Kigoma: Wanafunzi 4 wazama mto Luiche wakivuka kwenda shule. Miili 2 yapatikana kati ya watoto 4 waliozama

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Watoto wanne wamepotea kwa kuzama katika mto Ruiche na wengine wawili kuokolewa baada ya mtumbwi uliokuwa umewabeba kupinduka na kuzama katika mto huo uliopo Kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Watoto hao walikuwa wakielekea shule ya msingi Kagera, ambapo hulazimka kuvuka ng'ambo ya pili ya mto kwa kutumia mtumbwi ambapo nahodha alizidiwa nguvu kutokana na mto huo kujaa maji.

======
images
Wanafunzi wanne wa Shule ya misingi Kagera iliyopo Manispaa ya Kigoma ujiji Mkoani Kigoma wanasadikiwa kufariki baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kuvuka katika Mto Luiche kuelekea Shuleni kuzama.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Kigoma Inspekta Jacob Chacha amethitibisha kutokea kwa tukio hilo majira ya saa moja na nusu asubuhi ambapo licha ya kufanya msako wa uokozi lakini bado miili ya Wanafunzi hao haijapatikana.

Tangu majira ya saa moja na nusu asubuhi ya leo wakati tukio hilo linatokea mpaka hivi sasa licha jitihada za uokozi kufanywa na Askari wa Zimamoto na Uokoaji bado miili hiyo haijaonekana kwani Mto huo hupeleka maji yake katika Ziwa Tanganyika.

Wananchi wameeleza matukio ya vifo ya Watu kutokana na kuzama katika Mto huo ni mengi lakini hili la Wanafunzi akiwemo wa umri wa miaka 6 na 8 limekuwa na hisia kali hata zaidi na majonzi wa Wananchi.

Wanafunzi ambao hadi sasa hawajulikani walipo ni Ashura Haruna darasa la kwanza, Zabibu Jumanne darasa la pili (8), Ramadhani Kwila darasa la tano (12) na Tatu Sanaari darasa la kwanza (6) huku ambao wameokolewa wakiwa ni Issa Omary darasa la 6 na Michael Logoro darasa la kwanza.

=====

SASISHO
Miili ya Wanafunzi wawili kati ya wanne waliozama katika tukio la mtumbwi kuzama katika Mto Luiche Mkoani Kigoma imepatikana leo asubuhi na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Maweni.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Inspekta Jacob Chacha ametaja majina ya Wanafunzi hao kuwa ni Tatu Sanaari na Ramadhani Nkwila (12) darasa la tano.

Zoezi la uokoaji wa Watoto hao limeendelea leo asubuhi baada ya siku ya jana kufanyika kwa siku nzima bila mafanikio ya kuipata miili hiyo, majira ya asubuhi leo miili hiyo imeanza kuonekana ikielea katika Mto Luiche karibu kabisa na Ziwa Tanganyika.

Miili ambayo haijapatikana hadi sasa ni ya Watoto wawili Ashura Haruna wa darasa la kwanza na Zabibu, juhudi za utafutaji zinaendelea kufanywa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka Kigoma.

Pia soma: Serikali kugharamia mazishi ya wanafunzi waliofia mto Luiche wakivuka kwenda shule

Chanzo: EATV
 
Watoto wanne wamepotea kwa kuzama katika mto Ruiche na wengine wawili kuokolewa baada ya mtumbwi uliokuwa umewabeba kupinduka na kuzama katika mto huo uliopo Kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Watoto hao walikuwa wakielekea shule ya msingi Kagera, ambapo hulazimka kuvuka ng'ambo ya pili ya mto kwa kutumia mtumbwi ambapo nahodha alizidiwa nguvu kutokana na mto huo kujaa maji.

Ngoja walamba asali wanunue ma V8 kwanza
 
Watoto wanne wamepotea kwa kuzama katika mto Ruiche na wengine wawili kuokolewa baada ya mtumbwi uliokuwa umewabeba kupinduka na kuzama katika mto huo uliopo Kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Watoto hao walikuwa wakielekea shule ya msingi Kagera, ambapo hulazimka kuvuka ng'ambo ya pili ya mto kwa kutumia mtumbwi ambapo nahodha alizidiwa nguvu kutokana na mto huo kujaa maji.
Mungu awape pumziko la amani.. Gone too soon!
 
Na bila aibu inspekta chacha anasubiria 24hrs zipite ndio wakaopoe miili ya wahanga!jeshi hili halina kikosi maji pale kagera!,Urais wangu wa 24hrs nitarudisha idara hii ya uokoaji na zimamoto kuwa chini ya municipalities, polisi wote wanaofanya kazi kwenye idara hii nitawarudisha vituoni
 
Ila mabingwa wa mazoezi ya utayari wa uokoaji:

FppTZwuagAIKRK7.jpeg
 
Watoto wanne wamepotea kwa kuzama katika mto Ruiche na wengine wawili kuokolewa baada ya mtumbwi uliokuwa umewabeba kupinduka na kuzama katika mto huo uliopo Kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Watoto hao walikuwa wakielekea shule ya msingi Kagera, ambapo hulazimka kuvuka ng'ambo ya pili ya mto kwa kutumia mtumbwi ambapo nahodha alizidiwa nguvu kutokana na mto huo kujaa maji.

======
images
Wanafunzi wanne wa Shule ya misingi Kagera iliyopo Manispaa ya Kigoma ujiji Mkoani Kigoma wanasadikiwa kufariki baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kuvuka katika Mto Luiche kuelekea Shuleni kuzama.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Kigoma Inspekta Jacob Chacha amethitibisha kutokea kwa tukio hilo majira ya saa moja na nusu asubuhi ambapo licha ya kufanya msako wa uokozi lakini bado miili ya Wanafunzi hao haijapatikana.

Tangu majira ya saa moja na nusu asubuhi ya leo wakati tukio hilo linatokea mpaka hivi sasa licha jitihada za uokozi kufanywa na Askari wa Zimamoto na Uokoaji bado miili hiyo haijaonekana kwani Mto huo hupeleka maji yake katika Ziwa Tanganyika.

Wananchi wameeleza matukio ya vifo ya Watu kutokana na kuzama katika Mto huo ni mengi lakini hili la Wanafunzi akiwemo wa umri wa miaka 6 na 8 limekuwa na hisia kali hata zaidi na majonzi wa Wananchi.

Wanafunzi ambao hadi sasa hawajulikani walipo ni Ashura Haruna darasa la kwanza, Zabibu Jumanne darasa la pili (8), Ramadhani Kwila darasa la tano (12) na Tatu Sanaari darasa la kwanza (6) huku ambao wameokolewa wakiwa ni Issa Omary darasa la 6 na Michael Logoro darasa la kwanza.

Chanzo: EATV
Zitto katoa
 
Back
Top Bottom