Basi mbili za abiria na lori mbili za Mizigo zapata ajali kwa pamoja mkoani Mbeya

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Taarifa za awali ni kuwa ajali imetokea asubuhi ya leo maeneo Katikati ya Chimala na Igurusi mkoani Mbeya ikihusisha mabasi mawili ya abiria yaani Fikoshi (Mbeya Mwanza), Special Hire na Lori mbili za mizigo.

Chanzo bado hakijajulikana.


IMG_8025.jpeg
IMG_8024.jpeg
IMG_8027.jpeg
IMG_8026.jpeg

===

UPDATE:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga

"Ni kweli ajali hiyo imetokea, nafuatilia kujua madhara yaliyoto, tayari maafisa wa Polisi wamefika eneo la tukio, nitatoa taarifa baadaye tukipata ripoti kamili ya kilichotokea"

===

Watu wanne wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea wilayani Mbarali, mkoani Mbeya leo Jumapili Julai 16, 2023 baada ya Coaster kugongana na basi la kampuni ya Fikosh linalofanya safari ya Mwanza kuja Mbeya.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Kanali Mstaafu, Denis Mwila amesema ajali hiyo imetokea saa 12.30 alfajiri katika kona iliyopo Kata ya Igurusi, Tarafa ya Ilongo.

“Ni kweli ajali hiyo imetokea leo ambapo basi la Kampuni ya Fikosh lililokuwa linatokea Mwanza kuja Mbeya limeigonga costa inayofanya safari kutoka Ubaruku kuja Mbeya na kusababisha kugongana na uso kwa uso na gari linguine (Lori) kisha kuanguka pembezoni mwa barabara,”amesema.

Ameongeza kuwa Coaster iliyogongwa kwa nyuma ni mali ya Umoja wa Madereva Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva Hemedy Bamboya (46).

Aidha Kanali Mstaafu Mwila amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Mathias Mashala (59) Mkazi wa Wilaya ya Mbozi, Justina Stephano (Mkazi wa Mbozi), Ngimba Mashala (43) na Ombeni Given (23) wote walikuwa wakisafiri kwenye basi la Kampuni ya Fikosh lililokuwa likitokea Mwanza kuja Mbeya.

Mwila amesema hadi sasa (saa 5. 46 asubuhi) kutokana na taarifa za daktari, majeruhi watatu wameruhusiwa na mmoja bado anaendelea na matibabu.

Diwani Kata ya Igurusi, Hawa Kihwele amesema ajali hiyo imetokea eneo la mpakani mwa Mbeya na Makambako kijiji Mapungu Kata ya Igurusi tarafa ya Ilongo.

“Hilo eneo ni baya sana mara kwa mara zinatokea ajali na watu kupoteza maisha tunaiomba Serikali kuangalia namna ya kufanya upanuzi wa miundombinu ya barabara ili kunusuru maisha ya Wananchi,”amesema.
 
Ajali hii imetokea maeneo ya chimala mbeya ikihusisha basi kampuni ya fikoshi linalofanya safari zake kati ya mwanza kwenda mbeya na costa moja lililokua likitoka mbeya kwenda iringa.

Chanzo cha ajali ni lori lilokua limefeli brake na kusababisha ajali kwa mabasi mawili ya Abiria na lori jingine moja


241FED2B-5B0D-4670-8C13-6E1574319AAE.jpg

426BC0FA-C3D6-4884-95E5-5B132AB2AED5.jpg

868C1F0D-3808-4457-934E-93BF0B1921C1.jpg
 
Hivi kwanini wanasingiziaga malori kufeli brake!

Picha za hilo lori lililofeli brake zipo wapi! Na picha ya hilo lori lingine ipo wapi
 
Back
Top Bottom