Kibano cha Ngeleja Bungeni: Hotuba ya Madini na Nishati 2011

Status
Not open for further replies.

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Nikiwa kama mwananchi natoa ombi halali kwa wabunge wetu ambao leo wanatarajiwa kuijadili bajeti ya wizara ya nishati na madini kuipinga bajeti hiyo.misingi ya kuipinga bajeti hii iko miwili na iko wazi kabisa.Mosi;suala zima la nishati ya umeme limebakia kuwa kero toka waziri huyu ashike wizara hii.wizara inatuhadaa kwa kuingiza mtambo wa Mw 34 siku moja kabla ya bajeti ili tuone wanafanya effort??!Pili;kuhusu nchi yetu kushindwa kunufaika na madini yanayovunwa kila kukicha badala yake tunaumizwa na uchafuzi wa mazingira pamoja na mauaji ya raia.Kama kwa miaka yote zaidi ya minne tunapitisha bajeti na kusisitiza mambo haya haya bila kufanyiwa kazi(wabunge mna uthibitisho) sioni sababu ya kupitisha bajeti hii,badala yake tumuwajibishe kwa kumtaka ajiuzulu.Nawasilisha.
 
Nikiwa kama mwananchi natoa ombi halali kwa wabunge wetu ambao leo wanatarajiwa kuijadili bajeti ya wizara ya nishati na madini.misingi ya kuipinga bajeti hii iko miwili na iko wazi kabisa.Mosi;suala zima la nishati ya umeme limebakia kuwa kero toka waziri huyu ashike wizara hii.wizara inatuhadaa kwa kuingiza mtambo wa Mw 34 siku moja kabla ya bajeti ili tuone wanafanya effort??!Pili;kuhusu nchi yetu kushindwa kunufaika na madini yanayovunwa kila kukicha badala yake tunaumizwa na uchafuzi wa mazingira pamoja na mauaji ya raia.Kama kwa miaka yote zaidi ya minne tunapitisha bajeti na kusisitiza mambo haya haya bila kufanyiwa kazi sioni sababu ya kupitisha bajeti hii,badala yake tumuwajibishe kwa kumtaka ajiuzulu.Nawasilisha.
Nipo kwenye foleni ya chapati hapa ktk Mkahawa wa wapemba nimepita tu! Pole na hongera kwa ndoto Mkuu! Kitu kama hiko hakipo magambaz we hujui!? Bajeti itapita tu. Kama huaminii... Muongo wako mie!
 
Bajeti inapitishwa bungeni na siyo JF. Wewe unatoa kilio hapa unafikiri nani anakusikiliza? Wabunge wenyewe wa CHADEMA hamfikii hata theluthi ya wa CCM halafu unawaza kuzuia bajeti.
 
Eti jana kwenye vyombo vya habari wameonyesha majenereta ndani ya maboksi..hatutaki hizo longolongo zao..
 
Nipo kwenye foleni ya chapati hapa ktk Mkahawa wa wapemba nimepita tu! Pole na hongera kwa ndoto Mkuu! Kitu kama hiko hakipo magambaz we hujui!? Bajeti itapita tu. Kama huaminii... Muongo wako mie!
"ujinga ni kufanya jambo lile ukitegemea matokeo tofauti" ndio maana leo hii nawataka wabunge wetu wafanye MAAMUZI MAGUMU!
 
Bajeti inapitishwa bungeni na siyo JF. Wewe unatoa kilio hapa unafikiri nani anakusikiliza? Wabunge wenyewe wa CHADEMA hamfikii hata theluthi ya wa CCM halafu unawaza kuzuia bajeti.
mimi siwaombi wabunge wa cdm,nawaomba wabunge wa wananchi!najua kuna wabunge wengi tu wanapitia jamvi hili.
 
Wabunge wa ccm walivyo wa ajabu, utawasikia watakapoanza kuchangia: "Kwanza nimshukuru waziri kwa kazi nzuri anayofanya kutekeleza ilani ya chama chetu" Naanza kwa kuunga mkono hoja mia kwa mia". Yaani utadhani kama alivyowahi kusema Hayati baba wa taifa "Kama Mazuzu vile".

Inahitaji uwe na akili mbovu kuipongeza wizara ya Ngeleja. Huu ndo ukweli, lakini kwa vile wabunge wa ccm wamekuwa mawakala wa serikali sifa zote nzuri atapewa Ngeleja. Subiri si bado masaa mawili tu!!.

Taifa hili hapa tulipofika ni Mungu pekee ndiye atakayetuokoa, yaani tusubiri Miujiza. Vinginevyo tuchukue maamuzi magumu. Kwa mfano wabunge wote wakishikamana bila kujali itikadi za vyama vyao na wote kwa pamoja wakasema NO kwa porojo za Ngeleja, utakuwa mwanzo mzuri wa kuiwajibisha serikali hii. Lakini kama tujuavyo utafika ule wakati wa Ndiyooooooooooo. Na mchezo utakuwa ule ule.

Mimi nadhani wabunge wetu wa ccm, wakubali wasikubali WANA LAANA>
 
2015, 30% ya wananchi wote kupata umeme toka 14% ya wananchi wote kwa sasa!
 
huyu jamaa hatumwamini tena, boss wake ameshaachia ngazi sasa sijui yeye kama atapona!!!
 
Maeneo ya vipaumbele: kupeleka umeme hadi vijijini, kuwezesha STAMICO kufanya kazi, kuendeleza Mgodi wa Kiwira, nk.
 
Mafanikio: kukamilika ununuzi mafuta kwa pamoja, kugunduliwa kwa gesi kwenye deep sea, kutungwa kwa sheria mpya ya madini, kupatikana kwa mwekezaji mpya mgodi wa Backleaf, 109 bn/- zilikusanywa!
 
Wakati Naibu Speaker akimkaribisha waziri wa Nishati na Madini, ametahadharisha kuwa wabunge walioomba kuchangia ni wengi sana hivyo watakaopewa kipaumbele ni wale ambao hawajawahi kuongea kabisa na wale waliowahi kuchangia mara moja tu. Maana yake ni kwamba watu makini kama Tundu, Mbowe, Zitto, Mdee n.k hatutawasikia. labda wangoje kwenye kamati

Huu ndio ule UTATU USIOKUWA MTAKATIFU niliokuwa naulaani (Kiti cha Speaker, Wabunge wa CCM na Serikali). Watasema sana mwisho utasikia naunga mkono hoja asilimia 100
 
At least anasema kwamba mgodi wa Resolute umelipa kodi ya TZS 32b kama corporate tax....Ila ukusanyaji wa mirahaba toka kampuni zingine ni TZS 700m tu!
 
Changamoto: kuporomoka kwa TSh kunaongeza gharama za uagizaji mafuta, nk
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom