Kibano cha Ngeleja Bungeni: Hotuba ya Madini na Nishati 2011

Status
Not open for further replies.
hii miahadi ya miaka nenda rudi wanapoteza muda tuu hapo, sioni km kuna jipya hapoo!
 
Muulizeni atajiuzulu lini????? Tumemchoka! Na Tanesco lini nao watajiuzulu tumewachoka!
 
Miradi 4 ili kukwepa kutegemea nishati ya maji: Mnazi Bay, Kiwira Coal Mines, Tegeta na Ubungo ilianzishwa lakini haikuzalisha vya kutosha....
Wakuu umeme ndio umekatika, tena niko jimboni kwa Ngeleja mwenyewe, wengine mtujulishe kinachoendelea!
 
Tumechoshwa na ahadi za hawa Magamba, haiingii akilini huo umeme wa kutosheleza asilimia 30 utatoka wapi hali leo hii hiyo asilimia 14 tunapata umeme kwa shida, giza kwa siku tatu mfululizo? Hatudanganyiki Ng'o. Tumewachoka CCM
 
hivi kama walitoka hotuba ya mkuu wa kaya kwanini wasioneshe reaction na leo wabunge wa CDM maana inatia kichefuchefu mtu anaonekana anashindwa kutimiza wajibu wake halafu bado wanamlea . step down kistaarabu ......... hakika moto wa jehanamu uko juu yako wewe uliye mnafiki
 
Wakati Naibu Speaker akimkaribisha waziri wa Nishati na Madini, ametahadharisha kuwa wabunge walioomba kuchangia ni wengi sana hivyo watakaopewa kipaumbele ni wale ambao hawajawahi kuongea kabisa na wale waliowahi kuchangia mara moja tu. Maana yake ni kwamba watu makini kama Tundu, Mbowe, Zitto, Mdee n.k hatutawasikia. labda wangoje kwenye kamati

Huu ndio ule UTATU USIOKUWA MTAKATIFU niliokuwa naulaani (Kiti cha Speaker, Wabunge wa CCM na Serikali). Watasema sana mwisho utasikia naunga mkono hoja asilimia 100

Hata mimi nimemsikia na nimeshangaa sana. Haya mambo ya kuleta usanii na ujanja ujanja kwenye mambo magumu yanayogusa maisha ya Watanzania ya kila siku yatatufikisha pabaya.

Ina maana kama Mbunge huwa hachangii siku zote, leo anatoa wapi data za kumfanya achangie? Kuchangia bungeni mara kwa mara kunatokana na uwezo wa kupambanua mambo. Kwa hiyo Mbunge asiyechangia mara kwa mara ni mvivu wa kifikiri na anaweza kuwa mmoja kati ya wale watoro wa vikao au wasinziaji bungeni.

Tusubiri tuone!
 
nimesikia hiyo taarifa imeniuma sana! huyu job na yule mama fikra zao ni sawa sawa. Ngereja yupo na tension kubwa sana. cha maana alichokiona ni kututarifu ujio wa mtoto wake mwingine duh bunge letu la ajabu sana!
 
Jamaa walikuwa na kikao jana kuanzia saa 2 usiku wabunge wote wa magamba,hicho ndicho walichokijadili jana na jinsi ya kuwazuia wapinzani.bajeti imepita tayari wakubwa njoo kwenye maandamano bungeni hatuwawezi kabisa.
 
Spika na naibu spika wamewekwa kwa ajili ya waliowaweka. Hilo bunge lilishanunuliwa na mafisadi.....wapambanaji wayalete kwetu tuamue wenyewe.
 
Wakuu mlioko karibu na runinga zenu mtujulishe kinachoendelea, sisi wengine TANESCO wamefanya mambo yao!
 
Kiti cha Spika (regardless aliyepo ni Spika mwenyewe au Naibu wake) waamue moja, ama waruhusu hoja makini ziongelewe ndani ya jengo huko Dodoma au hoja hizo ziongelewe huku uraini. Lakini wakae wakijua fika kuwa kama hoja 'makini' zitaongelewa huku uraini basi mjadala huo utakuwa ni kwa 'gharama' ya ccm na serikali yake. CHADEMA na wapambaji wengine wala msiwe na wasiwasi, andaeni hoja zenu vizuri kama kiti cha spika kitazuia au wabunge wao (maCCM) watazomea na kuzipiga chini, basi zileteni huku uraini. Huku tuko milioni 40 na ushee na ndio tuna kauli ya mwisho. Zileteni tuzifanyie kazi. Na come 2015 tutamwaga OMO kali kuondoa haya madoa kwenye utawala wa kinafiki unaoibia watu.
 
Wabunge wetu mnaopita humu JF mtusaidie haya kwa huyu Mh:
-Uchakachuaji wa mafuta wameshindwa vipi kuudhibiti kama serikali hadi kupelekea bei ya mafuta ya taa kupanda kiasi hiki. Wanashindwa kuwadhibiti wafanyabiashara kwa sheria kali na usimamizi makini badala wanasalimu amri na kupandisha kodi kwenye mafuta ya taa yanayotumiwa na watu wa kawaida
-Kwa nini wanaendelea kukodi badala ya kununua majenereta ya megawati ndogo hadi 100? Kuna nini hasa kwenye biashara hii ya kukodi?
-Mafuta mazito yanayoendesha mitambo ya IPTL ni tenda ya nani kuyaleta nchini?
 
Sinema la ccm limetengenezwa hao wabunge ambao hawajawahi kuongea wametengenezwa ili wapinzani wasipewe nafasi ya kuzungumzi mambo ya Taifa, kwa kifupi wabunge wa ccm wanamkingia kifua Kilaza Ngeleja.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu agamiza wabunge wa ccm wasiolipenda hili Taifa letu
 
umeme upi watatupa? Miaka saba ameshindwa kuletta umeme wa uhakija...alikuwa wapi???
 
Wawape wale ambao hawajawahi kuchangia? Where were they all this time? Kulala bungeni or kutoa ndoto as to when the day would end so they can continue kutanua? Or when they will get their whole package na wakajijenge before things turn around someday? It is pathetic kuwapa watu kama hao nafasi kuchangia hoja...kwanza hawana hoja, wala hawana uchungu na wananchi, wako pale kuchunga maslahi yao maana wako bungeni basi hilo latosha....wawape nafasi wabunge wenye hoja full stop. Kwani kuna kifungu kinachosema kwamba mbunge asichangie mara kwa mara?
 
Inatia hasira sana. Nitashangaa sana kama wabunge Magamba watamteteaNgeleja. Suala la umeme linatuathiri wote.
 
Kwa hali ilivyo sasa, ilibidi tuwe Dodoma kwa maandamano tunapinga bajeti ya wizara ya nishati na madini na kuwakataa mawaziri, wakurugenzi wote wa wizara na tanesco. Vilele kumtaka waziri mkuu naye ajiuzulu kwani kashindwa. Mamvi alijiuzulu kwa kunshindwa kuwasha umeme kwa kutumia kampuni yenye vifaa chakavu, leo Pinda anatetea ununuzi wa machine za spana mkononi, kweli kazi tunayo. Fedha wamemwachia RA kaondoka nazo.
 
Duh!!! Kinachoniuma sana ni kwamba hao watakaopewa nafasi ya kuzungumza wataanza na shukrani nyingiiiiiii, oooh, mume wangu/mke wangu, watoto wangu, wazazi wangu, wananchi wa jimbo langu, namshukuru mheshimiwa Rais kwa ushindi, PM, spika, naibu spika, etc dakika zikikaribia kuisha "nashukuru sana mheshimiwa naibu spika, naunga mkono hoja". Pumba tuuu wanazungumza huko
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom