GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 306
Wakati uchaguzi wa Arumeru Mashariki ukikaribia , hali kwa baaadhi ya vyama vya upinzani ni tete na haitii matumaini kabisa kwa wao kushinda. Hali hiyo ni mbaya zaidi kwa CDM kwani waliyokuwa wakiyategemea sivyo yalivyo.
- CDM walitegemea wapiga kura wengi ni vijana. Ila imedhihirika kuwa vijana wengi hawakujiandikisha na hawana sifa yakupiga kura. Kwa maana hiyo basi waamuzi wa Mbunge ajae yako kwa wazee na wanawake. Ambapo makundi haya CDM wameyasahau na kujihusisha na vijana tu
- CDM walitegemea utumiaji wa fomu no. 17 uwe ni ukombozi wao. Ila tume ya taifa ya uchaguzi imeisha tangaza kuwa fomu hiyo haijawahi kutumika katika uchaguzi wowote nchini, na kwenye uchaguzi huu wa Arumeru haitatumika. Hii yaonyesha ule mpango wao wakuruhusu hata wasio na shahada za kupiga kura wapige kura umekufa. Na hili ni pigo kubwa sana kwao
- CDM ilifanya harambee ya SADAKA pale Naura, na walikusanya pesa nyingi tu. Ila mpaka sasa pesa hizo hazija saidia sana chama. Kwani kwa tathmini CCM wao walikuwa wanafanya mikutano takribani 30 kwa siku, CDM wao walikuwa 18 kwa siku. Na CCM hivi sasa watafanya mikutano 50 kwa siku, CDM wao 23 kwa siku. Hii yaonyesha , uwezo mdogo wa CDM kufanya mikutano. Sasa tatizo mwanzo tuliambiwa ni pesa, sasa pesa zipo na mikutano haifanyiki kwa wingi