Kikongwe wa miaka 90 adaiwa kuuawa kisa kumkataza kijana asipande mnazi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Hilda Ngassa (90) ameuawa kwa kudaiwa kukatwa kwa panga na Yohana Luhanga (32) ambaye naye ameshambuliwa na wananchi wenye hasira kali na amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma akipatiwa matatibabu.

Inadaiwa sababu za kuuliwa kwa Hilda ni kutokana na kumkataza Luhanga asiangue makuti ya mnazi nyumbani kwake katika Mtaa wa Kinyambwa, Kata ya Kikuyu jijini hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda Otieno amesema tukio hilo lilitokea Julai Mosi mwaka huu katika Mtaa wa Kinyambwa, Kata ya Kikuyu jijini hapa.

Shuhuda wa tukio hilo, Rehema Ntaki amesema Luhanga alikwenda Hilda na kuomba kuangua makuti ya mnazi lakini alimkatalia kupanda juu ya mnazi kutokana na tatizo lake la ugonjwa wa kifafa.

"Ni hivi wanasema alikuja kuomba kuangua makuti ya mnazi akiwa na panga, bibi akamkataza yaani ndiyo kisa, akaanza kumshambulia kwa kumkata kwa panga," amesema shuhuda huyo.

Shuhuda mwingine Lazaro Juma amesema tukio hilo lilitokea saa sita mchana Julai Mosi mwaka huu.

Amesema Hilda alifariki eneo la tukio kutokana na kukatwa sehemu kubwa ya mwili wake hasa maeneo ya kichwani.

Mkuu Kitengo cha Wagonjwa wa Nje, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Samwel Magesa amekiri kupokea mwili wa marehemu pamoja na majeruhi Luhanga ambaye anaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Otieno amewataka wananchi kutojichukulia sheria mikononi kwani kufanya hivyo ni kosa.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom