Kigoda cha mwalimu live ITV

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,450
12,317
Shughuli ya kuaga Kigoda cha Mwalimu iko live ITV kutoka Nkurumah Hall UDSM.

Mada kuu ni "utatanishi na ukimya katika rasimu ya katiba mpya".

wageni mashuhuri ni pamoja na prof. Shivji,Mukandara,Lipumba,Mzee Butiku,Kingunge n.k.

Nawasilisha.
 
Pamoja na kumuaga pro.Shivji watakuwa na madahalo unaosema Utatanishi na ukimya katika Rasimu ya katiba mpya ipo ITV sasa namuona Dr Abushili Ally anaimba shairi la kuoga nitawajuzi kinachoendelea wanajamvi.
 
Pamoja na kumuaga
pro.Shivji watakuwa na madahalo unaosema Utatanishi na ukimya katika
Rasimu ya katiba mpya ipo ITV sasa namuona Dr Abushili Ally anaimba
shairi la kuoga nitawajuzi kinachoendelea wanajamvi.

Namsikiliza Prof Shivji kupitia Radio One. Anazungumzia "Ukuu wa Katiba" yaani The Supremacy of the Constitution.
 
Natazama mwanazuoni huyu anavyo bainisha viraka vya rasimu.... Anasema ujamaa umeondolewa,,imebaki kujitegemea:anasema ni sawa na kukata kidole ukabaki na pete.....
 
Mada

UTATANISHI NA UKIMYA KATIKA RASIMU YA KATIBA MPYA.
 
Last edited by a moderator:
Hawakumuweka kwa sababu ya msimamo wake kuhusu Ujamaa na kujitegemea, viongozi wengi wa sasa wana allergy na siasa za nyerere. Hawana tena mawazo ya kujitegemea.
 
Polisi sio japo la muungano kwa mujibu wa rasimu. Aisee asante Mwanazuoni PROF. SHIVJI kututoa kwenye majani na kutuweka Barabarani. Wengi wetu tuliishabikia tu lkn imejaa viraka kibao.
 
Duh katumwa na chichiemu nini au anataka kuua muungano!

Hapana Mito hii ni Rasimu ya jamhuri ya muungano kwa hivyo Pro anajaribu kuonyesha kuwa pamoja na baadhi ya ibara hizi kuwa nzuri lakini baadhi ya serikali washirika wanaweza kukwepa kuziweka kwenye katiba zao sio kama ametumwa
 
Prof.PALAMAGAMBA KABUDI,simuoni hapa ukumbini maana ni gwiji wa sheria ila amekuja na rasimu yenye viraka makumi kwa mamia.
Itabidi azichukue hizi hoja azipeleke kwa WARIOBA
 
Tuwekeeni hapa huo mhadhara na sisi tuufaidi.
Ndo mhadhara wake wa mwisho kama mwenyekiti wa kigoda cha mwalimu Nyerere.
 
Wakuu, ki ukweli, Prof. Issa Shivji kanena ukweli mtupu! Nimefurahi sana binafsi. Pia akina Prof. Lipumba, Mzee Butiku, Kingunge, na wengineo wanaonekana kabisa kukubaliana na hoja za Shivji.

Na katika hoja kubwa ambayo hata mimi ilikuwa inanipa tabu, ni kuhusu aina ya Katiba Wananchi waliyokuwa wanatolea maoni. Prof. Anasema, tulitaka Mlima, tukaletewa Kichuguu. Kwa maana ya kwamba, Tulijua kabisa tunataka katiba ya Bara pamoja na ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, sasa Tume imekuja na katiba moja, tena yenye mkanganyiko kibao.

Na alienda mbali zaidi na kusema kuwa, je, kama siyo hujuma kwa tume kutumia pesa yote na kuja na rasimu moja tu, ni lini Wananchi wataitwa tena kutoa maoni ya Katiba ya Zanzibar na Bara, kwa gharama zipi na muda gani???.

Inaonekana Jaji Warioba na timu yake ndo wanataka kufanya hicho kijiwe cha kuvuna.

Wataalam wakiipata wailete hapa ili tuisikilize tena!
 
Back
Top Bottom