Kibanda: Msitumie matatizo yangu kisiasa, Nape aumbuka hospitalini!

Kila anayedhuriwa lazima JK aende kumtembelea wa kwanza! Maana hata kwa Kubenea alifanya hivyo hivyo. Uki-connect the dots utajua wazi kwamba "Ikulu haihusiki"!

wewe uliyeandika hii red thread ni wakutiliwa shaka
 
Mungu inusuru nchi yetu. Tunakuhitaji wakati huu. Kila anayefanya mambo ya maana kwa nchi hii anadhuriwa kisha wanasiasa kujipendekeza kama vile hawahusiki. Jamani jamani!!!! kuweni na huruma ndugu zangu hakuna atakayeondoka na haya ya duniani. Vyote tutaviacha. Tuweni na hofu yake aliyetuumba
 
Nape kaenda SA? likizo au kikazi? Wakati wa Mwalimu, makatibu waenezi wa CCM walikua wakisafiri vijijini na mikoani kuimarisha uhai wa chama
 
Nape alikwenda south ktk mkutano ulioandaliwa na chama cha ANC wa vyama vilivyopigania uhuru.so kwenda kumjulia hali kibanda ilikuwa ni hali ya kibinadamu kwakuwa ni mtanzania mwenzake.

Ameenda kama nani coz CCM imezaliwa mwaka 1977, uhuru ulikuwa miaka 12 kabla ya CCM, so sioni mantiki ya Nape kuwa kule
 
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Absalom Kibanda ambaye anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini baada ya kuumizwa vibaya na watu wasiojulikana, amesema ni upuuzi kutumia hali ya afya yake kufanya siasa.

Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, alieleza masikitiko yake hayo jana, wakati akizungumza kwa simu na Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Ansbert Ngurumo. Kauli ya Kibanda inakuja zikiwa ni siku chache tangu mtu aliyejitambulisha kama Ridhiwani Kikwete, atumie ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook kutoa maneno ya kejeli, akihoji kama naye ametekwa na Ikulu.

Kejeli kama hizo pia zilidaiwa kuandikwa katika ukurasa wa facebook wa Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akionesha kufanya propaganda chafu zilizoonesha kama "anawajua" waliomtesa Kibanda. Katika ukurasa huo wa mtu aliyejitambulisha kama Ridhiwani, aliandika: "Je, hii nayo ni kazi ya Rama (Afisa Usalama wa Taifa) wa Ikulu?"

Rama Ighondu ndiye alitajwa na gazeti la MwanaHALISI kuhusika na mateso ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka Juni 26 mwaka jana. Kauli hizo zilichefua kwa kiwango kikubwa viongozi wa juu wa Kampuni ya New Habari anayofanyia kazi Kibanda, kiasi cha kumfanya Ofisa Mtendaji Mkuu, Hussein Bashe kuhoji chanzo chake.

Hata hivyo, kwa nyakati tofauti Nape na Ridhiwani Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, wamekanusha kuhusika kwa namna yoyote kuandika ujumbe huo wa kejeli. Katika utetezi wake, Ridhiwani alidai kuwa kuna mtu ameingilia akaunti yake ya mtandao wa kijamii na hivyo kutumia nafasi hiyo kuandika kejeli hizo.

Katika mazungumzo yake na Ngurumo, licha ya kuzungumza kwa shida huku akisikika vizuri, Kibanda alisema kuwa amekerwa na watu wanaotaka kutumia ugonjwa wake kufanya siasa. "Wanafanya siasa katika hali kama hii? Mambo ya kipuuzi kabisa," alisema. Pia alieleza kuwa Nape alifika hospitalini hapo jana asubuhi kumjulia hali. Hata hivyo, Nape alitaka kupiga picha na Kibanda lakini alikataliwa na walinzi wa hospitalini hapo.

Kuhusu hali ya afya yake, alisema kuwa anasubiri upasuaji wa kuwekewa jicho la bandia baada ya siku 45 kuanzia jana. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika saa 7 alasiri, Kibanda alisema kuwa anasubiri kufanyiwa upasuaji wa pili baada ya jana kurekebishwa uso, taya na meno.

