Kigezo alichotumia Rais Samia kuongeza posho za wanafunzi akitumie pia kuongeza posho zetu askari

Kyenyabasa

JF-Expert Member
Mar 8, 2023
248
712
Raisi Samia Askari tunahitaji uongeze posho zetu kwa KIGEZO kilekile kwamba gharama za maisha zimepanda!! Kama ilivyo kwa watu wengine nasi maisha yamepanda Sana hivyo hakikisha unaongeza posho zetu ikiwezekana kabla ya mwezi July.

Sisi kama unavyoelewa muda wote tunakutumikia wewe iwe mvua liwe jua hatuna hata muda wa kuuza barafu na visheti Kama wenzetu walimu kujiongezea kipato, posho zetu hazijaboreshwà kwa miaka mingi sasa, ni wewe peke yako ambae hujaweka alama katika vyombo vyako vya ulinzi na usalama tofauti na watangulizi wako.

Askari wote Wizara ya ulinzi na Wizara ya Mambo ya Ndani tuonee huruma uongeze POSHO zetu.

NI SISI WALINZI WAKO, WENYE NJAA NDANI GWANDA. Samahani mama imetumika lugha ya kijeshi yenye amri kidogo usichukie uuonapo ujumbe huu.Tunakupenda na tunakutakia kazi njema
 
Rais Samia tunakusalimu. Mama tunakuomba uongeze ppsho zetu ambazo hazijaongezwa kwa muda mrefu sasa.

Rais Samia wewe tu ndio bado hujaona umuhimu wa kuweka alama yako katika vyombo vyako tofauti na watangulizi wako.

Rais Samia sisi askari wako hatuna muda wa ziada wa kujitafutia vipato vya ziada nje ya stahiki zetu Kama ambavyo watumishi wenzetu hufanya maana muda wote tuko utumwani makambini mwetu au nje tukihakikisha Taifa liko salama.

Wizara ya Ulinzi na Wizara ya Mambo ya Ndani tunakuomba uchukue hatua za haraka kutunusuru na ugumu huu wa maisha. Mama njaa haifichwi kamwe.

Tunakupenda sana lakini tuna njaa inayotishia ufanisi wa kazi zetu kama Askari wa nchi hii.

Kazi njema mama.
 
Ngoja kidogo..

Unazungumzia askari gani...?

Trafiki , wa posho ya kubrashia viatu..

Askari polisi wa vituoni wanaobambikia watu kesi...

Askari wa jeshi (Sidhani maana wanaposho toshelezi)..

Final, Posho za Askali wa tz ni zaidi ya mshahara wake..

(Posho ya pango,posho ya mwezi, na posho za ulinzi (itategemeana na eneo analolinda)...

Acha uongo
 
Mama amesema anapitapita Jamiiforums. Walau tutaona mengi. Hadi madokezo yanaweza kuletwa huku
 
Hao wanafunzi bila shaka watarejesha
Ulifikiri wanapewa bure? Hilo ni boom lazima urudishe ili wengine wapate. Sio unafurahia kuongezwa tu, furahia na kurejesha.

Naona madogo wanamodify mageto ya kutombea tu huku mtaani, kumbe pesa za boom.
 
Mkuu, ndani ya saa moja umeanzisha nyuzi mbili za kuomba maboresho ya maslahi kwa maaskari

1678300925047.png
 
Back
Top Bottom