Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,504
- 113,618
- Thread starter
- #121
BHT, asante kwa hili, kila jambo linafanyika kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, imeshatokea mara nyingi tuu, wale wenye wajibu wa kusimamia hizo sheria, taratibu na kanuni, ndio wako mstari wa mbele kuzivunja sio kwa makusudi tuu, bali kwa kutojua sheria. Kuna makosa kibao polisi wanafanya kinyume cha sheria na yanaachwa kwa vile raia hawajui haki zao!.Pasco, umegusia jambo la muhimu saana uliposema unataka kusaidia wengine wajue haki zao...
Kwa kweli hili ni tatizo hasa pengine zaidi ya wengi wanavyodhani...(kuna mahala mtu anasema utaratibu wa PF3 uko wazi na unafahamika...nimesikitika sana)
eneo hili la huduma linahitaji saaana msaada wa wataalam husika. Umechagua njia iliyo njema kwa kweli kama uyasemayo utayaweka kwenye matendo.
Juzi baada ya ule mgomo wa madaktari, nimefanya video documentary kuonyesha uzembe wa serikali kwenye mgomo huo uliopelekea loss of life, mwisho wa kipindi nikasema serikali lazima iwajibike for all the life lost kwenye mgomo huu na nikasema ingekuwa nji za wenzetu, hospitali zikashapelekwa mahakamani zamani na kudaiwa fidia!. Kipindi hicho kimekataliwa, eti ni uchochezi!.
Kila siku ajali zinatokea, watu wanapoteza maisha and its the end. Wenye magari yao ndio hudai fidia ya mali zao and no body cares kuhusu waliopoteza maisha kwa vile watu hawajui haki zao.
Ziko kesi nyingi ni criminal watuhumiwa wakishashinda kesi tuu na kuachiwa huru, wanashukuru kwa kuona hawana hatia na wala hawajui kuwa wanaweza kufungua kesi za madai na kufidiwa mateso na usumbufu wowote uliotokana na kesi hizo!. Kwenye tasnia ya haki za raia, Watanzania bado tuko nyuma sana!.
Kwa vile kifo cha Kanumba kina public interest element, I hope haka kabinti katakuwa treated fairly!.