Kikao kati ya CHADEMA na Serikali (Ikulu) chaisha, makubaliano haya hapa!

Waliotaka page nyingi walitaka kuanzia ngapi?
JE wanaofurahia muafaka huu wa kuanzia wanashabikia chama au maendeleo ya nchui?
Wanaoshabikia CDM kukubaliana, walitegmea kuwa walioenda kule walienda kugombana na na kuhakikisha kuwa hawajadiliani kwa muafaka?

Mie niko confused.

kwani nilivyokuwa nawaza mie katika majadiliano, mtu unapokuwa unataka kujadili jambo, kurudi mezani, kupata forum, tayari umekuwa tayari wa kupoteza baadhi na kupata baadhi,
sasa unapotegemea kwenda kwenye mazungumzo, ili wewe hoja zako zote ndio ziwe halali, yani umbadili mwenzako 100% akuunge mkono, nahisi huwezi kuita hiyo meza ya majadiliano kutafuta muafaka,
Mimi naomba niwapongeze wote walioenda kwenye huo mjadala, walivyoweza kuieleza, na walivyoweza kuonyesha umuhimu wa hoja zao,
Tanzania kwa hili tumepiga hatua,

sasa tuendelee na kipengele ambacho pia kinatupa shida sana, UTEKELEZAJI, wanapofika wale wataalamu wetu wa kuchambua yaliyosainiwa na viongozi, ili kuyaweka katika action plan inayotekelezeka,

Nawatakia mafanikio mema kwa ajili ya Tanzania yetu

Kwa sasa tujue Rais ana nguvu ya dola, ni nguvu kubwa na tunaiheshimu, na CDM wana nguvu ya watu wengi kiasi cha kutosha, wako na wakati, pia tunaheshimu hilo
Pia Rais anaelemewa na hitoria ya CCM, ukosefu wa imani kutoka kwa watu wengi, CDM wanaelemewa na historia ya kutokuaminiwa kwani hawajapata madaraka wakaonekana wanvyofanya kazi
 
Wasomi wamekuwa wasaliti wanaotia kichefuchefu. Kama usomi unashindwa kutoa majibu yenye tija kwa umma ni afadhali tuitazame elimu yetu upya kwani tunapotezeana muda. W/Mkuu mpya wa italia amethubutu kwa kuwaengua wanasiasa ambao wanaongozwa na maslahi binafsi kwenye baraza lake la mawaziri, sisi tumewajaza wanasiasa kibao, tuache ushamba.........
 
Mfumo wa kuendesha mambo yetu una makengeza, muafaka usipatikane katika mhimili husika ukapatikane kwenye mhimili mwingine, tunafanya nini? Huku si kuwacheza shere wananchi?
 
Waliotaka page nyingi walitaka kuanzia ngapi?

JE wanaofurahia muafaka huu wa kuanzia wanashabikia chama au maendeleo ya nchui?
Wanaoshabikia CDM kukubaliana, walitegmea kuwa walioenda kule walienda kugombana na na kuhakikisha kuwa hawajadiliani kwa muafaka?

Mie niko confused.

kwani nilivyokuwa nawaza mie katika majadiliano, mtu unapokuwa unataka kujadili jambo, kurudi mezani, kupata forum, tayari umekuwa tayari wa kupoteza baadhi na kupata baadhi,
sasa unapotegemea kwenda kwenye mazungumzo, ili wewe hoja zako zote ndio ziwe halali, yani umbadili mwenzako 100% akuunge mkono, nahisi huwezi kuita hiyo meza ya majadiliano kutafuta muafaka,
Mimi naomba niwapongeze wote walioenda kwenye huo mjadala, walivyoweza kuieleza, na walivyoweza kuonyesha umuhimu wa hoja zao,
Tanzania kwa hili tumepiga hatua,

sasa tuendelee na kipengele ambacho pia kinatupa shida sana, UTEKELEZAJI, wanapofika wale wataalamu wetu wa kuchambua yaliyosainiwa na viongozi, ili kuyaweka katika action plan inayotekelezeka,

Nawatakia mafanikio mema kwa ajili ya Tanzania yetu

Kwa sasa tujue Rais ana nguvu ya dola, ni nguvu kubwa na tunaiheshimu, na CDM wana nguvu ya watu wengi kiasi cha kutosha, wako na wakati, pia tunaheshimu hilo
Pia Rais anaelemewa na hitoria ya CCM, ukosefu wa imani kutoka kwa watu wengi, CDM wanaelemewa na historia ya kutokuaminiwa kwani hawajapata madaraka wakaonekana wanvyofanya kazi

HAIKA, Naunga mkono maoni yako, NI MAONI CHANYA NA YA KUJENGA KWA PANDE ZOTE. WELL DONE!
 
