Kigamboni yasimama...Prince Charle akaushiwa

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,037
24,595
Shughuli na Mawasiliano kati ya Kigamboni na maeneo ya katikati ya jiji yalisimama leo hii na kusababisha usumbufu na misongano. Hali hii ilisababishwa na hatua ya mtoto wa malkia wa Uingereza Prince Charles kuamua kuelekea maeneo ya Kigamboni.

Watu wakiwa wamelazimika kusubiri huku Pantoni kubwa lililokuwa limesheheni abiria wengi, mizigo na magari nalo lilisimamishwa katikati ya maji kusubiri mpaka Prince Charles atakapofika, pamoja na malalamiko toka kwa watu hali katika maeneo ya feri ilikuwa ya utulivu huku maofisa usalama wa taifa, Polisi na askari wa kutuliza ghasia (FFU)na maofisa usalama wa Uingereza wakiwa wametanda na magari yao pampja na magari ya agonjwa ambulance.
Kuzuiwa huko kwa shughuli za usafiri kulipelekea watu kulundikana sehemu moja na kwa muda mrefu kitu kilichoonekana kama mbinu iliyotumika kuwaweka watu sehemu moja ili kujenga taswira ya watu kujitokeza kumlaki mgeni, wakati hata ujio wake wengi wao hawakuwa wakiujua licha ya kutangazwa na vyombo vya habari
Baada ya wananchi kusubirishwa kwa muda mrefu hatimaye Prince Charles aliwasili eneo hilo akiwa ndani ya gari lake yeye pamoja na mke wake na kuanza kupungia watu mikono waliopo maeneo hayo lakini kama vile walioambiana kuanzia watoto hadi watu wazima hakuna hata mmoja aliyepunga mkono kama ishara ya kujibu salamu ile, bila kusimama akaelekea moja kwa moja katika Pantoni ndogo ya MV KIGAMBONI, ambayo ilikuwa imeandaliwa mahsusi kwa ajili ya kumpeleka ng'ambo ya pili (Kigamboni).
Sintofahamu majini
Pantoni iliyombeba ikiwa inakaribia katikati ya maji ikajikuta inaingiliana na Meli ya mafuta iliyokuwa inaelekea bandarini, hapo ikabidi kanuni zivurugwe ambapo boti ya ya jeshi la polisi ilibidi iende kuizuia na kuiamuru meli ile kusimama kwanza nayo ikabidi ifanye jitihada kusimama eneo la soko la samaki la feri ile kupisha msafara upite, ieleweke kuwa ni kawaida meli ikishavuka bomba limwagalo maji machafu baharini , maarufu kama bomba la Muhimbili huwa Pantoni na meli nyingine zote hulazimika kusubiri ili ile ipite kwanza kwani kwa mujibu wa wataalam wa vyombo vya majini ni kuwa ni rahisi kusababisha ajali kama chombo kingine kikubwa kitakatisha mbele yake au kuelekea uelekeo wake..
Baada ya kuelekea Kigamboni ilibidi watu waendelee kusubiri kwa saa nyingine mpaka alipoanza kurudi ndipo Pantoni likaruhusiwa kuanza kupakia na kupeleka abiria kama kawaida.
Picha chi
Maoni ya Watu
Ziara hiyo ya Mwana wa Malkia ilionyesha kuchukiza wengi na kutofurahiwa kabisa kutokana na kauli iliyotolewa hivi karibuni na waziri mkuu wan chi hiyo kuhusu masharti mapya ya utoaji wa miasaada kwa nchi wananchama wa Jumuiya ya madola watakaotaka kuendelea kupokea misaada ya nchi hiyo.
Masharti ambayo wengi wanayatafsiri kama haki kwa gharama ya utu wa mtu, maadili na heshima kitu kinachoonekana kama dharau.
Pia watu wengi wameilaumu serikali kwa aina ya mapokezi waliyompa Prince Charles, kwani ni serikali hiyo hiyo iliyowaongoza wananchi na iliyokuwa mstari wa mbele katika kutoa msimamo dhidi ya mashart hayo yaliyojaa dharau na yenye kutojali ndani yake, lakini cha ajabu alipokuja mgeni toka nchi hiyo hiyo na bado upepo wa swala hili ukiwa na nguvu yake ile ile serikali ikawaacha wananchi wake na kwenda upande wa mgeni kumpa aina ya mapokezi ambayo yakazidi kuwa kero kwa raia wake, kitu kilichowafawafanya watu wengi washindwe kuelewa ni wapi hasa ulipo msimamo wa serikali? Kwenye Matendo Yake? Au kwenye Maneno yake?
 
Du Bushi kanunua kigamboni nae prince anaenda kununua wapi katiba mpya tutakuja kuzichukua tu
 
Ameleta waraka wa ushoga baadae atamegewea sehemu katika shamba la bibi
 
kuna kijana wangu nilimtuma kariakoo, anasema foleni ni kubwa sana, ndiyo kavuka sasa hivi. mnaokaa kigamboni leo mtafika saa nne usiku ma kwenu, waiting room pale feli ilijaa hadi watoto wakaanza kulia kukosa hewa, wananchi wana haki ya kukasirika maana wanaotegemea risk za fasta leo siku imekula kwao.
 
​anashangaa mambo kimya kimya huku watz wanaomsindikiza wanajidai kumweleza watanzania wamechoka ndio maana hakuna vigelegele
 
Watu jua kali na matumbo hayana kitu unafikiri wanajua hata Prince Charles ni nani??
 
anatayalisha sehemu ya sodoma na gomola, bush kaishachukua mapema Clinton yeye Kisarawe
 
Back
Top Bottom