KIGWANGALLA apendekeza Rais Asitishe Bunge Maalum la Katiba ili Kukubaliana Kuhusu Muundo Muungano!

Mjamaa yupo sawa kabisa ,sitisha hili bunge ,rudisha Tanganyika ,tengeza katiba yake ,halafu tunaingia kama tupo kamili kwa maana wahusika wote wapo hai ,Tanganyika na Zanzibar !

Inakuwaje mnaenda na maiti ,hivi mna akili timamu ? Warioba amka na waombe samahani WaTZ haraka sana ,maana jahazi ndio hilo ,Irudisheni Tanganyika japo kwa kuiweka ICU !:A S 114:
 
Kigwangala ni wale wale wenye kufikiri kwa kutumia ubongo wa kuku!

mkuu aka ka neno kako bana kamenivunja mbavu,kiualisia wana ccm hawa mpendi ndg warioba kutoka rohoni maana anataka kuwatilia kitumbua chao mchanga, ccm wanajua faida na maslai yao kisiasa juu ya muungano, ukweli ndio uo, wajibu hoja wasiwatishe watanzania,
 
Maswali kwa Muheshimiwa Kingwangwala:

"....tume ya Mhe. Jaji Warioba imepotoka..."


1. Umefikiaje hili hitimisho wakati hujui hata methodology iliyotumiwa na tume?
2. Umetumia mtazamo gani wa kisayansi katika kukosoa methodology na hitimisho lililofikiwa na tume?

"Lakini pia hapa hatuwezi kuondoa ukweli kwamba malalamiko na manung'uniko ya baadhi ya watu yana mashiko, kuwa hivi kama hoja ya Chama Cha Mapinduzi ilikuwa ni kuilinda ‘status quo' ya muungano wa serikali mbili na kama walifanya kazi ya kuwaelimisha wanaCCM nchini, na wanaCCM walikuwa wengi zaidi kwenye mabaraza ya katiba ya wilaya [walishinda kwa zaidi ya asilimia 65, inatokeaje asilimia 61 watake muungano wa serikali 3?"

Kumuelimisha mtu sio kumlazimisha afuate kile unachokitaka. Hao watanzania, uliowaita wana CCM sio "matabula rasa" kiasi hicho kiasi cha kuchukua kila wanaloambiwa kama lilivyo. Enzi hizo zinatoweka. Huenda walitumia busara za "mbayuwayu" kuwa "Za kuambiwa changanya na za kwako" na ndio maana wewe na wafananao na wewe imekuwa suprise ktk hilo na maoni ya tume.


Kwa mtazamo wangu, uliyoyatoa ni maoni yako na sidhani kama yanakidhi kiwango cha kuwa ya kisayansi kama ulivyotaka iwe. Na yanaonekana wazi kuwa ni ya "kimtego". Unataka uonekane kwa wenzako kuwa unapingana na tume na wakati huo huo unataka yaonekana yanakubaliana na maoni ya watu wengi kuhusu muundo wa muungano wa serikali tatu.

La kusitisha bunge la katiba pekee halitoshi, labda tuanze moja kwenye sheria ya mabadiliko ya katiba ambayo wewe ni miongoni mwa walioipitisha. Naungana na tume kuwa serikali tatu ni maoni ya watanzania walio wengi na sina shaka na methodology na hitimisho lililofikiwa na tume.
 
Mbona inaeleweka ata JK .alisemea hili kwenye hotuba yake sherehe za ccm miaka 37.ili ibaki serikali mbili .kunatatizo litakalo kuwepo.ambalo hapana shaka ni katiba ya Zanzibar itabidi ifanyiwe marekebisho .na kwa serikali 3 itabidi itabidi katiba ya Tanganyika itengenezwe .sasa ni nini hambacho huyu mjumbe wa bunge la katiba .ajaelewa mpaka kufikia leo siku 3 bado .bunge la katiba linaanza .!!? Huyu kweli sio mmoja wapo wa wabunge wa katiba .mzigo ?
 
Nadhani ni maoni yake na Kimsingi inaonekana yeye mtoa maoni ndiyo mwenye Utata kwa kutokuelewa hata majukumu ya Mabaraza ya Katiba ambayo Kimsingi CCM walifikiri ndiyo watakayo yatumia kuvurugha maoni ya wananchi wengi. Hili linaonekana hapa hata katika hilo bandiko lake ame comment hicho bila soni na pili anyamaze asiwe msahaulifu hawa ndo waliopiga kura za Ndiyooooooo...wakati wanaambiwa na kuelimishwa kuwa Tume ya Warioba isivunjwe kwaqnza na isubiri kukamilika kwa mchakato au mpaka mchakato utakapo kamilika .

Hili ndiyo Tatizo la kusinzia Bungeni na kuendekeza ushabiki na kupambana na hoja za wabunge wa CHADEMA na Vyama vingine vya upinzani badala ya maslahi mapana ya Taifa na kwataarifa yake asome vizuri sheria inayo waongoza hapo ilipofika unga umekwisha mwagika aendelee mbele na upuuzi wao Mwingine wa ndiyoooooo wakati wa Bunge la Katiba.
 
Sioni sababu ya kumpinga huyu mr. Kuna vitu vya msingi kavigusa na kwa sasa hatuwezi viona ila bunge likianza tutaona na kugundua makosa yalipotokea. Pia kama wananchi wengi walishapendekeza serikali tatu kuna haja gan ya kwenda kujadili tena kipengele hiki? Si wengi washaamua?
 
Kwa hili,nakuunga mkono,hizi haraka zinaweza kuzaa katiba mbovu,waliowengi kwenye hilo bunge la katiba ni CCM na ndiyo wanataka serikali mbili,watanzania wengine waliobaki ni mbumbu mzungu wa reli,swala likirudi kwa wanachi hili,maoni ya serikali mbili ndiyo yatakayopita ili mradi yamepita kwa CCM.Jiulizeni kama ile tume ilipita vijijini na wakapata maoni juu ya muungano,haya maoni ya serikali tatu ni ya wanasiasa na si ya watu wote.
 
Dr.Kigwangalla anayaona haya LEO??? Kweli wonders shall never End.Alivyokuwa anaporomosha matusi kule bungeni alidhani ATASHINDA??? Anasema watu wengi eti WANAMUULIZA kuhusu muundo wa Muungano.Hivi mtu na akili zake atafute ushauri kwa Kigwangalla???! Hana jipya ni mtu wa kujisifia tu.Tumeshuhudia, ametafuta sifa kwa mambo mengi sana, ila yote kashindwa.Huyu ni nadhani ndiye daktari wenye upeo mdogo kuliko wote (nadhani).Ilifika wakati watu walianza kulihusisha jina la "khamis" na ka-hali fulani ka-kupungukiwa akili.Mtanisamehe wale wenye jina hili"khamis" ila mwenzetu anawatia AIBU sana.Unataka upewe"methodology" iliyotumika kutaka serikali tatu!! Njia iliyotumika ni "MAONI" ya wananchi, on random SAMPLE basis!!! Haturajii wananchi WOTEEEEEE 45 Milioni wahojiwe.Ni random sample tu.Hoja ya MUUNDO wa serikali ndugu HAIBADILIKI.Usanii huu wa kuja humu jamvi na hoja za kijinga, uache, humu kuna watu Intellectuals.Ni bahati mbaya siku hizi kuna mamluki wengi wameingia kwa IDs tofauti tofauti lakini ukisoma kwa makini utagundua ni mtu mmoja ambaye mjinga(si tusi hili).
 
Huyu Kigwangala sio mtanzania nakumbuka alipowekewa pingamizi akasaidiwa na familia ya kikwete kwa vile ndiye dk wa familia ya kikwete! sasa anataka mchakato huu uharibike kwani hata kwa akili ya kawaida yeye anazaungumzia sera za ccm wakati hii ni katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kwa akili yake anakili Zanzibar ni hai na wamekuwa hai zaidi kwa kuvunja katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania walipotunga yao 2010 na huyu anayemuomba asitishe mchakato alikuwepo akawacha na akashindwa kulinda katiba aliyoapa kuilinda!kuanzia hapo Kikwete ni dhaifu sana na hafai kuendelee kuwa rais naye Kigwangala asifikiri sasa yuko anashi....ya S... akiwa uchi! maana huyu ni dk wa magonjwa ya akina maama!
 
Katika Ukurasa wake wa facebook Mhe Kigwangalla ameandika muda si mrefu:


TAMKO LANGU KWA UMMA KUHUSU MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Ndugu wanahabari na waTanzania wenzangu,


Nimekuwa nikilazimika kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wanahabari, ndugu, jamaa na marafiki kuhusiana na namna mchakato wa kuandika katiba mpya ya Taifa letu unavyoenda; wengi wakipenda kujua nini mtazamo wangu kuhusu mambo mengi, haswa hili la serikali mbili ama tatu kwenye muungano wetu. Mara nyingi nimekuwa nikikwepa kusema msimamo wangu ni nini kwa sababu niliona ni vema nikajipa muda wa kutafakari kabla ya kuamua kujenga msimamo yangu. Ila kwa kuwa wakati wa kwenda Bungeni umefika na mimi nimepata bahati ya kuwa miongoni mwa wajumbe wa Bunge hili la kihistoria nimeona leo nitoe mtazamo wangu.


Kwanza, nianze kwa kuonesha wasiwasi wangu kama tutaweza kufika salama huko tuendako. Si kwa sababu za kitabiri kama mnajimu, la, ni kwa sababu za kisayansi, ambazo nitaziweka wazi hapa kama ifuatavyo:


(i.) Pamoja na kwamba tume imefanya kazi nzuri ya kukusanya maoni na kuyaweka katika nyaraka ambayo tutapaswa kuifanyia kazi, napata shida kama walikuwa makini katika kuendesha zoezi hili. Kivipi, binafsi napata shida na methodology iliyowawezesha kufikia ‘conclusion' madhubuti kwamba watanzania asilimia 61 walitaka serikali tatu. Kwa sababu za kisayansi naona tume ya Mhe. Jaji Warioba imepotoka na kwamba kusema hivyo ni kutaka kulazimisha uhalali wa hoja hii nyeti kwenye dokumenti ya Rasimu ya Katiba tunayopaswa kuipitisha bila kuwa na msingi wa kitakwimu unaotokana na njia (methodology) za kisayansi za kukusanya ‘data' na kutafuta ‘validity' na ‘generalizability' ya taarifa husika.

(ii.) Kwa jinsi mchakato ulivyo ni ngumu kusema kuwa leo tutaweza kubadili jambo nyeti kama la ‘Muundo wa Muungano' kuwa uwe ni wa Serikali mbili, ama moja, wakati mapendekezo ya Tume, ambayo ‘yanaelezewa' na Tume kuwa yanatokana na ‘maoni' ya wananchi walio wengi, 61% na pili mabaraza ya katiba [cf. Muundo katika mchakato huu ni wa pyramid, kwamba unaanza na maoni ya wengi huku chini kwenye kitako, baadaye mabaraza ya katiba hapo katikati na mwisho Bunge la Katiba, kabla ya kura ya maoni]. Hivi inawezekana wapi Bunge Maalum la Katiba, kwa hapa tulipofikia, likafanya mabadiliko kwenye mambo yanayohusu ‘muundo' (structure) wa Katiba? Yaani, kwamba inawezekana vipi wajumbe hawa 640 wabadilishe jambo zito la kimuundo kama hili? Kimantiki haingii akilini. Uhalali huo unatoka wapi? Lakini pia hapa hatuwezi kuondoa ukweli kwamba malalamiko na manung'uniko ya baadhi ya watu yana mashiko, kuwa hivi kama hoja ya Chama Cha Mapinduzi ilikuwa ni kuilinda ‘status quo' ya muungano wa serikali mbili na kama walifanya kazi ya kuwaelimisha wanaCCM nchini, na wanaCCM walikuwa wengi zaidi kwenye mabaraza ya katiba ya wilaya [walishinda kwa zaidi ya asilimia 65, inatokeaje asilimia 61 watake muungano wa serikali 3?]

Nini tafsiri ya haya yote? Kwamba ukisema unabadili leo muundo wa Muungano ukaleta wazo tofauti na lile linalotokana na mapendekezo ya tume, kama yanavyosomeka kwenye Rasimu (sura ya 6), mfano ukasema, ziwe serikali mbili tu badala ya tatu zinazopendekezwa, maana yake unaongelea kuanza upya kutengeneza vifungu vipya vya ‘kimuundo' vya serikali za mitaa, wawakilishi wa wananchi, mambo ya wakuu wa mikoa ama majimbo(provinces) – jambo ambalo litakuwa cumbersome! Vurugu mechi bila uwepo wa rasimu! Swali la kujiuliza hapa ni kwamba – hivi tume hawakuliona hili? Pengine wangeweka chaguzi (option) pembeni, maana maoni yote haya wanayo, ila kwa sababu ya muundo wa Muungano ‘waliouchagua' hawakupenda kuelezea mambo binafsi ya serikali hizi ‘mbili' za ‘iliyokuwa Tanganyika' na Zanzibar kwa madai kwamba jukumu lao ni kuandaa rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kinachoonekana hapa ni kwamba walikwishaamua kuwa ziwepo serikali tatu kwa madai kuwa ndiyo maoni ya wananchi na kwa kuzingatia msingi wa hoja kwamba Bunge la Katiba haliwezi kuwa na uhalali wa kubadili mambo ya msingi ya kimuundo wa katiba, kama hili la Muundo wa Muungano, bali ‘kuboresha' tu yale yaliyomo. Mtu makini atahoji kuwa ni kwa nini wamekwepa kuzungumzia ukweli kwamba ‘Tanganyika' hayupo? Na nini itakuwa hatma ya Katiba yake? Na ni lini wabia hawa wa Muungano walikaa wakakubaliana washirikiane kwenye mambo yapi kwenye huo muungano wa Shirikisho?

Sasa wabunge wa Bunge maalum la katiba tukiukataa huu muundo wa serikali tatu nini kitatokea? Maana yake sehemu kubwa ya rasimu hii italazimika kubadilishwa.

(iii.) Jambo lingine ambalo litatusumbua ni kuwa, vipi kama wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba tukiamua tujenge msimamo kwenye hoja ya Serikali Moja itakuwaje? Maswali mengi yataibuka bila kupata majibu hapa, kuwa ni nani atakuwa ‘Mpatanishi' kwa niaba ya Tanganyika (ama Tanzania bara)? Maana Zanzibar yupo na ana uhai wake kamili, Tanganyika yuko wapi hapa?

Mhe. Jaji Joseph Warioba na wenzake wanapaswa wajibu maswali haya:

1. Ni njia (methodology) ipi ya kisayansi na kitakwimu walitumia kufikia ‘conclusion' hiyo madhubuti kabisa kuwa 61% ya watanzania walitaka Muundo wa Serikali Tatu? Watueleze watanzania sample size, sampling technique, sampling frame na namna walivyowafikia na kuwahoji watu hao.

2. Watueleze ni nani aliyewatuma kwenda kubadilisha Muundo wa Muungano?

3. Ni nani sasa atakuwa na mamlaka ya kuandika Katiba ya Serikali ya Tanganyika (ama Tanzania Bara – ambaye aliishakufa?), kama tukiamua kwenye Bunge la Katiba kupitisha Rasimu hii yenye Muundo wa Muungano wa Serikali tatu? Tunaanzia wapi kumfufua Tanganyika?

Maoni yangu: Mtu yeyote mpenda demokrasia ataona wazi kwamba kuna utata uliogubikwa na ukungu wa presha za kisiasa za kuona zoezi hili linakamilika. Utata wa uhalali wa Bunge la Katiba kubadili hoja za msingi kwenye rasimu ni jambo zito, na mashaka kwamba pengine Jaji Joseph Warioba na wenzake walikuwa na ajenda yao ya siku nyingi ya kuleta serikali tatu kinyume na matakwa ya Chama Tawala, CCM, ni jambo zito zaidi. Hivyo, kuondoa mamlaka na madaraka ya wananchi (kama kweli yapo kama inavyosema tume) kwenye jambo zito la kimsingi kama Muundo wa Muungano ni jambo linalotishia usalama wa mchakato na ni jambo lisilokubalika kwa kuwa linaondoa haki, wajibu, mamlaka na madaraka ya wananchi kufanya maamuzi kuhusu katiba yao (an act of popular sovereignity). Mkanganyiko huu unatia mashaka zaidi ya kuleta mwangaza wa mabadiliko ya kutokea kwa maridhiano. Jaji Warioba na wenzake walilijua hili na wameleta ‘chaos na frustration' kwa maksudi kwa kujificha chini ya kivuli cha ‘uhalali' wa Bunge la katiba (yaani ‘legitimacy of rule or of law is based on the consent of the governed') na nadharia pana ya demokrasia yenye msingi kwenye kanuni za ‘popular sovereignity' wakijua kabisa wabunge tutashindana, tutatofautiana!

Mimi nina maoni kwamba, ili mchakato uishe salama, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete aingilie kati, atumie mamlaka yake kusitisha mchakato huu mpaka itakapoundwa tume nyingine ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu suala la Muundo wa Muungano na kisha ipigwe kura maalum ya maoni kuhusiana na jambo hili ili watanzania washiriki kikamilifu na waamue na siyo kufanya maamuzi ya kubadilisha Muundo wa Muungano bila kutupa fursa ya kujadiliana na kushiriki kufanya uamuzi kuhusu jambo hili. Ni jambo lisilo na busara hata kidogo kwenda kujadili Rasimu ya Katiba bila kuwa na suluhu inayokubalika kuhusu Muundo wa Muungano wetu.

Kama kuna presha ya muda wetu wa miaka mitano kuisha kuna dirisha la kutokea; tusogeze mbele muda wa uhai wa Uongozi wa awamu hii ama turudi nyuma tufanye mabadiliko ya sehemu za katiba zinazohusiana na Tume ya Uchaguzi tu. Hatuna namna ya kukwepa moja kati ya mambo haya kwa sababu hata tukifanikiwa kufunika kombe mwanaharamu apite, tukapitisha Katiba hii, bado tutahitaji kufanya mabadiliko makubwa ya Sheria mbalimbali nay a kitaasisi kutokana na Katiba mpya itakayokuwa imepatikana, zoezi ambalo kwa kila namna litahitaji muda wa kutosha na sioni kama upo! Demokrasia ni gharama na haikwepeki!

Maswali ni mengi zaidi ya Majibu. Wasiwasi ni mwingi kuliko uhakika. Tutafika salama kwenye kupata Katiba hii kweli? Ni bora tukawie kuliko kuvurunda. Tusikimbie kwa kasi bila kutazama tuendako, tutambae lakini macho njiani na mbele tunakoelekea.

Tamko hili limetolewa na Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Nzega.

HK (Nimesaini)
Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB.


Kwanza nakupongeza kwa uchambuzi wako, wewe ni miongoni mwa watu wachache wanaojitokeza waziwazi kueleza misimamo yao katika mambo nyeti kama haya.

Sasa turudi kwennye hoja, Kingwangwala ukisoma pale kwenye red utaweza kuona ni jinsi gani nyie watu wa CCM mnavyopenda kujisahihishia mitihani na kujipa maksi za uongo na kushangilia kama mazuzu. kwenye mabarza ya katiba si wana CCM wengi waliochaguliwa, upinzani ulitoa watu wengi. Tatizo likawa wale waliochaguliwa nikiwemo mimi kutoka katika kijiji kimoja hapa nchini tulienda ngazi ya mchujo katani kwenye mabarza ya WDC ambayo yametawaliwa na wenyeviti wa CCM. Hapo ndipo wale tuliopitishwa na wananchi tulipopigwa panga na wana CCM tu ndiyo waliosalimika. Endapo wale tuliochaguliwa na wananchi tungekwenda moja kwa moja wilayani hizo takwimu unazotoa zisingekuwa hivyo. Bungeni uliibuka mjadala mkali lakini kwa wingi wa wabunge wa CCM ikapitishwa kuwa mchujo ngazi ya WDC ili kuwabakiza CCM ni lazima. Hoja yako ni nzuri, ukiacha pale kwenye red.
 
Tamko kwa wanahabari linatolewa FACEBOOK duh! kaaazi kwelikweli.na hii inanikumbusha yale matamko ya wale wenyeviti wa CDM wa mikoa waliyokuwa wakiyatoa baada ya ZITTO kuvuliwa vyeo.
 
Duniani kote ukisikia muungano maana yake serikali moja ss hii serikali 3 sijapata kusikia ila wale wanaong"ang'ania serikali 3 lengo ni kuelekea kuuvunja muungano,wale wanaotakata serikali 2 nao lengo lao nao nikuendelea kubaki madarakani suluhisho ni serikali 1 kama haiwezekani kila mtu achukue inchi yake bac.kigwangala anapiga blabla 2 hana jipya.
 
Huyu nae hajui cho chote kuhusu reseach, anabwabwaja tu. Alitaka watu wote nchini 45 mil waulizwe?

aisee! Sijui tatizo ni uelewa au maji ya bendera waliyokunywa! Mbona hili suala liko wazi tu, na wengi twafurahi Tanganyika irudi? Au hawa jamaa wanafurahia nchi jirani kututukana kila wakati? Nina hofu kubwa sana na hawa wabunge wa CCM. Wazanzibar mnaombwa kukomalia hili suala la serikali 3, huenda ikawaingia.
 
Nadhani ni maoni yake na Kimsingi inaonekana yeye mtoa maoni ndiyo mwenye Utata kwa kutokuelewa hata majukumu ya Mabaraza ya Katiba ambayo Kimsingi CCM walifikiri ndiyo watakayo yatumia kuvurugha maoni ya wananchi wengi. Hili linaonekana hapa hata katika hilo bandiko lake ame comment hicho bila soni na pili anyamaze asiwe msahaulifu hawa ndo waliopiga kura za Ndiyooooooo...wakati wanaambiwa na kuelimishwa kuwa Tume ya Warioba isivunjwe kwaqnza na isubiri kukamilika kwa mchakato au mpaka mchakato utakapo kamilika .

Hili ndiyo Tatizo la kusinzia Bungeni na kuendekeza ushabiki na kupambana na hoja za wabunge wa CHADEMA na Vyama vingine vya upinzani badala ya maslahi mapana ya Taifa na kwataarifa yake asome vizuri sheria inayo waongoza hapo ilipofika unga umekwisha mwagika aendelee mbele na upuuzi wao Mwingine wa ndiyoooooo wakati wa Bunge la Katiba.
Wananchi gani unaowasemea wewe,unajua watu wengi humu jf mnaangalia nani kaleta mada humu,kama CCM basi wale wasio upande wake ni kupinga bila kutoa suluhisho,kama ni CDM basi,wasiokuwa chama hicho watashupaza shingo zao bila kuangalia uzuri wake wala ubaya wake,em jaribuni kubadilika na muwe na mitazamo chanya.Madhara ya kuvunja Muungano ni makubwa kuliko nyie mnavyofikilia,jifunzeni kwa Kenya,leo meri zote zinazoingia kenya lazima zipitie Tanzania mnajua kwa sababu gani? Kenya hawako kwenye Muungano wanaathiriwa na nchi ya Somalia,sababu mnazijua,mkivunja Muungano na Zanzibar,mtaathiri nchi zote za Afrika mashariki kiuchumi,mwenye akili na atazame,kwanini meri za kwenda Kenya lazima zipitie Tanzania?Sio kukurupuka na kupinga kila kitu.
 
Suluhu ya yote ni serikali moja...SMZ ipotee na Tanganyika isirudi....Na tukishafanya hivyo...hakuna kuchaguana kwa kuangalia huyu katoka sehemu gani ya Tanzania...Watanzania tukiona Rais, makamu, waziri mkuu, spika na Mwanasheria Mkuu, Jaji mkuu Mkuu wa majeshi na wengine kama hao ,kwenye serikali moja ya Tanzania, wanatoka Mkoa wa Pemba, ama wilaya moja ya Magu ama vyovyote...wala tusihoji ili mradi wanaweza kututoa hapa tulipo...na kutupeleka kwenye Tanzania yenye maendeleo ya viwanda ya kweli huku wananchi wote wakiwa na fursa ya kujiari ama kuajiriwa kwenye viwanda hivyo.
 
Mimi nafikiri,serikali moja ndiyo mwisho wa matatizo,hakuna kuweka 2 wala 3.Hakuna haja ya kupoteza pesa nyingi kwa maslahi ya wanasiasa,ukiweka serikali tatu huyo Rais wa muungano atafanya kazi gani kama sio kutumia pesa bila sababu za msingi.Ndugu zangu tusifanye propaganda kwenye hili,tutakuja juta na kuja kuibadili tena hiyo katiba itatugharimu.
 
maswali ya mhe. kingwangwala,

1. Ni njia (methodology) ipi ya kisayansi na kitakwimu walitumia kufikia ‘conclusion' hiyo madhubuti kabisa kuwa 61% ya watanzania walitaka Muundo wa Serikali Tatu? Watueleze watanzania sample size, sampling technique, sampling frame na namna walivyowafikia na kuwahoji watu hao.

2. Watueleze ni nani aliyewatuma kwenda kubadilisha Muundo wa Muungano?

3. Ni nani sasa atakuwa na mamlaka ya kuandika Katiba ya Serikali ya Tanganyika (ama Tanzania Bara – ambaye aliishakufa?), kama tukiamua kwenye Bunge la Katiba kupitisha Rasimu hii yenye Muundo wa Muungano wa Serikali tatu? Tunaanzia wapi kumfufua Tanganyika?

majibu:
1. wakati wa kuanndika rasimu ya kwanza wananchi walipendekeza mfumo wa serikali na video zipo mkitaka mtapewa bungeni na kati ya hao waliosema wanataka serikali ya tatu ni asilimia 61.
kuhusu hoja yako ya mabaraza ya katiba kwamba wengi ni wana ccm that's is nonesense kwani kwenye rasimu ya pili hoja haikuwa uwingi wa watu bali ni uzuri wa hoja kurekebisha kile kilicholetwa na rasimu ya kwanza kutoka kwa wananchi na wana ccm walioulizwa kuhusu hoja za kupinga serikali majibu yao yalikuwa dhaifu kwani walikuwa wakisoma mavitabu waliyopewa na ccm kinyume na utaratibu wa kupata maoni kutoka kwa wahusika wenyewe na sio watu wengine.

2. muungano upo ndani ya katiba kwenye page ya mwisho ya katiba na unaposema unakwenda kutengeneza katiba mpya ina maana kila kilichokuwepo ndani ya katiba ni fair game kwahiyo huwezi kumkabidhi mtu chumba cha kulala na baadaye nani amekupa ruhusa kulala kitandani it is a part of the package huwezi kudai unataka katiba mpya huku ukichagua kipi kisijadiliwe huo utakuwa usulutani. kama ulikuwa na kipengele kinachosema muungano usijadiliwe kitoe ??

3. Tanganyika ni watu na siyo viongozi au wabunge. watanganyika wenyewe wapo tena wengi kuliko wa mwaka 1961 kwahiyo wanaweza kujadili katiba yao bila wasiwasi kwani katiba bora utokana na watu na watu wenyewe ni watanganyika wapo. kumfufua Tanganyka ni rahisi kwani katiba ikishaundwa na watanganyika wenyewe uchaguzi ukaitishwa Tanganyika imefufuka unataka nini tena kilichobakia ni utekelezaji tu.
 
Kwakuwa ni wewe muheshimiwa umeanzisha thread hii, ni matumaini yangu kuwa utaipitia hapo baadae! Hivi WaTanganyika mbona naona kama mna kasoro? Upande mmoja uko huru kupigania maslahi yao, huku nyinyi akina muheshimiwa mnaona kama ni dhambi kupigania maslahi ya watu wenu? Mmelogwa?
 
Hawa ndio ma dk. Watu uwa hawaoni taabu wala aibu kuweka pembeni degrees zao na kuanza kuandika utumbo wa kisomi kwa nia moja tu kutetea maslahi yao ya kisiasa
 
Sasa jamani hivi hawa ndio wanaenda eti kujadili rasimu mbona hatari sana! Umeuliza very awkward questions kama vile mwanafunzi wa sekondari. Methodology naona umekazania neno hilo sana, hivi unajua maana yake kweli wewe! Huyu nafikiri ameandika hili TAMKO akiwa na viroba kama kumi kichwani...

Nini cha ajabu 61% kutaka serikali tatu? Kama upo makini hata wewe mwenyewe leo hii chukua watu kumi na waulize maswali MAZURI kuhusu MUUNGANO na mapendekezo kuwa na serikali ngapi kama hujapata wote wakisema serikali tatu..

Mimi binafsi naamini Tume kwani uliundwa na watu WASOMI WABOBEVU katika sio tu UTAFITI bali hata SIASA. WEWE NI DAKTARI haya ya UTAFITI na kuuliza maswali magumu tuachie sisi TUNAOJUA PLEASE.

Your analysis is CLUMSY, INEPT and CHILDISH, full of sweeping OVERGENERALIZATION

Nafikiri wewe unayesema kuwa UNAJUA ndiyo haujui kabisa. Daktari ameuliza swali nzuri kabisa ambalo kama ungekuwa unajua ungejibu na watu tungekuelewa. Katika utafiti wowote ni lazima ueleze ni njisi ngani ulivyofikia uamuzi wa kuchukua idadi fulani ya watu/vitu (sample size) ili kuwakilisha idadi kubwa ya watu/vitu (general population) na hii ni sehemu ya methodology na kuna fomula zake siyo swala la kaamua tu kama wewe ulivyosema hapo juu kuwa uliza watu kumi. Ulichotakiwa kutueleza kama kweli unajua ni kanuni gani tume ya warioba ilitumia ili kupata sample size ya watanzania waliohojiwa kuhusu muudo wa muungano inayowafaya waje na majumuisho ya asilimia 61 kama watu waliokubali muundo wa serikali tatu. Utafii wowote hauwezi kukubalika kisayansi kama sample size ilikuwa ni ndogo sana kulinganisha na general population unless kuna sababu za msingi za kushindwa kupata sample size ya kutosha na sababu lazima zielezwe. USIKIMBILIE KUTUKANA JIBU HOJA KISAYANSI.
 
Back
Top Bottom