Kiingereza lugha ya east african community

mwitasa

Senior Member
Dec 28, 2013
199
476
Kipindi napitia taarifa mbalimbali kwenye mtandao nimekutana na taarifa moja kuwa yafuatayo ndio makubaliano kuhusu lugha rasmi ya east africa.

1. Lugha iliyopitishwa rasmi kutumika katika jumuia ni kingereza hivyo kiswahili na kifaransa vimekataliwa.

2.Nchi zote za jumuia zitakuwa na mtaala mmoja wa kufundishia kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya juu.

3.vyeti vya wahitimu wa elimu ya daraja husika vitakuwa na uzito sawa kwenye soko la ajira kwenye nchi wanachama.

Nisilolijua ni je
1. Tanzania itabadili mfumo wa ufundishaji kwenye elimu ya shule za msingi kutoka kiswahili kuwa kiingereza?

2.je vipi kuhusu waalimu wetu tunaowatumia kwa sasa kufundisha masomo hayo kwa kiswahili wameandaliwa kuanza kufundisha kwa kiingereza?

Toa mawazo na maoni yako mwana jf hii imekaaje.
 
Hata AU wamekubali kiswahili kuwa moja ya luhga zao, EAC kitu gani? Tusepe tu tuwaachie kiumoja chao cha hovyohovyo.

Tubaki na SADC yetu, wanachama wanaopendana na kuheshimiana.

Rwanda, Kenya, Uganda wanafki sana hawa watu.
 
Kipindi napitia taarifa mbalimbali kwenye mtandao nimekutana na taarifa moja kuwa yafuatayo ndio makubaliano kuhusu lugha rasmi ya east africa.

1. Lugha iliyopitishwa rasmi kutumika katika jumuia ni kingereza hivyo kiswahili na kifaransa vimekataliwa.

2.Nchi zote za jumuia zitakuwa na mtaala mmoja wa kufundishia kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya juu.

3.vyeti vya wahitimu wa elimu ya daraja husika vitakuwa na uzito sawa kwenye soko la ajira kwenye nchi wanachama.

Nisilolijua ni je
1. Tanzania itabadili mfumo wa ufundishaji kwenye elimu ya shule za msingi kutoka kiswahili kuwa kiingereza?

2.je vipi kuhusu waalimu wetu tunaowatumia kwa sasa kufundisha masomo hayo kwa kiswahili wameandaliwa kuanza kufundisha kwa kiingereza?

Toa mawazo na maoni yako mwana jf hii imekaaje.

Mkuu mimi kati ya vitu vinavyonichanganya ni hii Serikali yetu kusisitiza matumizi ya kiswahili na kukiweka pembeni kiingereza.
Ikumbukwe kwamba Pamoja na kukienzi kiswahili, kiingereza hakiepukiki. Juzi tu kuna mbunge mmoja amenukuliwa akilalamika kuwa wafanyakazi wengi wa shirika la ndege la Emirates wafanyakazi wengi wanatoka nchi jirani, hali kadhalika kwenye mahoteli kwenye mbuga za wanyama.[Hii ni kwa sababu ya uelewa wao wa Lugha ya Kiingereza]
Sasa kama jumuia ya Africa mashariki wana opt kiingereza, kinachofuata kila mtu anakijua.
Mtazamo wangu mm ni kuwa serikali isikitupe kiswahili, halikadhalika kiingereza.
 
Ni ukoroni wa mwingereza unaendelea na kwa sababu viongozi wetu ni kina Nape, kina mwigulu nchemba na kina mulugo hakuna la maana laweza fanyika kupingana nao...
 
Inasikitisha zaidi kuona Umma umekuwa kama mbuni uliyetumbukiza kichwa chake mchangani, eti anajificha, wakati jimwili lote liko nje!
Tumekuwa waoga wa tusichokifahamu, tumetokwa na utukutu wa kujithubutisha, tumebaki kujibana nyuma ya uzalendo.
Hata hicho Kiswahili.... hatukijui. Naona EAC iamue tutumie "ruga setu sa makabira adi apo malekebisho ya mitara ya erimu" Au mnasemaje wadau?
 
MizChief Likes This.
 
Leo nimekuwa na jamaa flani ambaye kamaliza Form Four ambaye kwa sasa anatafta kazi.Amenielezea ya kwamba aliulizwa iwapo anaelewa English ya kuandika na kusoma akajibu Ndio.Akaambiwa aende Interview baadaye.Amekiri ya kwamba hafahamu namna ya kuwasiliana in English.
My question,if we don't embrace English,to whom will such working opportunities go to?Alafu we start crying wolf eti foreigners are exploiting our country!Smh!
 
Kama unasafiri, ukipita viwanja vya ndege vya karibu nchi zote za uarabuni, utakutana vijana wakiume na kike wahudumu katika maeneo kadhaa ambao wamepata ajira kutoka Kenya. Kilichowapatia ajira nzuri zenye kipato cha kueleweka ni elimu yao na uwezo wa kuzungumza na kuelewa Kiingereza.
Hukuti Mtanzania hapo, labda awe kazaliwa hukohuko au masalia ya East African Airways!
Lakini bado tunaponda Kiingereza!
Kuna waliomaliza chuo kikuu....wao wanasema kiiingereza ni kipaji....
 
Ukweli ni huu kiswahili hakisaidii kabisa.
Jua kiingereza nchi yoyote duniani utapeta.
Kiswahili kinakusaidia kununua vitu sokoni na story kwenye vijiwe.

Nimeshuhudia kwa macho yangu wakenya na waganda wakipata kazi sababu ya kujua english uku watanzania wakilia na kusaga meno.

Kampuni nyingi za kigeni kama ujui english ata uwe profesa kama slim shady hupati kazi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom