KIGWANGALLA apendekeza Rais Asitishe Bunge Maalum la Katiba ili Kukubaliana Kuhusu Muundo Muungano!

Wanabodi,
Kuuliza sii Ujinga,
Hivi ni sababu gani haswa zilizojitokeza na kusababisha kuhitajika kwa katiba Mpya?
 
Naunga Mkono hoja ya Kuitisha Kura kuhusu Muundo wa Muungano.
Na hakika hili Lilipaswa kutangulia kabla ya Katiba yenyewe.

kuhusu kura ya maoni,hii serikali dhaifu ya magamba ilishauriwa sana ikaziba maskio kwa kuhofia kushindwa vibaya kwa serikali 2!!!! kwa sasa hatutaki huo upuuz na wasitake kuchezea kodi za watz!
 
bogus kabisa,..eti kikwete aongezewe mda wa urais,kujipendekeza kwa huyu mfanyakazi wa zamani wa tamwa!hajui kuwa ile sheria inasema maoni kuhusu muungano yawe ya kubiresha na sio kuuvunja na maoni ya watu kuhusu serikali tatu ni moja ya maoni ya kuuboresha.,eti naye huyu anaenda kulamba laki saba kwa siku.!
 
Nafikiri wewe unayesema kuwa UNAJUA ndiyo haujui kabisa. Daktari ameuliza swali nzuri kabisa ambalo kama ungekuwa unajua ungejibu na watu tungekuelewa. Katika utafiti wowote ni lazima ueleze ni njisi ngani ulivyofikia uamuzi wa kuchukua idadi fulani ya watu/vitu (sample size) ili kuwakilisha idadi kubwa ya watu/vitu (general population) na hii ni sehemu ya methodology na kuna fomula zake siyo swala la kaamua tu kama wewe ulivyosema hapo juu kuwa uliza watu kumi. Ulichotakiwa kutueleza kama kweli unajua ni kanuni gani tume ya warioba ilitumia ili kupata sample size ya watanzania waliohojiwa kuhusu muudo wa muungano inayowafaya waje na majumuisho ya asilimia 61 kama watu waliokubali muundo wa serikali tatu. Utafii wowote hauwezi kukubalika kisayansi kama sample size ilikuwa ni ndogo sana kulinganisha na general population unless kuna sababu za msingi za kushindwa kupata sample size ya kutosha na sababu lazima zielezwe. USIKIMBILIE KUTUKANA JIBU HOJA KISAYANSI.

Sasa ww ndio mjinga zaidi ya huyo Daktari wa watu; yeye anajenga hoja ya kuwa katika mabaraza ya katiba CCM ilikuwa na almost 65% ya wajumbe iweje tena 61% watake serikali tatu wakati msimamo wa CCM ni serikali MBILI? Mimi kiurahisi kabisa nikaona anauliza maswali ya kitoto hasa akitegemea ile 65%. Sasa methodology ni science ambayo haihusishi sampling na njia ya kuuliza tu, inahusisha mambo mengi zaidi kama approach/design, jinsi ya kuuliza maswali na hata jinsi yakuchambua majibu (analysis). Idadi ya watu waliokuwa kwenye mabaraza kata inajulikana; HAPA SWALI LA KIGWANGALA LINA MANTIKI GANI KAMA SIO KUTOKUJUA TU:

Angalia kwa mfano, TUME YA JAJI NYALALI pamoja na mambo mengine kipindi kile ilitumia njia hii hii ya sasa, 77% walisema wanataka chama kimoja, 23 vyama vingi lakini katika 77% watu zaidi ya 80% walitaka mabadiliko makubwa sana ndani ya mfumo wa chama kimoja ambayo yasingeweza kufanywa kwa chama kimoja and therefore wakaconclude ya kuwa INABIDI TUINGIE MFUMO WA VYAMA VINGI.

Watu kumi nimetoa kama mfano ambapo hata yeye anaweza akafanya pilot study kidogo aone majibu atakayopewa lakni lazima atengeneze maswali mazuri ya kiutafiti.

Kama hujui hujui tu...
 
kupunguza mamlaka ya rais,mawaziri wasiwe wabunge etc etc etc
Haya yote mbona yanawezekana kubadilishwa pasipo kuwa na katiba mpya?. Nijuavyo mimi katiba mpya inahitajika tu ikiwa tunabadilisha
1. Mfumo wa Utawala (ruler), iwe kutoka kutawaliwa, Udikteta na kadhalika.
2. Mfumo wa kiuchumi(Transitional economy)
3. Muundo wa nchi - Muungano wa nchi ama kuvunjika kwa muungano.

Hadi leo hii kusema kweli sijasikia sababu kubwa ya kuwa na katiba mpya ikiwa swala la Muungano halina uzito.
shingwengwe, mkuu wangu wala sijaingia kwa bahati mbaya ila nataka tu kuwakumbusha tulikotoka maana wengi mnaichukulia safari hii kwa matatizo tunayokutana nayo njiani kama ndizo sababu badala ya maamuzi ya mwanzo kufikia maamuzi ya kutaka na kuanza kusafiri.
 
Last edited by a moderator:
kwa hiyo ndugu yangu ingekuwa wewe ungetakaje hasa? Zanzibar wana nchi yao, ya Tanganyika iko wapi? kwa Wazanzibari Tanganyika yao. na kwa Watanganyika Zanzibar ni nchi ya watu. wewe ndugu penda nchi yako na kama mbunge usirudie kutoa hoja ya kikwete kubaki madarakani.
 
Inabidi wasomi wetu mnapojitokeza kutetea jambo kuacha kuwa biased Hili swala la zanzibar kuwa na katiba yake inayodeclare kuwa ni nchi huru kwa nini halizungumziki? Je, ni kitu gani kinachohalalisha uwepo wa serikali ya zanzibar lakini kinaharamisha uwepo wa serikali ya tanganyika? Katiba itaandikwa based on the majority opinions na haihitaji any methodological approach kwani sio scientific research. Katiba ni ya watu wote, hivyo CCM inabidi kuheshimu maamuzi ya wananchi.
 
ImageUploadedByJamiiForums1392479898.459251.jpg
 
How dare mtu kama Kigwangala anauliza eti ' nani aliwatuma tume kwenda kubadili muundo wa Muungano? Du! kweli kuelimika si kupitia wingi wa madarasa
 
Dr hana msimamo kwenye mambo yake. Michango yake ya awali kwenye facebook alikuwa anataka Serikali 3 Leo anauliza tume imetoa wapi serikali3
 
Hivi muundo wa serikali mbili una uhalali gani dhidi ya muundo wa serikali moja au tatu?!

Ni wananchi gani waliwahi kuhojiwa na kupendekeza serikali mbili?!

Muungano wenyewe ni haramu tangu kuasisiwa kwake kwani hauna baraka za watanzania(wenye nchi).
 
Katika Ukurasa wake wa facebook Mhe Kigwangalla ameandika muda si mrefu:

TAMKO LANGU KWA UMMA KUHUSU MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Ndugu wanahabari na waTanzania wenzangu,

Nimekuwa nikilazimika kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wanahabari, ndugu, jamaa na marafiki kuhusiana na namna mchakato wa kuandika katiba mpya ya Taifa letu unavyoenda; wengi wakipenda kujua nini mtazamo wangu kuhusu mambo mengi, haswa hili la serikali mbili ama tatu kwenye muungano wetu. Mara nyingi nimekuwa nikikwepa kusema msimamo wangu ni nini kwa sababu niliona ni vema nikajipa muda wa kutafakari kabla ya kuamua kujenga msimamo yangu. Ila kwa kuwa wakati wa kwenda Bungeni umefika na mimi nimepata bahati ya kuwa miongoni mwa wajumbe wa Bunge hili la kihistoria nimeona leo nitoe mtazamo wangu.

Kwanza, nianze kwa kuonesha wasiwasi wangu kama tutaweza kufika salama huko tuendako. Si kwa sababu za kitabiri kama mnajimu, la, ni kwa sababu za kisayansi, ambazo nitaziweka wazi hapa kama ifuatavyo:

(i.) Pamoja na kwamba tume imefanya kazi nzuri ya kukusanya maoni na kuyaweka katika nyaraka ambayo tutapaswa kuifanyia kazi, napata shida kama walikuwa makini katika kuendesha zoezi hili. Kivipi, binafsi napata shida na methodology iliyowawezesha kufikia ‘conclusion’ madhubuti kwamba watanzania asilimia 61 walitaka serikali tatu. Kwa sababu za kisayansi naona tume ya Mhe. Jaji Warioba imepotoka na kwamba kusema hivyo ni kutaka kulazimisha uhalali wa hoja hii nyeti kwenye dokumenti ya Rasimu ya Katiba tunayopaswa kuipitisha bila kuwa na msingi wa kitakwimu unaotokana na njia (methodology) za kisayansi za kukusanya ‘data’ na kutafuta ‘validity’ na ‘generalizability’ ya taarifa husika.

