Kifo Kimegoma Muda mrefu sasa.Inakuaje Mtu anakosa bahati ya Kufa anaishi tu?

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,744
sisi binadamu tunaoishi uswahilini ni mateso bila chuki. mchana nzi, usiku mbu. yaani hakuna uafadhali.kila siku ni afadhali na jana. hakuna jema si mvua, si jua. usiku balaa kubwa. ndani joto, nje mbu. yaani sisi maisha yetu! we acha tu. hakuna jema mchana nzi usiku mbu. utadhani tumepewa trial version ya jehanamu huku huku duniani.

maisha yamekuwa magumu mtu unatafuta kifo halaf hakiji, unakosa hata pesa ya kununua sumu. mambo magumu unaona bora ufe tu. hata vitu tunavyotumia huku ni feki au vime expire.fikiria mtu unaenda kuazima kamba ujinyonge nayo inakatika. kumbe nayo ilioza unatafuta kwa majirani. hamna mwenye kamba mpya. yaani ni mateso kwa kwenda mbele. unaenda kuomba mtu akusaidie kiasi kidogo kama ana sumu ya panya ili ujinywee ukufilie mbali anakushangaa ..... anakwambia pesa ya kula tu hana ndo akahangaike kununua kitu cha kuwalisha panya wafe.si angekuwa nayo hiyo pesa angewanunulia watoto wake hiyo sumu wanywe wafe apunguze mzigo na pia apate pesa za michango? unagundua kumbe afadhali na wewe. unaondoka kwa unyoooonge.kila unapogusa ni miba na moto.hakuna unafuu.

usiku ukifika haulali.utalalaje na mbu nao wanakuja kudai chao...damu yenyewe uliyo nayo ni ya kukutosha wewe tu kusukuma moyo tena kiubishi maana kama ni mafuta ya gari pump imevuta mpaka mchanga au matope kule chini, but mbu nao wanakuzonga bila aibu wakitaka kushare. watoto wanagombana pale chini kugombea kulala kwenye godoro maana ni nchi nne kwa sita halafu wao wapo watano. hivyo inabidi kuwah kulala katikati maana wa mwishoni huwa wanalala chini.ukicheki saa ni saa saba hiyo bado hakuna usingizi si wewe si watoto. nawe unawavizia tu walale ujipindue umnanii mkeo.maana angalau hapo nawe ndo unatua mzigo.

kazin kila mtu anakutulia wewe mizigo.ukanunue chips za watu mchana,ukirudi ukapeleke sijui nini kwa nani,ukikaa kidogo umetumwa sijui wapi.ukirudi unapewa kazi nyingine ufanye basi wewe ni kama hutakiwi kuonekana umepumzika au umekaa kuvuta pumzi.wanakutulia mizigo yooote wewe.ukirudi home na watoto nao wanakutwisha mizigo mara uniform zimeisha n.k. hapo ndo unagundua ule msemo wa ukubwa jalala.

wewe unakitendo kimoja tu cha kushusha mzigo wako. kwa mkeo. na usipokuwa mwangalifu utajikuta siku zote yeye hashushi unashusha wewe tu na unalala unamwacha yeye na yake mengi.kesho na keshokutwa naye anajaribu angalau akashushe mzigo kwa mtu hapo mtaani.basi ni balaa juu ya balaa.

unawaza ufe lakini kifo kinagoma kabisa... hivyo kufa hufi ila cha moto utakiona.wakati unawaza hayo unaona mwanga wa torch dirishani.vibaka nao wanapita waangalie kma kuna simu wachane dirisha waibe.unasonya kwa hasira unageuka upande mwingine kibaka naye anakutukana "fala wewe mpaka muda huu hujalala " anasonya anaondoka. haya ndo maisha yetu uswahilini.kushikana uchawi, vibaka kila siku,kukabwa vichochoroni, kusikia kelele za wanawake wanasutana, au kusikia kuna mchawi anakimbizwa. ni kawaida tu watu kupandisha mashetani na kudai vitu flan flan...

jana mke wangu nlimsikia anampigia simu mama ashura kumuuliza amepika nini yule mama akasema dagaa basi mke wangu akamwambia huku yeye kapika maini ila umudi na shabani hawapendi maini hivyo anamtuma chausiku akachukue hao dagaa. mi sikumbuki kama nilinunua maini. nikamuuliza toka lini umudi na shaban hawali maini na mbona sikuacha pesa ya maini? akatabasamu akasema we huoni kuna maharagwe tu humu ndani? nilikuwa nataka nibadili mboga. baada ya muda akarudi chausiku ana kibakuli cha dagaa na kingine aliomba awekewe maini ili ampelekee mama ashura. nikatikisa kichwa ,nikajiinukia niondoke nikacheze bao....