Source: Tanzania Daima
Mtakapokuja kugundua kuwa Riz1 ndiye stirling mwenyewe kwenye uharamia wote mtajiua!! Mimi ninaamini hasa baada ya maneno ya kejeli aliyotoa. Hata hiyo video ya Rwakatare ameibumba!! yeye. Tukishamgundua ni yeye njia ya HAGUE yake na Dhaifu itakuwa NYEUPEEEEEEEEEEEEE!
 
Hawa ndiyo waandishi wetu.

Kama gazeti linachokisema ni kweli, alichowakataza Absolum Kibanda wasikifanye, Tanzania Daima ndiyo wanakifanya.

Tanzania Daima linawafanya wananchi kama wajinga na wasiojua kama hiki wanachoandika ni siasa na propoganda uchwara.

Ngoma ikipigwa sana........

Nimejaribu kurudia kuusoma mchngo waako mara mbili, lakini nimeshindwa kukuelewa ulimaanisha nini uliposema wanachokiandika Tanzania Daima ni siasa na propaganda?

Kwamba Bw. Kibanda hayupo A/Kusini, kwamba hajateswa kama inavyosemwa, kwamba Bw. Ngurumo hawezi kuongea au hakuongea na Kibanda, au kipi ambacho kwako siyo cha kweli???

tafadhali mkuu, fafanua.
 
Mkuu, hizo channel hata kama zingekuwa zinatolewa bure hapa UK, nisingepoteza muda wangu kuziangalia. Sisi huku ni mwendo wa SKY Cable, Freesat, BT Vision na Virgin Tv.

Channel gani hizo hata watayarisha wa vipindi hawajui ni muda upi na kipindi gani kinatakiwa kuwekwa. Hata wanaojiita watangazaji (reporter) hawajui hata kuongea achalia mbali kutangaza.

Hizo ni channel za kufurahisha wageni na wasaka visa Ubalozini London.
pole sana,kumbe kukaa huko umeshasahau kwenu,si ajabu ukawakana hata ndugu zako kisa ubebaji wa maboksi huko,msomi hawezi kutoa majibu ya hovyo namna hiyo,hata jina lako ladhihirisha ulimbukeni wako
 
pole sana,kumbe kukaa huko umeshasahau kwenu,si ajabu ukawakana hata ndugu zako kisa ubebaji wa maboksi huko,msomi hawezi kutoa majibu ya hovyo namna hiyo,hata jina lako ladhihirisha ulimbukeni wako
Nani kakwambia nimesahau kwetu. Kutokuangalia program za TV fake za Tanzania kwako ni kusahau nyumbani. Sikufahamu wewe, lakini nina imani, ninafahamu mengi, may be more than you kuhusu Tanzania pamoja na kwamba makazi yangu yako nje.

Sihitaji kuangalia TV fake za Tanzania kufahamu kwa undani kinachoendelea Tanzania. You may agree or not, huu ndiyo ukweli halisia.
 
Kila anayedhuriwa lazima JK aende kumtembelea wa kwanza! Maana hata kwa Kubenea alifanya hivyo hivyo. Uki-connect the dots utajua wazi kwamba "Ikulu haihusiki"!
hujawaona wachawi wakimloga mtu wanavyogara gara msibani.
 
Nani kakwambia nimesahau kwetu. Kutokuangalia program za TV fake za Tanzania kwako ni kusahau nyumbani. Sikufahamu wewe, lakini nina imani, ninafahamu mengi, may be more than you kuhusu Tanzania pamoja na kwamba makazi yangu yako nje.

Sihitaji kuangalia TV fake za Tanzania kufahamu kwa undani kinachoendelea Tanzania. You may agree or not, huu ndiyo ukweli halisia.
na ikibidi usirudi maana hii haifai tena kuitwa nchi,hakika haina tofauti na kijiwe
 
Back
Top Bottom