Kijiji cha Ruhita Karagwe kunawaka moto, tabaka tawala mmetutelekeza tena sisi masikini!

Omona Wanyu

Member
Feb 29, 2012
51
6
Ndugu watanzania wenzetu sisi wanakijiji wa kijiji cha Ruhita wilayani Karagwe ambao ni wafugaji hivi sasa navyoandika tunapigwa na kuchomewa Nyumba zetu hali ni mbaya sana zaidi ya Nyumba zetu 93 zimeshachomwa moto mpaka jana, Ngombe zaidi ya 163 zimepotea katika vurugu, watoto wamepotea, wake zetu wamepigwa na kunyanyaswa kijinsia, watu wanapata vilema vya maisha, familia zimekuwa wakimbizi ndani ya nchi yao wenyewe, wanapika na kulala nje na kuishi vichakani kwa hofu ya kukamatwa, Jeshi la Polisi Mkoa wanatekeleza amri na unyanyasaji huu wa kutisha, wakituita sisi wahamiaji haramu, huku Wanyarwanda MATAJIRI waliovamia na kupora ardhi yetu wamekwisha waweka sawa, kwa kuwapa mboga na kuachwa wakiendelea kupora ardhi yetu adhimu na kutuacha sisi wakiwa mbele ya serikali yetu, mpaka sasa hatuna Chakula watoto wanalia, Chakula kimechomwa moto, na wamepotezana na wazazi. WATANZANIA MLIOKO HUKO MJINI MTUSAIDIEEE! WENZENU TUNATESEKA NA HATUNA MATUMAINI NA SERIKALI YETU! Mheshimiwa Prof Anna Tibhaijuka binti yetu sisi wenyewe kweli hii ndio fadhila ya Usomi wako kwetu Mama?
 
Mkuu hii habari kama ni ya kweli haipendezi hata kidogo. Nina imani hapo kijijini kwenu kuna serikali ya kijiji ambayo siamini kama kweli inaweza kuacha watanzania halali wafurumushwe na FFU na kuitwa wahamiaji haramu wakati si kweli. Mleta hoja nina wasiwasi kuna mahali hautwambii ukweli.

Hebu twambie undani wa hilo zoezi!!!!!

Tiba
 
Si walikataa hoja ya Mdee ona sasa huu ufirahuni,mbunge wenu yule kilaza yuko wapi? kwel mpaka 2015 nchi itakuwa vpande
 
Huko ndio kwao Mbunge wa zamani wa TLP Benedict Mutungilehi, aende akaokoe jahazi wananchi na genge la majambazi ya ccm chini ya Mkuu wa Wilaya.Taarifa nilizo nazo ni kwamba Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kyerwa baada ya kufika huko ametekwa na kundi la wafugaji na kupewa zaidi ya ng'ombe 100 ambao naye ameanza kufuga kwa ujira wa kuwalinda wafugaji.asipokuwa kuwa makini atajikuja anaingia kwenye kashfa kubwa ya kutumikishwa na wafugaji kulinda maslahi yao.
 
Ndugu watanzania wenzetu sisi wanakijiji wa kijiji cha Ruhita wilayani Karagwe ambao ni wafugaji hivi sasa navyoandika tunapigwa na kuchomewa Nyumba zetu hali ni mbaya sana zaidi ya Nyumba zetu 93 zimeshachomwa moto mpaka jana, Ngombe zaidi ya 163 zimepotea katika vurugu, watoto wamepotea, wake zetu wamepigwa na kunyanyaswa kijinsia, watu wanapata vilema vya maisha, familia zimekuwa wakimbizi ndani ya nchi yao wenyewe, wanapika na kulala nje na kuishi vichakani kwa hofu ya kukamatwa, Jeshi la Polisi Mkoa wanatekeleza amri na unyanyasaji huu wa kutisha, wakituita sisi wahamiaji haramu, huku Wanyarwanda MATAJIRI waliovamia na kupora ardhi yetu wamekwisha waweka sawa, kwa kuwapa mboga na kuachwa wakiendelea kupora ardhi yetu adhimu na kutuacha sisi wakiwa mbele ya serikali yetu, mpaka sasa hatuna Chakula watoto wanalia, Chakula kimechomwa moto, na wamepotezana na wazazi. WATANZANIA MLIOKO HUKO MJINI MTUSAIDIEEE! WENZENU TUNATESEKA NA HATUNA MATUMAINI NA SERIKALI YETU! Mheshimiwa Prof Anna Tibhaijuka binti yetu sisi wenyewe kweli hii ndio fadhila ya Usomi wako kwetu Mama?

Mh Waziri Tibaijuka anasema hao wawekezaji hawana tatizo, na Serikali haitawazuia kuja. Lipo tumaini moja tu - to vote for change 2015 otherwise sisi wenyewe tutaja uzwa mchana kweupe
 
daa! poleni sana uko,mambo yanayoendelea uko ni kinyume na haki za binadamu,mi nimewai ona sana masikin wakinyanyaswa japo hawana atia,pesa imearibu dunia,wenye pesa wanafanya vile wanataka
 
wakuuu poleni sana kwani nyinyi mlipiga kura chama gani???
Sisi watu wa rombo 2nakura rahaa na mbunge we2 selasini coz ndie 2liyemchaguwa 2015 msifanye makosa tena
 
Ndugu watanzania wenzetu sisi wanakijiji wa kijiji cha Ruhita wilayani Karagwe ambao ni wafugaji hivi sasa navyoandika tunapigwa na kuchomewa Nyumba zetu hali ni mbaya sana zaidi ya Nyumba zetu 93 zimeshachomwa moto mpaka jana, Ngombe zaidi ya 163 zimepotea katika vurugu, watoto wamepotea, wake zetu wamepigwa na kunyanyaswa kijinsia, watu wanapata vilema vya maisha, familia zimekuwa wakimbizi ndani ya nchi yao wenyewe, wanapika na kulala nje na kuishi vichakani kwa hofu ya kukamatwa, Jeshi la Polisi Mkoa wanatekeleza amri na unyanyasaji huu wa kutisha, wakituita sisi wahamiaji haramu, huku Wanyarwanda MATAJIRI waliovamia na kupora ardhi yetu wamekwisha waweka sawa, kwa kuwapa mboga na kuachwa wakiendelea kupora ardhi yetu adhimu na kutuacha sisi wakiwa mbele ya serikali yetu, mpaka sasa hatuna Chakula watoto wanalia, Chakula kimechomwa moto, na wamepotezana na wazazi. WATANZANIA MLIOKO HUKO MJINI MTUSAIDIEEE! WENZENU TUNATESEKA NA HATUNA MATUMAINI NA SERIKALI YETU! Mheshimiwa Prof Anna Tibhaijuka binti yetu sisi wenyewe kweli hii ndio fadhila ya Usomi wako kwetu Mama?
Ndio mkome kuwa mnachagua magamba,si nyinyi ndio uwa mnajifanya wakereketwa?hamna mbunge hata mmoja ukanda huo,mnao wachumia tumbo tu wananosinzia bungeni,hamna wa kuwasemea,kwanza wabunge wenu hawana hata Mkazi Karagwe na wengine wanaishi nyumba za kupanga Dar,hawana anuani maalum
 
Hivi karne hii bado mnaishi kwenye mpita mzee,hata hivyo kama bado mna matumaini na serikali yenu hapa jamvini unataka msaada gani? Mi sina msaada!
 
Taarifa hizi kama ni kweli siyo njema. Najaribu kuwasiliana na rafiki zangu juu ya undani watukio hilo.

Kwa wale wasiotokea maeneo haya wanaweza wasijue nini mtoa thread anamaanisha. kwa kifupi Ruhita ni miongoni mwa vjiji vilivyokaliwa na wafugaji pamoja na wakulima. Suala la kuwa ni wahamiaji alamu au la hicho nikitu kingine. Ninachojua nikuwa kuna watanzania tena maskini wanaoendesha maisha yao hapo na wengi wakiwa wanachama na wapiga kura wa ccm.

Nikawaida vijiji vya mipakani kuwa na mwingiliano wa wakazi pande zote zinazopakana kama inavyowezakuwaMusoma, Arusha na maeneo mengine Tanzania inayopakana nayo .

Nijikumu la serikali kuhakikisha usalama wa wakazi na mali zao vinalindwa. Hata hivyo si mara yakwanza serikali ya chama tawala kutumia madaraka yake vibaya kuwanyanyasa wananchi ktk maeneo hayo. Serikali maranyingi imetumia vibaya operations za kuwatafuta wahamiaji alamu kwa kunyanganya na kupora mali za raia pamoja na 'wahamiaji alamu'. Si vyema serikali ikae kimya na maeneo hayo yakaliwe na wahamiaji alamu lakini pia si vyema serikali inapofanya operations za wahamiaji hao ziambatane na uporaji wa mali pamoja na vitendo vya uzalilishaji wa watu.

Wito wangu kwa serikali ya mkoa, wilaya na vijiji nikuwa wawatendee haki watu hawa; wawe raia au wawe wahamiaji alamu. Ninamaana sheria na taratibu zitumike ktk operations hiyo. Nakama kuna police, ama mtu yeyote aliyekabidhiwa madaraka na akayatumia vibaya basi mkono wa sheria na uwe juu yake.
 
ninajaribu kumtafuta mh Mbunge kujua kulikoni,Mathias Byabato anaweza kutusaidia kufatilia pia maana ni mdau humu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom