Kigwangalla aitwa na kamati ya maadili na maandamano yake kusitishwa na CCM, yeye asisitiza yapo!!

Anayetaka kuja kugombea Nzega aje, kwa chama chochote, maana kila mtu ana haki ya kugombea kadri anavyoona inafaa - ndo demokrasia hiyo! Sijui utaratibu wa kugombea Ubunge 2015 utakuwaje, maana hatujui nini kitakuja na Katiba mpya...hivyo kuna wengine wanaweza kugombea kupitia vyama, wengine wakawa wagombea binafsi, ama pengine utaratibu ukawa ni ule wa proportional representation ampao kunakuwa na closed list ya chama...tusubiri tu
Big up Mh HK, this is how the young MP is supposed to act. This is in the name of democracy, hakuna haki miliki ya jimbo hata kama una fedha kiasi gani au unatoka chama gani. Mbunge unatakiwa kuwa karibu na wananchi kuliko chama na kama katiba mpya itakuwa ya haki na chama chenu hakitaichakachua utarudi bungeni next term kwa kura nyingi zaidi huku Selelii na Bashe wakiishia kunawa
 
HKigwangala hommie hebu nijuze kwa kifupi tu malengo ya maandamano na sehem ya mkutano/maandamano. Ili niweze changia vzur
 
... Dr. Kigwa ameonyesha ujasiri mkubwa wa kuwatumikia wananchi wake bila kujali chama chake kinataka nini..

...Dr. Kigwa anajiunga na timu ya kina Deo Filikunjombe kusimama kuhesabiwa na 2015 ataendelea kuwa mbunge wa Nzega kwa sababu ameweza kuona mbali!.
.

Pasco, naweza kuelewa mtihani uliowakuta wabunge wa CCM kuhusu 70 signatures. Maana kupitia signature tunakuwa tumechora mstari, nani ana imani na utendaji wa serikali na nani hana imani? Jina la Deo Filikunjombe lipo upande wa wale walionesha kutokuwa na imani na utendaji wa serikali na ndio maana wakatumia kanuni za bunge dhidi ya waziri mkuu. CCM kama chama kilitoa maagizo mengine, lakini wakina Deo Filikunjombe walienda kinyume.

Sasa leo unataka tuamini Dr Kigwa yuko upande mmoja na Deo Filikunjombe kwa vipi? We are dealing with facts, jina la Kigwa ni number ngapi kwenye orodha ya 70 signatures? Kwa maneno mengine Dr Kigwa anataka kuikosoa serikali ipi? Amekosa imani na serikali tangu lini?

Dr. Kigwa ana mtihani mkubwa sana. Anatakiwa akae chini na kutengeneza mikakati yake bila kutumia the same political fabric zilimuingiza madarakani. Hii ni kwa sababu siasa za Tanzania na hasa siasa za CCM kwa sasa ni tofauti sana na siasa za 2010. Hata yale makundi ya 2010 si wamoja tena. Akiweza kulitambua hili basi anaweza kupiga hatua. Haya maandamano anayosema ni 2nd attempt, anatakiwa awe makini, maana akishindwa kuyafanya political capital yake itapungua kwa kiasi kikubwa. Na naweza kusema alitakiwa apime (kwa hali ya sasa ndani ya ccm) kama kweli maandamano ni the most realistic approach anayeweza kuchukuwa ili kupata results.

Kwa nini kwa mfano asitafute namna na kuunganisha nguvu na wabunge wa Tabora ili waje na mkakati wa kutetea maslahi ya Tabora kwa pamoja? Just becuase maandamano ya CHADEMA yanaleta results it does not mean CCM au mwana-CCM anaweza ku-copy & paste na akapate the same results!
 
Labda sijaelewa

Hivi Kigwa anaitisha maandamano kwa ajili ya watu wa ccm au watu wa jimbo lake?? naona kama sio fair ccm kuvalia njuga mwakilishi wa wanachi wote
 
Anayetaka kuja kugombea Nzega aje, kwa chama chochote, maana kila mtu ana haki ya kugombea kadri anavyoona inafaa - ndo demokrasia hiyo! Sijui utaratibu wa kugombea Ubunge 2015 utakuwaje, maana hatujui nini kitakuja na Katiba mpya...hivyo kuna wengine wanaweza kugombea kupitia vyama, wengine wakawa wagombea binafsi, ama pengine utaratibu ukawa ni ule wa proportional representation ampao kunakuwa na closed list ya chama...tusubiri tu

Mkuu Dr Kigwangalla hivi unafikiri matokeo ya hayo maandamano itakuwa nini? unafikiri yatasaidia kuibadilisha serikali hii ambayo siyo sikivu Mimi nafikiri dawa ni kukomaa nao huko huko bungeni tuu
 
Hapo hauko sahihi. Tafsiri yako si sahihi kabisa. Siku zote mimi hufanya kazi zangu bila unafiki, nasema kweli hata kama itanipunguzia umaarufu kwenye kundi fulani, nasema kweli hata kama itanimaliza, period!
mkuu wewe ni mnafiki.... na unalitumia hilo neno vibaya (in most of your comments hulitumia kama defense shield)

viashiria vipo vingi tu, lakini kwa sasa tunasubiri kama utaandamana au la, usipoandamana basi unafiki utakua umepiga camp
 
Nauliza tu! hivi HKigwangalla alimwaga wino wake katika karatasi ya Zitto kuhusu kumng'oa PM? jamani nauliza tu.

Na iwapo hakumwaga wino anapata wapi haki ya kuitisha maandamano kwa issue ndogo na huku akijaribu kupingana na chama chake ngazi ya wilaya. Kwa ujumla huyu Daktari wa watu mwenye kashfa ya kutokuwa raia ni MUHUNI tu.

Ndimi Bazazi!
 
Last edited by a moderator:
HKigwangalla acha uongo na wewe alokutuma pia acheni uongo na wala usitafute umaarufu kwa kupitia maandamano yasokua na tija kwa wana nzega kiufupi nakupa habari za uhakika kwani mie nipo familia na mazingira ya wana nzengo, hakuna anaetambua maandamano yako.

Labda uje na hao magamba wenzako muandamane wenyewe ila wananchi hatutaki kabisa kuskia mambo yako.
 
Last edited by a moderator:
Huyo mbunge wako muongo kwani kaanza leo kuitisha maandamano? Hii ya tatu lakini huwa anaandama toka facebook mpaka kwenye comment yanakua yameisha. Hoja zake hazina msingi, maneno mengi.
 
Kigwangalla acha uongo na wewe alokutuma pia acheni uongo na wala usitafute umaarufu kwa kupitia maandamano yasokua na tija kwa wana nzega kiufupi nakupa habari za uhakika kwani mie nipo familia na mazingira ya wana nzengo,hakuna anaetambua maandamano yako.labda uje na hao magamba wenzako muandamane wenyewe ila wananchi hatutaki kabisa kuskia mambo yako.
wewe ni mtu mmoja tu na wala haulazimishwi kuja kuandamana na sisi. Na hatutegemei kuwa na watu wengi sana wasio na tija, tunataka watu wenye kuamini katika movement yetu na siyo kila mtu
 
Sijawahi kuomba kura za kuchaguliwa kuwa Waziri wala sijawahi ku-lobby nipewe Uwaziri. Usipoteze muda wako kudhani kuwa niliwahi kuutamani sana Uwaziri na hata kufikia kuuomba kwa wakubwa, sijawahi hata siku moja. Wakiniona nafaa nitakuwa tayari kutoa mchango wangu, wakiniona sitoshi wataniweka benchi. Na ndiyo maana sijawahi kubadili staili yangu ya siasa ninazofanya hata siku moja. Nashangaa kilamtu kunisema kuwa nitakuwa Waziri, mara Naibu Waziri inatoka wapi. Mimi ni Mbunge, niliutamani na kuutafuta Ubunge na nikaupata na kwa sasa ndiyo kazi yangu ninayofanya, nimeacha biashara, nimeacha kutoa ushauri wa kitaalamu kwa muda sasa, nafanya kazi ya utumishi wa wananchi kama Mbunge, na ninaendelea na masomo yangu ya Ph.D na utafiti kama kawaida!
Huna haja ya kushangaa ni kwa nini wengi tulidhani lazima ungeukwaa uwaziri, sababu ni moja tuu, mule bungeni ni wabunge wa CCM wachache sana wenye genuine CV za Dr. wa ukweli. Wengi wa Dr. walioko CCM wakiwemo mawaziri, u Dr. wao ni fake, kwa vile wewe ni miongoni mwa hao genuine wachache, watu wamekuwa na very high expectation on you na kiukweli JK alipata shida sana kutafuta mawaziri wapya miongoni mwa wabunge wenu, alikosa kabisa na kulazimika kukopa hata kwa kuvunja katiba ili mradi bora liende!.

Majaaliwa ya CCM kwa 2015 yako mikononi mwenu nyinyi vijana ama chama chenu kibadilike na kukubali kuwatumikia wananchi, ama king'ang'anie ku maitain status quo, wananchi wakiache rasmi na kupeleka matumaini yao kwenye tumaini jipya.

Naamini hili JK ameliona, na amini nawaambia kuliko kuwapoteza watu kama nyinyi, mtavutwa karibu kabla ya 2015!.
 
mbona una chuki sana na kigwangallah wewe? hii ni mara ya pili na-post hapa habari zinazomhusu huyu jamaa na wewe huibuka na negativity zako, una nini?


Dogo usilazimishe watu wampende mtu, jenga hoja za msingi apendwe, kama anakununulia unga na nguo ya mkeo/mmeo si wote wanaweza kununuliwa kirahisi. Hata mimi simpendi, ni mjinga sana, na huo udokta wake hafikiri unafaa kuchungia ng'ombe tu.
huyu kingwangallah hana maana kabisa, unakumbuka katika sakata la kumng'oa waziri mkuu! aliibuka na hoja ya kipuuzi kabisa kutuaminisha ujinga wake wa kwanini hakusaini azimio la kumpinga PM, inaonekana alikuwa anategemea uwaziri au unaibu, sasa katoswa anaanza kuleta hojz zisizokuwa na mashiko
imekula kwake, ukitenda dhuluma tegemea kudhumiwa, maana hakupata ubunge kihalali baada ya kuwachakachua Selelii, na Bashe, sasa dhambi ya ubaguzi inawatafuna. Nyerere kaisha sema ni sawa na kula nyama ya Mtu
nyinyiem sisiCDM
 
Gamba ni gamba tu na asipovua Gamba akavaa Gwanda, kelele zake zitakuwa tu kelele za chura!

Aaaaaaaaaaaaaaah, Kigwangala, hakuna kitu hapo jamani, huyo sawa na Nepi Nnauye, alishasema utakataje tawi la mti ulilokalia? Kiukweli sina imani kabisa na hicho anachosema Kigwa, kama Chama Chake wanamkataza anatakiwa aheshimu kama alivyosema wakati wa saini za Zitto, ukiwa mnafiki wakati wa ujana, ukifikia uzee utakuwa mchawi!
 
Even if huwa siwapendi wanafiki kama ninyi type ya shibuda but sina jinsi maana hili linahusu mkoa wangu wa Tabora.

Go.........kigwangallah.
 
Yaani CCM ina viongozi wa wilaya wasioweza hata kuandika sentensi sahihi za kiswahili?!!!! Walimu wa Kiswahili wana kazi...
 
Back
Top Bottom