Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Shibuda amwakilisha baba wa Kanumba Send to a friend
Tuesday, 10 April 2012 20:49
0diggs
digg
Vicky Kimaro
MBUNGE wa Maswa Magharibi, John Shibuda jana alimwakilisha baba wa msanii maarufu wa filamu nchini marehemu Steven Kanumba katika mazishi ya msanii huyo akidai kuwa baba huyo Charles Kusekwa Kanumba ameshindwa kuhudhuria mazishi hayo kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya malaria na shinikizo la damu na si matatizo yake na merehemu huyo.
Kupitia uwakilishi huo, Shibuda pia alisoma barua aliyoeleza kutoka kwa mzazi huyo wa Steven Kanumba akieleza kushindwa kwake kufika kwenye mazishi hayo na kwamba ametuma watoto wake na wakwe zake kumwakilisha.
"Baba yake Kanumba siku ya Jumamosi alikuwa anajisikia vibaya na alipokwenda hospitali alipimwa na kukutwa ana malaria 15 na shinikizo la damu likiwa 180 - 140. Lakini pia ana matatizo ya miguu kwa muda mrefu, anatembea kwa msaada wa baiskel,"alisema Shibuda.

Akisoma barua hiyo Shibuda alinukuu barua ya baba wa Kanumba akisema:"Salam, nashukuru wana kamati ya mazishi ya mwanangu kwa kunitumia nauli ili niweze kuja kumzika mtoto wangu. Lakini kutokana na maradhi yanayonikabili sitaweza kuja, ila nawatuma wanangu Michael na Mjanael, pia mkwe wangu Chrisant Msipi waniwakilishe. Matatizo yangu na mwanangu yalishakwisha."
"Msianze kuleta maneno yenu ya umbea umbea na uzushi eti hajafika kwenye msiba wa mwanawe kwa kuwa hawaelewani huo ni uzushi, walishaelewana na alikuwa na mawasiliano mazuri na mke wake mama Kanumba na ndiyo maana akatuma wawakilishi wake,"alisema Shibuda.


Source: Gazeti Mwananchi
"Msianze kuleta maneno yenu ya umbea umbea na uzushi eti hajafika kwenye msiba wa mwanawe kwa kuwa hawaelewani huo ni uzushi, walishaelewana na alikuwa na mawasiliano mazuri na mke wake mama Kanumba na ndiyo maana akatuma wawakilishi wake,"alisema Shibuda.
 
hata huyu binti ana gari? Dah lazima nipambane mwaka huu na mm nivute kasuzuki.....habari za kiitelijensia zinasema huyo mtu ni vicent kigosi.
 
Kuna habari za kuaminika kuwa Marehemu Kanumba alikuwa hadi kaagiza RPG na Heavy Machine Gun hapo kwake.

Na ili kujilinda na kupata usafiri wa uhakika, Kanumba alikuwa mbioni kuwa Muafrica wa kwanza kuwa na Apache yake.

Nashindwa kuelewa siku ikifika, itauzwa Kenya au JWTZ wataamua kuinunua maana sidhani kama wanayo.

800px-Westland_apache_wah-64d_longbow_zj206_arp.jpg
 
kama unavyosema inaweza kuwa sahihi kufikiri nje ya mawazo tuliyonayo sasa...japo ndio hivyo mara freemansons mara pombe basi ilimradi kila mtu anastory yake

Hapoooo ndio sielewi mbona wanasema jamaa alikua hatumii hiyo kitu,lipi ni lipi???!!!waiiiii wanatuchosha tu.
 
Kanumba alipewa sumu muda mrefu kabla, pengine jioni ile alipotoka matembezi (au kazini) na labda siku moja au mbili kabla.

Lulu kwa kuwa alikuwa na mahusiano ya karibu alitumwa kwenda kuangalia effect ya kilo alichopewa huyo mnayemuita 'the great,' maana jamaa aliyeleta hiyo kitu kutoka Nairobi si ajabu aliwaingiza mjini

Kwa kuwa kabinti ni kichwa hewa kalienda tu kama zuzu na kalipokuwa huku jamaa kwa mchecheto wakata kujua hali ya kanumba kupitia simu ambazo Lulu aliogopa kuzijibu akihofu mhusika kusikia kuwa alikuwa anaongea na mmoja wa maadui zake.

Na hakika Kanumba alipofanikiwa kuipokonya Simu ya Lulu akagundua kuwa binti alikuwa anateta na adui yake mkuu, yaani Mr X.

"Yaani huyu ndiye ......!" akakata kauli na kuanguka maana dawa ilikwisha kuchukua effect.

Eeh hii tena mpyaaaa......kama muvi vileeeee teh teh teh kasheshe.
 
Ooh yeah....kanang'aa kweli kweli. Sasa najiuliza kama huko jela wanaruhusiwa kuwa na make-up, kutumia simu (manake kuna taarifa kuwa kuna watu walikuwa wanawasiliana naye kwa njia ya text messages), na kadhalika.

Hata nywele zake zipo freshi na sio tim tim kama za Wema enzi zile alipotoka Segerea
Hiyo picha si ya leo! Ni moja ya kesi zake za zamani...
 
....i pity her.....
Hyu mdogo wa Kanumba kwanin yuko huru.....
Kuna kitu bado kinafichwa....

...intellijensia uharo....
 
Back
Top Bottom