Watanzania wenzangu mabadiliko ya kweli ya taifa hili hayataletwa na vyama vya siasa tunaona njia ileile CUF waliyopita CHADEMA wanaifuata. Kweli viongozi wote wa siasa bongo ni sana na maslahi binafsi. Real Changes italetwa na watanzania watakapoamu kufanya hivyo na siyo vyama vya siasa. Kwa hili la Katiba CHADEMA tumeona mmepotoka mnakurupuka blia strategies. Kwa mmeshindwa kutumia kanuni ya 86. Pili mnakula matapishi yenu.
 
Sheria itaboreshwa kivipi wakati imepitishwa na bunge? Ina maana itarudishwa tena bungeni kufanyiwe marekebisho? Wananchi wanataka kufahamu wazi wazi nini kinaendelea baada ya haya mazungumzo.

Changa la macho hili.
 
Hivi ni kwanini muafaka wa chadema na Serikali usainiwe na waziri wa michezo john nchimbi? Kuna mantiki ipi? je sio danganya toto?
 
UPUUZI MTUPU KWA KUTAFUTA UMAARUFU AMBAO HAUNATIJA KWA TAIFA>HAYO MAKUBALIANO NI YAKUJIKOSHA KWA VILE MULIFANYA MAMBO YA KITOTO KUSUSA VIKAO VYA BUNGE AMBAKO MNGEWEZA KUCHANGIA KWA UWAZI>RAI YANGU KWA VYAMA VINGINE VISIKURUPUKE KUANDAMANA WALA KUSUSIA VIKAO HALALI VYA BUNGE>CHADEMA WAMETHIBITISHA WALIKUWA WANATAKA UMARUFU KWENYE MEDIA kwakujifanya wanamambo ya msingi kumbe si lolote.Waache kuwahadaa watanzania kwa kushawishi maandamano.
 
MAKUBALIANO HAYA HAPA CHINI:

30tothx.jpg

Kumbe Rais ameishasaini muswada uliopitishwa na bunge na kuwa sheria!!! maana naona katika makubaliano hayo mawili inazungumzwa kuboresha sheria hiyo. Tulitakiwa tujulishwe hili kuwa Rais alikubaliana na bunge juu ya mswada huo
 
Mnyika alikua katibu kwa upande wa ujumbe wa CDM ikulu,na Nchimbi alikua katibu kwa ujumbe wa serikali.What is your problem there?
 
Wana JF, labda mie sielewi, maana nasoma taarifa katika mwananchi katika Waraka wa makubaliano kati ya JK na Chadema kwamba "Waraka huo umependekeza sheria ibadilishwe ili kuweka utaratibu wa kuanzishwa tena kwa Serikali ya Tanganyika itakayoweza kujadiliana mustakabali wa Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa usawa. Walitaka serikali mpya ya Tanganyika itakayoundwa ijadiliane upya na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya mambo ya Muungano na muundo wa Muungano wenyewe."

Hi ina maana gani? Kwamba tunaanzisha serikali ya Tanganyika ili katiba mpya itungwe? Je serikali hii ya Tanganyika itaongozwa na nani? Itakuwa ya muda gani? Itaathirije muungano ambao upo tayari? Itaathirije makubaliano ya Tanganyika na Zanzibar yaliyofanywa ili kuunda Tanzania?

Yaani hapo jamaa wamenikoroganya najikuta kichwani niko Maswa na mwili uko Kindondoni! Nisaidieni wajameni.
 
Pale kulikuwa na ujumbe wa Ikulu na ujumbe wa Cdm, na kila ujumbe ulichagua Katibu wake...Usinakili vyeo vyao huku mtaani!
 
CDM ikaendelea kuacha ombwe la habari litajazwa na uvumi. CHADEMA ISIPOKUWA MAKINI HII INAWEZA KUWA HATUA MOJA NYUMA.
CDM ni chama makini, wana focus na vision ya Tanzania hii kwa miaka zaidi ya 200 sina wasiwasi kwa hilo, wapo kutetea wananchi wanyonge kama sisi.
 
Ulitaka asaini Mkama? Ule haukuwa mkutano wa vyama.

Ulikuwa mchezo fulani wa kuigiza....hivyo hayo ni mambo ya wizara ya Dr Nchimbi.
 
Back
Top Bottom