Binadamu anaponzwa na matumaini ya muda mrefu

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,520
6,503
Kila mwanadamu huwa na matumaini kwamba hakika yeye bado ana mda mrefu wa kuishi duniani,na kwamba uzima wake na afya yake nzuri ndio viashiria ambavyo humuaminisha kwamba yeye bado yupo yupo kwanza.

Ukitaka uamini hili ninalosema ebu msikie huyu mtu ikiwemo mimi na wewe mara tunapo sikia habari ya mtu fulani amekufa mara moja huanza kuuliza, vipi alikuwa anaumwa? Au amekufa kwa maradhi gani?

Hii yote inadhihirisha kwamba tunaamini wote wanao kufa basi lazima wawe wanaumwa kwanza au lazima wawe hawako vizuri kiafya hii ndio mitazamo yetu kwa wengi wetu.

Matokeo yake kwa sisi ambao alihamdulillah tumejaaliwa afya njema kwa mda huu huwa na matumaini makubwa sana ya kuishi mda mrefu, na matokeo yake tunashindwa kukumbuka kwamba ipo siku nasi tutakuwa marehemu watarajiwa na tutakutana na Mola wetu.

Matumaini ya kuishi mda mrefu hutufanya tuweze kuwadhulumu watu haki zao huenda labda kutokana na vyeo vyetu au connection zetu katika jamii, kutotenda haki kwa wanadamu wenzetu, kujilimbikizia mali zisizo halali ili tu tunufaishe matumbo yetu, kuchukua rushwa na mambo kama hayo.

Mtu mwerevu ni yule ambaye siku zote hukumbuka kuwa yeye ni mavumbi na hakika mavumbini atarejea, hivyo hana budi kujitengezea mazingira mazuri ya huko anakokwenda baada ya kifo chake,hakika huko atahojiwa kwa kila tendo alilolifanya hapa duniani.

Mwanadamu anarekodiwa kwa kila tendo na jambo analolifanya ima liwe kubwa au dogo,yote hayo yako katika kumbukumbu zake, mwanadamu huyu anakuwa salama tu pale anapokuwa amelala au pale anapokuwa hajazungumza chochote, au hajafanya tendo lolote, kwani Mwenyezi Mungu ametusamehe kwa yale ambayo yapo katika mawazo maadamu tu hatujayafanya.

Mfano naweza kuwaza kwamba nataka nikazini na fulani,kwakuwaza huku sitakuhukumiwa ila nikilitekeleza wazo langu kwa kuenda kuzini hapo sasa nitachukuliwa kumbukumbu zangu kwa matumizi ya baade huko akhera.

Mwanadamu atambue kuwa kila mtu ana malaika wawili ambao anaambatana nao katika maisha yake yote, mmoja yupo kuliana kwake huyu huandika mambo mema na yule wa kushoto huandika matendo mabaya ya mja huyu, ima umezungumza chochote au kuandika chochote au kufanya chochote basi kumbuka kumbukumbu zinahifadhiwa kwa matumizi ya baadae.

Acha kuwa na matumaini ya mda mrefu kwani hakika mwanadamu hujui mda wala saa ya kuondoka kwake,hakikisha unayatarisha makazi yako ya mbinguni mapema kabisa.


Ni hayo tu!
 
Mkuu, hakuna mbingu nyingine zaidi ya hii.... Ukifa tu ni chakula cha wadudu. STORY INAISHIA HAPO...
 
Bibi yangu alikufa mwaka 1998 akiwa na umri wa miaka 87 alikuwa ajuza.

Lakini bado watoto wake hawakukubali wakidai ameuawa kwa kurogwa, gharama za kwenda kwa wataalamu (waganga wa Jadi) kwaajili ya kumjua mchawi aliyefanya hivyo.

Ulikuwa ni ujinga na ukengeukaji uliopitiliza,hakika huwa nikikumbuka naumia sana.

Elimu, Elimu, Elimu

Elimu ni muhimu mno kwa ustawi wa familia na jamii kiujumla
 
Bibi yangu alikufa mwaka 1998 akiwa na umri wa miaka 87 alikuwa ajuza.

Lakini bado watoto wake hawakukubali wakidai ameuawa kwa kurogwa, gharama za kwenda kwa wataalamu (waganga wa Jadi) kwaajili ya kumjua mchawi aliyefanya hivyo.

Ulikuwa ni ujinga na ukengeukaji uliopitiliza,hakika huwa nikikumbuka naumia sana.

Elimu, Elimu, Elimu

Elimu ni muhimu mno kwa ustawi wa familia na jamii kiujumla
Huo kweli ulikuwa ujinga uliopitiliza, ukichukulia umri wake kwa hakika ilikuwa wazi kuwa mda wake umefika.

Lakini hata kama ungekuwa mmoja kati ya hao waliofanya hivyo maadam nafsi inajuta basi ingekuwa sehemu ya toba yako, kwani kujuta kwa nafsi ni dalili ya kutaka toba kwa mungu
 
Back
Top Bottom