana wa kikosi cha pili "Black Stars" kujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza likaja pambano la Simba na Yanga,pambano hilo lililisha 0-0 huku Mzee wa Kiminyio akiminywa vikali na Anwar Awadh,baada ya mechi mashabiki walimbeba juu juu Anwar Awadh hawakuamini kama angemudu kumkaba Madaraka Suleimani "Mzee wa Kiminyio".

Black Stars ya Tambwe Leya ndio Yanga imara iliyokuja kucheza nane bora ya ubingwa wa Afrika mwaka 1998 na ndio Yanga iliyochukua ubingwa wa Afrika Mashariki na kati mwaka 1999 nchini Uganda,hiki ndio kikosi kilichopambana kuvishinda vikosi kamili vya timu kubwa za nchi hii kama Mtibwa Sugar pamoja na Malindi,Mlandege na KMKM za visiwani Zanzibar,hiki ndio kikosi cha Yanga kilichoanzishwa kukabili matatizo ya vkikosi cha kwanza,ni sawa na kikosi kile cha Simba cha mwaka 1977 kilichoongozwa na Abdallah "king" Kibadeni Mputa kilichoifunga Yanga 6-0, Nimalizie kwa salute kubwa kwa wachezaji wa muda wote wa Yanga Ali Mayay,Salvatory Edward,Akida Makunda,Bakari Malima, Edibily Lunyamila,Kwa faida wa vijana waliozaliwa mwaka 2000, Hapa chini naweka kikosi kazi cha wachezaji wa Yanga ambao walikuwa tishio sana miaka hiyo.

1) Goli kipa- Steven Nemes, huyu hakuna mtu wa miaka hiyo, asiejua kazi kubwa aliyoifanya kwa timu ya Yanga pamoja na timu yetu ya Taifa (jamaa utahisi alikuwa na sumaku mikononi kwa jinsi alivyoivuta mipira mikononi mwake). 2) Difenda- Mwanamtwa Kihwelo, huyu kumpita ilikuwa ni kazi ngumu sana kwa vile alikuwa na akili ya kile anachokifanya uwanjani (kwake yeye ilikuwa ni bora mpira upite ila mchezaji abaki, au mchezaji akipita basi mpira utabaki) 3) Kenneth Mkapa, mkongwe halisi na moto wa kuotea mbali ambae hajawahi kutoa boko au kuharibu mpira hata siku moja (mkapa hata timu za nje zilikuwa zinamhofia sana, kutokana na umahiri mkubwa wa uchezaji wake). 4) Midfielders- Sanifu Lazaro, ukipenda mwite Mwiba (sifa zake hazina shaka kiuchezaji). 5) Thomas Kipese, winga machachari ya kushoto (ilikuwa ukimpa pasi anatembea na mpira mdogo mdogo, maana wachezaji wa timu pinzani walikuwa wanaogopa kumfuata asiwadhalilishe kwa kanzu au tobo. 6) Salvatory Edward, mzee wa pasi to pasi. 7) Nico Bambaga, kichoteo (yani alikuwa akishika mpira anauchota tu mpaka kwa mfungaji, sasa hapo inabaki kazi ya mfungaji, afunge au atoe nje) 8) Forwards- Salumu Kabunda, tingatinga (jamaa alikuwa kajaa kama mzee wa "GYM" afu misuli iliyokakamaa kiasi kwamba ukipigana nae bambi lazima utoke nje ukapokee matibabu) 9) Shaban Nonda "Papii" (Mkongo), huyu nae hakuwa nyuma katika kufanya kile kilichompeleka uwanjani baadae akahamia Monaco ya Ufaransa,rennes, Roma na Galatasaray 10) Saidi Mwamba Kizota, mzee wa kunyakuwa (alikuwa na uwezo wa kunyakua mpira juu ya kichwa cha mtu kupitia miguu yake mirefu tena bila kumgusa aliechukuliwa mpira) kwa ufungaji pia alikuwa tishio,

Kwa namna ya pekee kabisa katika mechi ya Taifa Stars vs Liberia,George Weah hatosahau siku aliyopigwa tobo na baadae kanzu na mzee huyu wa kiminyio,wengi tulimfananisha na Rivaldo wa Brazil,niwie radhi sana Mh George Weah,wewe utabaki kuwa nembo ya mpira barani 11) Edibilly Jonas Lunyamila, huyu hata ukienda Rwanda, Congo, Burundi, Zambia, Kaburu na kwengineko wanamfahamu fika kwa umahiri wake wa kutambaa na mpira hasa pembezoni mwa chaki, (mabeki walikuwa wanasakiziana kumfuata) na yeye alitumia mwanya huo kufanya yake, kwa kufunga magoli mengi. Nikija upande wa Simba naweza kusema wachezaji wao wengi nimewasahau ila kuna baadhi nawakumbuka kama vile 1) Goli kipa- Mohammed Mwameja, Tanzania one (huyu aliisaidia sana Simba na Taifa Stars, mpaka kuna watu walihisi labda jamaa ana mikono mingine pembeni ya akiba) 2) Difender- Alphonce Modest. 3) Husein Marsha. 4) Forwards kuna- Dua Saidi. 5) Madaraka Selemani, "mzee wa kiminyio" , yani alikuwa anatisha kama anaenda mbele afu anauminya mpira, beki anajikuta kapitiliza mzima mzima afu yeye anamua atoe pasi au aendelee na mpira akafunge. Hao ni baadhi ya wachezaji hodari na mahiri wa timu hizo wa muda wote. Ila kama kuna mdau mungine aliekuwa anafatilia timu hizi, na michezo kwa ujumla anaweza akaongeza wengine tuliowasahau kutoka hata timu zingine kongwe za miaka hiyo.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business administration in International Business.

-Master of Leadership and Management

Recent Publications;
-Assessment on the Effects of Microfinancing on Poverty Reduction.
 
😅😅😅
Simba imeshinda dunia nzima imefurahi na Taifa liko mikono salama😅😅😅
 
IMG-20230417-WA0029.jpg
 
Hamisi Kinye 1
Yussuf Athumani Ismail Bana 2
Ahmed Amasha 3
Goodwin Aswile "Scania" 4
Athumani Juma Chama 5
Juma Mkambi na Issa Athumani 6/8
Charles Boniface Mkwasa 8
Makumbi Juma "Homa ya Jiji" 9
Omar Hussein " Keegan", Abeid Mziba na Edgar Fongo 10
Rashid Hanzuruni 11
 
Back
Top Bottom