jaman tunaposema hali ni ngumu mjue hali ni ngumu kweli kweli. hali inakuwa ngumu kiasi kwamba hata kwenye makaburi nako maiti wanashauri watu mlio hai msife kwa sababu kule chini nako kuna ukata. yaani watu wabaki hai tu maana huko waliko wafu nako hali ni ngumu sana. imefikia hatua walioko hata ughaibuni wanatwambia sisi tusiende kule na wao tunawaambia wasije huku. hivi haiwezekana tukaanzisha tu sayari nyingine tukaenda kujiishia huko maisha mapya ambayo hamna haja ya nguo wala magari,nyumba n.k ni kula tu na kulala? of course kuwe na matunda mengi na wanyama wa kutosha.

nshajichokea miye sasa nawaza nikagongwe tu na gari nifilie mbali.shida madereva hivi sasa nao wapo makini sana. wanafunga break hapa miguuuni... wanakukosa na unaweza kuta ukakoswa na ajali usife ila ukaja kujeruhiwa kwa kipigo.bado hufi ila cha moto unakiona.anyway ngoja tuendelee kubuzi buzi tu hapa duniani.mtu unawaza sijui uwe kambale doa?maana huchelewi hata kuwaacha watoto wako wawe machangudoa aaargh.....! sasa ya nini wakae nacho na hakiwalipi mibazazi inakitumia tu bure bure inaondoka wewe ndo unavilisha vitoto vyako vya kike viende vikaliwe...inaudhi sana.

maana unajua watoto wako wanaliwa pale mtaani na vitoto vingine navyo choka mbaya.sasa badala ya kuliwa bure si bora wakauze? hayo mawazo ya kishetani ngoja niyakemee.na mimi pia nikiwa kambale doa si kuna wamama wana pesa ila...aaarghh si naweza oa wake hata wawili zaidi? nakuja kushtuka ni saa 10:10 alfajiri sijalala toka jana na wife sikumgeukia...sijashusha mzigo.sasa ndo usingizi unaninyemelea tena mkali sana.wakati muda huu inabidi niwah kuamka nikawah foleni ya kuoga pale nje chooni.sijalala toka jana.naamka haraka na kumwamsha wife aniwahie folen maana ukichelewa inakuwa issue...

kuna jirani hapa kijana naye ana watoto watatu chumba kimoja anashangaza sana wanajifanya wanapendana na mkewe. asubuh wanaenda kuoga ila sasa ndo wanachelewa kutoka mpaka kero.dk 40 wanaoga huelew wanapakana sabuni au nini..maana utasikia tu sauti kwa chini na ukimyaaa flan halafu sauti za kugugumia.baaadaye ndo unasikia sauti ya maji. wanakera sana.hivyo kila mtu anawahi kwenda kuoga kabla yao. baba chande ye ndo alishagundua ujanja.anaamka saa tisa anaoga halafu anarudi analala mpaka saa 11 kamili anaenda kazini. huwa tunashangaa maana joto la hizi nyumba zetu ni kama upo kwenye oven au microwave.yeye akirudi ndani si anaokwa tena kama kawaida na jasho?

sisi nyumba zetu ni kama tunaokwa.... ni joto mwaka mzima....yaani sijui huku kukoje?....nasikia kuna mabadiliko ya tabia nchi basi nadhan huku ndo yalikoanzia na kuishia.joto mchana, joto usiku. na tunavyolala kwa mahaba yaani kubanana... inakuwa INSHU kweli.anyway ipo siku moja nasi tutawin.maisha ni haya haya hamna mengine.
 
Sasa wewe ukifa mimi nitammwagia nani matope nitakapo pita na Prado langu kwenye mtaa wenu.?

We ukifa nani atachimba kaburi langu na kulijengelea.?

Au pengine we ufe then nimchukue mwanao nimfanye kamchepuko nikajengee na nyumba pembeni ya mji.

Hakuna kufa hapa wote lazima tuisome namba ili huyu mtu 2020 asirudi tena. Anza kufikiria kufa walau 2026
 
sisi binadamu tunaoishi uswahilini ni mateso bila chuki. mchana nzi usiku mbu. yaani hakuna uafadhali.kila siku ni afadhali na jana hakuna jema si mvua si jua. usiku balaa ndani joto nje mbu. yaani sisi maisha yetu we acha tu. hakuna jema mchan nzi usiku mbu. utadhani tumepewa trial version ya jehanamu huku huku duniani.

maisha yamekuwa magumu mtu unatafuta kifo halaf hakiji unakosa hata pesa ya kununua sumu. mambo magumu unaona bora ufe tu. hata vitu tunavyotumia huku ni feki unaenda kuazima kamba ujinyonge inakatika kumbe nayo ilioza hamna mwenye kamba mpya. yaani ni mateso kwa kwenda mbele. unaenda kuomba mtu kama ana sumu ya panya ili ujinywee ukufilie mbali anakushangaa .. anakwambia pesa ya kula tu hana ndo akahangaike kununua kitu cha kuwalisha panya wafe.si angekuwa nayo hiyo pesa angewanunulia watoto wake? unagundua kumbe afadhali na wewe.

usiku ukifika haulali.utalalaje na mbu nao wanakuja kudai chao..damu yenyewe uliyo nayo ni ya kukutosha wewe tu but mbu nao wanakuzonga wakitaka kushare. watoto wanagombana pale chini kugombea kulala kwenye godoro maana ni nchi nne kwa sita halafu wao wapo watano. hivyo inabidi kuwah kulala katikati maana wa mwishoni huwa wanalala chini.ukicheki saa ni saa saba hiyo bado hakuna usingizi si wewe si watoto. nawe unawavizia tu walale ujipindue umnanii mkeo.maaana angalau hapo nawe ndo unatua mzigo.

kazi kila mtu anakutulia wewe mizigo.ukanunue chips za watu mchana,ukirudi ukapeleke sijui nini kwa nani,ukikaa kidogo umetumwa sijui wapi.ukirudi unapewa kazi nyingine ufanye basi wewe ni kama hutakiwi kuonekana umepumzika au umekaa kuvuta pumzi.wanakutulia mizigo yooote wewe.ukirudi home na watoto nao wanakutwisha mizigo mara uniform zimeisha n.k. hapo ndo unagundua ule msemo wa ukubwa jalala.

wewe unakitendo kimoja tu cha kushusha mzigo wako. kwa mkeo. na usipokuwa mwangalifu utajikuta siku zote yeye hashushi unashusha wewe tu na unalala unamwacha yeye na yake mengi.kesho na keshokutwa naye anajaribu angalau akashushe mzigo kwa mtu hapo mtaani.basi ni balaa juu ya balaa.

unawaza ufe lakini kifo kinagoma kabisa... hivyo kufa hufi ila cha moto utakiona.wakati unawaza hayo unaona mwanga wa torch dirishani.vibaka nao wanapita waangalie kma kuna simu wachane dirisha waibe.unasonya kwa hasira unageuka upande mwingine kibaka naye anakutukana "fala wewe mpaka muda huu hujalala " anasonya anaondoka. haya ndo maisha yetu uswahilini.kushikana uchawi, vibaka kila siku, kusikia kelele za wanawake wanasutana, au kusikia kuna mchawi anakimbizwa. ni kawaida tu watu kupandisha mashetani na kudai vitu flan flan...
jana mke wangu nlimsikia anampigia simu mama ashura kumuuliza amepika nini yule mama akasema dagaa basi mke wangu akamwambia huku yeye kapika maini ila umudi na shabani hawapendi maini hivyo anamtuma chausiku akachukue hao dagaa. mi sikumbuki kama nilinunua maini. nikamuuliza toka lini umudi na shaban hawali maini na mbona sikuacha pesa ya maini? akatabasamu akasema we huoni kuna maharawe tu humu ndani? nilikuwa nataka nibadili mboga. baada ya muda akarudi chausiku ana kibakuli cha dagaa na kingine akomba awekewe maini ili ampelekee mama ashura. nikajiinukia niondoke nikacheze bao....

jaman tunaposema hali ni ngumu mjue hali ni ngumu kweli kweli. hali inakuwa ngumu kiasi kwamba hata kwenye makaburi nako maiti wanashauri watu mlio hai msife kwa sababu kule chini nako kuna ukata. yaani watu wabaki hai tu maana huko waliko wafu nako hali ni ngumu sana. imefikia hatua walioko hata ughaibuni wanatwambia sisi tusiende kule na wao tunawaambia wasije huku. hivi haiwezekana tukaanzisha tu sayari nyingine tukaenda kujiishia huko maisha mapya ambayo hamna haja ya nguo wala magari,nyumba n.k ni kula tu na kulala? of course kuwe na matunda mengi na wanyama wa kutosha.

nshajichokea miye sasa nawaza nikagongwe tu na gari nifilie mbali.shida ma madereva hivi sasa nao wapo makini sana. wanafunga break hapa miguuuni... wanakukosa na unaweza kuta ukakoswa na ajali hufi ila unakuja kujeruhiwa kwa kipigo.tena hufi ila cha moto unakiona.anyway ngoja tuendelee kubuzi buzi tu hapa duniani.mtu unawaza sijui uwe kambale doa?maana huchelewi hata kuwaacha watoto wako wawe machangudoa...aah sasa ya nini wakae nacho na hakiwalipi mibazazi inakula tu...maana unajua watoto wako wanaliwa pale mtaani na vitoto vingine navyo choka mbaya.sasa badala ya kuliwa bure si bora akauze? hayo mawazo ya kishetani ngoja niyakemee.na mimi pia nikiwa kambale doa si kuna wamama wana pesa ila...aaahh si naweza oa wake hata wawili zaidi?anywa ipo siku moja nasi tutawin.maisha ni haya haya hamna mengine.
Ukiendelea na kipaji hiki cha uandishi fikirishi utatoka huko Tandale sasa hivi. Uko juu. Ila tofautisha vituo, koma, semi koma nk pamoja na matumizi ya herufi kubwa na ndongo. Big up kwa uandishi mahiri, inalekea wewe ni mtu wa "classic novels".....
 
Back
Top Bottom