Kigoma: Abiria 60 wanusurika kifo baada ya basi walilopanda kugongwa na lori la mchanga

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
11015815_1544583422486275_2001989783_n.jpg

Watu Zaidi ya 60 wamenusurika kupoteza Maisha wilayani Kibondo mkoani Kigoma baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Mwanza kwenda mkoani Kigoma,kupinduka baada ya kugongwa na gari la mchanga lililoingia barabara kuu gafla,kutokana na kufeli mfumo wake wa breki.

Radio Kwizera imeshuhudia Basi hilo la kampuni ya Adventure lenye namba za usajiri T 133 AGD ( Pichani ) likiwa limepinduka majira ya saa nane mchana huku abiria Zaidi ya 60 wakiwa wanaokolewa na kukimbizwa hospitalini kwa kutumia magari ya halmashauri ya wilaya ya Kibondo.

Baadhi ya mashuhuda wamesema kuwa gari aina ya Lori tipa lenye namba za usajiri T 420 CPQ lilifeli mfumo wa break na lilikuwa likiteremka kuingia barabara kuu ndipo likagongana na basi kisha kugeuka na kuangalia liliko toka huku basi likipinduka baada ya kugonga ukingo wa barabara.

Chanzo: Radio Kwizera
 
Oh! thanks God for your grace, jamani waha wenzangu poleni sana. da naona gari kwa chini linaka vumbi ketu kale.
 
Back
Top Bottom