KIBITI: Mtendaji wa Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi wauawa kwa kupigwa risasi

WAZIRI mwenye dhamana mwenyewe anawaogopa hao so-called "wauaji" wa KIBITI maana hataki kuwaongelea kabisa yeye anataka apambane na SOFT TARGETS (kama NGOs) ambao hawajawahi hata kushika bunduki
 
Nakubali kuna maswali ya kufikirisha
1) Inaonyesha kuna set of rules ambazo wanafwata... na theory kwamba wanaua wale watu ambao tu walifanya dhuluma siyo ya kweli, kama wanauwa kwa ajili ya dhuluma basi inaonyesha hapa itakuwa wanaua wale watu wanao 'represent' hiyo dhuluma... Pi kuna swala la wether hawa wauaji ni wenyeji au sio wenyeji, the fact kwamba wanaomba waonyeshwe waliko viingozi...
2)Swala la pili, iweje hawa watu wawe free hivyo ku walk around the village kufanya rampage hiyo na wakati tumeambiwa Jeshi la Polisi, JWTZ, TISS wote wako huko?!!!!!! Aiseee!
Kweli mkuu, lakini nawaza pia kuwa hawa huenda wanatumia silaha zisizotoa sauti kiasi kwamba hata kama vikosi vyetu viko mita 300 tu kutoka eneo la tukio basi wasijue nini kinaendelea. Kibiti ,rufiji, mkuranga, hizi wilaya ni kubwa sana hatuwezi kuweka askari kila eneo
 
Kweli mkuu, lakini nawaza pia kuwa hawa huenda wanatumia silaha zisizotoa sauti kiasi kwamba hata kama vikosi vyetu viko mita 300 tu kutoka eneo la tukio basi wasijue nini kinaendelea. Kibiti ,rufiji, mkuranga, hizi wilaya ni kubwa sana hatuwezi kuweka askari kila eneo
Kweli mkuu hii ya silaha zisizotoa sauti nayo ni tafukuri nyingine ya kuzingatia...
 
mkuu, majeshi yetu yalikuwa busy jana kwenye doria ya "mhalifu" Lowasa, walichoka sana hadi wakachelewa kurejea MKIRU mapema, jamaa waka-take advantage. lakini sasa wamerejea hali ni shwari kama tulivyohakikishiwa na Majaliwa!
we jamaa wewe
 
tuiache serikali ifanye kazi yake na ikishindwa ndipo itatupa majibu sahihi kwamaana sioni kinachoshindikana hapo kibiti ni sehemu ndogo sana sioni ugumu wa kukidhibiti na kuwakamata hao waarifu .
 
na kama imeshindikana basi tuombe msaada wa majeshi ya umoja wa mataifa yaje yatusaidie kupambana na hao majangiri.
 
Hao wanakijiji nao waoga sana, ingekuwa wamekuja kukamatwa na POLISI usiku huo wangejifanya kuitana na kufanya vurugu na kila MTU angesikia, ila kwa majambazi wanekaa kimya hata simu hawajapiga na sio kuwa ni tukio la dakika chache, bali ni muda mwingi! Wananchi zindukeni, mnataka kutawaliwa na aya za shetani.

Hao wanakijiji nao waoga sana, ingekuwa wamekuja kukamatwa na POLISI usiku huo wangejifanya kuitana na kufanya vurugu na kila MTU angesikia, ila kwa majambazi wanekaa kimya hata simu hawajapiga na sio kuwa ni tukio la dakika chache, bali ni muda mwingi! Wananchi zindukeni, mnataka kutawaliwa na aya za shetani.
Sikia tu kuambia hivi mazingira ya watu kuuwawa kama ilivyo huko ni nani anaweza kuthubutu kutoka nje wakati unasikia chuma kinalia,acha kuongea usichojua
 
Nimenukuu yafuatayo na najaribu kufikiri kwa nguvu zaidi...
========

Ndugu aeleza wauaji walivyotekeleza mauaji

Mmoja wa ndugu za marehemu hao (jina linahifadhiwa) amesema watu wanne waliokuwa na bunduki wakiwa wamevaa nguo nyekundu na kuficha sura zao kwa soksi walivamia kijijini hapo saa nne usiku jana.

Amesema watu hao walianza kwenda kwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho (Hamis Bakari Mkima) (30) ambaye alifanikiwa kuwakimbia kabla hawajamfikia.

Amesema watu hao walimpiga na kitu chenye ncha kali katika mguu wake wa kushoto kisha kumrejesha kwake huku wakimtaka awapeleke kwa viongozi mbalimbali wa kijiji hicho.

Alieleza kuwa baada ya hapo walimtaka awapeleke kwa Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho (Mwarami Shamte) (40) na baada ya kufika huko walimpiga risasi tatu na alifariki dunia papo hapo.

Amesema watu hao bado walimtaka mwenyekiti huyo awapeleke kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo na baada ya kufika kwake walimpiga risasi ya usoni iliyoharibu macho yake.

Amesema baada ya hapo walimpiga risasi moja mwenyekiti huyo wa Kijiji cha Mangwi, (Hamis Mkima) na alifariki papo hapo.

Pia ameeleza kuwa wakati watu hao wakifanya hayo walikuwa tayari wamechoma moto nyumba ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo kwa kutumia mafuta ya petroli yaliyokuwemo kwenye pikipiki yake na kuteketeza kabisa nyumba yake yote.

Mdogo wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo (aliyepofuliwa macho) aliyejitambulisha kwa jina la Paul Martin amesema tukio hilo limetokea jana saa 4 usiku ikiwa ni muda mfupi tangu aagane na kaka yake.

“Nilikuwa nyumbani kwake na nimeondoka wakati huo huo kwenda kulala baada ya dakika chache kupita, tulianza kusikia kelele za watu nisiowafahamu wakiwa kwenye nyumba ya kaka yangu,” amesema.

Paul amesema baada ya kusikia kelele hizo alitoka nje ili ashuhudie lakini kabla hajafanya lolote aliwekwa chini ya ulinzi kwa kumulikwa tochi na kutishiwa kupigwa risasi.

"Niliona watu kama watano wakiwa na silaha ambao waliniweka chini ya ulinzi baada ya kunimulika tochi," alisema.

Amesema baadhi ya watu hao walikuwa ndani ya nyumba ya kaka yake wakiendelea kumhoji huku wakiwa wamefunika sura zao.

Ameongeza kuwa baada ya hapo watu hao waliondoka na kaka yake kwenda kusikojulikana na baada ya muda mfupi walirudi naye.

Amesema watu hao baada ya kurejea naye waliwaamrisha watoto wake waliokuwa wamelala kutolewa nje kisha walichukua mafuta ya petroli yaliyokuwa kwenye pikipiki ya kaka yake kisha kuyamwaga ovyo kwenye nyumba hiyo na kuichoma moto.

Amesema baada ya tukio hilo waliondoka naye kwa mara ya pili na kwenda naye kusikojulikana kisha wakampiga risasi ambayo imeharibu macho yake yote.

Amesema baada ya kumpiga risasi hiyo walimtelekeza katika barabara iendayo katika kijiji cha Misimbo ambapo walimkuta leo asubuhi akiwa hajitambui.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Onesmo Lyanga alithibitisha kutokea kwa matukio hayo.

Chanzo: Mwananchi

Baada ya kuweka "bold na underline" nazidi kusema kuna kitu kinaendelea huko Pwani na kuna mambo yanafichwa kimakusudi kabisa. Tunajengewa maswali zaidi kuliko namna ya upatikanaji suluhu na ukomeshaji unyama unaoendelea huko Pwani. Huyo shuhuda kuna mambo hajayaweka wazi kama ilivyo kwa vyombo vya usalama!!!
 
.....nafikiri ni muda tu haujafika,lakini serekali itatuambia nini kilichomo kibiti,haiwezekani na mkono wake mrefu mpaka leo tupo gizani na mauaji yasiyokoma,Mungu ibariki Tanganyika.
 
Back
Top Bottom