(ii.) Kwa jinsi mchakato ulivyo ni ngumu kusema kuwa leo tutaweza kubadili jambo nyeti kama la ‘Muundo wa Muungano’ kuwa uwe ni wa Serikali mbili, ama moja, wakati mapendekezo ya Tume, ambayo ‘yanaelezewa’ na Tume kuwa yanatokana na ‘maoni’ ya wananchi walio wengi, 61% na pili mabaraza ya katiba [cf. Muundo katika mchakato huu ni wa pyramid, kwamba unaanza na maoni ya wengi huku chini kwenye kitako, baadaye mabaraza ya katiba hapo katikati na mwisho Bunge la Katiba, kabla ya kura ya maoni]. Hivi inawezekana wapi Bunge Maalum la Katiba, kwa hapa tulipofikia, likafanya mabadiliko kwenye mambo yanayohusu ‘muundo’ (structure) wa Katiba? Yaani, kwamba inawezekana vipi wajumbe hawa 640 wabadilishe jambo zito la kimuundo kama hili? Kimantiki haingii akilini. Uhalali huo unatoka wapi? Lakini pia hapa hatuwezi kuondoa ukweli kwamba malalamiko na manung’uniko ya baadhi ya watu yana mashiko, kuwa hivi kama hoja ya Chama Cha Mapinduzi ilikuwa ni kuilinda ‘status quo’ ya muungano wa serikali mbili na kama walifanya kazi ya kuwaelimisha wanaCCM nchini, na wanaCCM walikuwa wengi zaidi kwenye mabaraza ya katiba ya wilaya [walishinda kwa zaidi ya asilimia 65, inatokeaje asilimia 61 watake muungano wa serikali 3?]

Nini tafsiri ya haya yote? Kwamba ukisema unabadili leo muundo wa Muungano ukaleta wazo tofauti na lile linalotokana na mapendekezo ya tume, kama yanavyosomeka kwenye Rasimu (sura ya 6), mfano ukasema, ziwe serikali mbili tu badala ya tatu zinazopendekezwa, maana yake unaongelea kuanza upya kutengeneza vifungu vipya vya ‘kimuundo’ vya serikali za mitaa, wawakilishi wa wananchi, mambo ya wakuu wa mikoa ama majimbo(provinces) – jambo ambalo litakuwa cumbersome! Vurugu mechi bila uwepo wa rasimu! Swali la kujiuliza hapa ni kwamba – hivi tume hawakuliona hili? Pengine wangeweka chaguzi (option) pembeni, maana maoni yote haya wanayo, ila kwa sababu ya muundo wa Muungano ‘waliouchagua’ hawakupenda kuelezea mambo binafsi ya serikali hizi ‘mbili’ za ‘iliyokuwa Tanganyika’ na Zanzibar kwa madai kwamba jukumu lao ni kuandaa rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kinachoonekana hapa ni kwamba walikwishaamua kuwa ziwepo serikali tatu kwa madai kuwa ndiyo maoni ya wananchi na kwa kuzingatia msingi wa hoja kwamba Bunge la Katiba haliwezi kuwa na uhalali wa kubadili mambo ya msingi ya kimuundo wa katiba, kama hili la Muundo wa Muungano, bali ‘kuboresha’ tu yale yaliyomo. Mtu makini atahoji kuwa ni kwa nini wamekwepa kuzungumzia ukweli kwamba ‘Tanganyika’ hayupo? Na nini itakuwa hatma ya Katiba yake? Na ni lini wabia hawa wa Muungano walikaa wakakubaliana washirikiane kwenye mambo yapi kwenye huo muungano wa Shirikisho?

Sasa wabunge wa Bunge maalum la katiba tukiukataa huu muundo wa serikali tatu nini kitatokea? Maana yake sehemu kubwa ya rasimu hii italazimika kubadilishwa.

(iii.) Jambo lingine ambalo litatusumbua ni kuwa, vipi kama wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba tukiamua tujenge msimamo kwenye hoja ya Serikali Moja itakuwaje? Maswali mengi yataibuka bila kupata majibu hapa, kuwa ni nani atakuwa ‘Mpatanishi’ kwa niaba ya Tanganyika (ama Tanzania bara)? Maana Zanzibar yupo na ana uhai wake kamili, Tanganyika yuko wapi hapa?

Mhe. Jaji Joseph Warioba na wenzake wanapaswa wajibu maswali haya:

1. Ni njia (methodology) ipi ya kisayansi na kitakwimu walitumia kufikia ‘conclusion’ hiyo madhubuti kabisa kuwa 61% ya watanzania walitaka Muundo wa Serikali Tatu? Watueleze watanzania sample size, sampling technique, sampling frame na namna walivyowafikia na kuwahoji watu hao.

2. Watueleze ni nani aliyewatuma kwenda kubadilisha Muundo wa Muungano?

3. Ni nani sasa atakuwa na mamlaka ya kuandika Katiba ya Serikali ya Tanganyika (ama Tanzania Bara – ambaye aliishakufa?), kama tukiamua kwenye Bunge la Katiba kupitisha Rasimu hii yenye Muundo wa Muungano wa Serikali tatu? Tunaanzia wapi kumfufua Tanganyika?

Maoni yangu: Mtu yeyote mpenda demokrasia ataona wazi kwamba kuna utata uliogubikwa na ukungu wa presha za kisiasa za kuona zoezi hili linakamilika. Utata wa uhalali wa Bunge la Katiba kubadili hoja za msingi kwenye rasimu ni jambo zito, na mashaka kwamba pengine Jaji Joseph Warioba na wenzake walikuwa na ajenda yao ya siku nyingi ya kuleta serikali tatu kinyume na matakwa ya Chama Tawala, CCM, ni jambo zito zaidi. Hivyo, kuondoa mamlaka na madaraka ya wananchi (kama kweli yapo kama inavyosema tume) kwenye jambo zito la kimsingi kama Muundo wa Muungano ni jambo linalotishia usalama wa mchakato na ni jambo lisilokubalika kwa kuwa linaondoa haki, wajibu, mamlaka na madaraka ya wananchi kufanya maamuzi kuhusu katiba yao (an act of popular sovereignity). Mkanganyiko huu unatia mashaka zaidi ya kuleta mwangaza wa mabadiliko ya kutokea kwa maridhiano. Jaji Warioba na wenzake walilijua hili na wameleta ‘chaos na frustration’ kwa maksudi kwa kujificha chini ya kivuli cha ‘uhalali’ wa Bunge la katiba (yaani ‘legitimacy of rule or of law is based on the consent of the governed’) na nadharia pana ya demokrasia yenye msingi kwenye kanuni za ‘popular sovereignity’ wakijua kabisa wabunge tutashindana, tutatofautiana!

Mimi nina maoni kwamba, ili mchakato uishe salama, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete aingilie kati, atumie mamlaka yake kusitisha mchakato huu mpaka itakapoundwa tume nyingine ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu suala la Muundo wa Muungano na kisha ipigwe kura maalum ya maoni kuhusiana na jambo hili ili watanzania washiriki kikamilifu na waamue na siyo kufanya maamuzi ya kubadilisha Muundo wa Muungano bila kutupa fursa ya kujadiliana na kushiriki kufanya uamuzi kuhusu jambo hili. Ni jambo lisilo na busara hata kidogo kwenda kujadili Rasimu ya Katiba bila kuwa na suluhu inayokubalika kuhusu Muundo wa Muungano wetu.

Kama kuna presha ya muda wetu wa miaka mitano kuisha kuna dirisha la kutokea; tusogeze mbele muda wa uhai wa Uongozi wa awamu hii ama turudi nyuma tufanye mabadiliko ya sehemu za katiba zinazohusiana na Tume ya Uchaguzi tu. Hatuna namna ya kukwepa moja kati ya mambo haya kwa sababu hata tukifanikiwa kufunika kombe mwanaharamu apite, tukapitisha Katiba hii, bado tutahitaji kufanya mabadiliko makubwa ya Sheria mbalimbali nay a kitaasisi kutokana na Katiba mpya itakayokuwa imepatikana, zoezi ambalo kwa kila namna litahitaji muda wa kutosha na sioni kama upo! Demokrasia ni gharama na haikwepeki!

Maswali ni mengi zaidi ya Majibu. Wasiwasi ni mwingi kuliko uhakika. Tutafika salama kwenye kupata Katiba hii kweli? Ni bora tukawie kuliko kuvurunda. Tusikimbie kwa kasi bila kutazama tuendako, tutambae lakini macho njiani na mbele tunakoelekea.

Tamko hili limetolewa na Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Nzega.

HK (Nimesaini)
Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB.

Hapo Dr umeyumba. Hivi tume ilitumwa kufanya research ama kukusanya maoni?? Hivi kila CCM anataka serikali mbili? Mpaka ushangae 61% kutaka serikali tatu? Hivi si ninyi CCM mliokuwa mnaporomosha matusi bungeni? Mkasahau kutunga sheria makini? Dr kuwa serious! Bunge la katiba si mmeshali-dominate? Sasa unahofu nini? Ama dhamira zinawasuta?
 
Hamis amepotoka....mheshimiwa jaji warioba na tume yake wamwzunguka Tanzania nzima a si sehemu ya Tanzania tu
 
...aache uchizi,wananchi wameshaamua hainakurudi nyuma...
 
Ni lini Watanzania tuliridhia japo kidogo serikali2? Pili Tanganyika hata icheleweshwe vp, ila itarudi tu!
 
Back
Top Bottom