kibaka akutana na nyoka LIVE akijaribu kuchomoa wallet!!

COURTESY

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
2,006
706
kiNdugu zangu kweli wizi nooma!
Nimeshudia live kibaka akipiga kelele baada ya kujaribu kumchomoa wallet mtu mmoja kwenye daladala na kukuta ni nyoka.
Tukio hilo limetokea pale ambapo kibaka huyo baada ya kugundua kuwa mhusika ana wallet mfukoni na kuna kila uwezekano wa kuichukua,ndipo alipojaribu mara ya kwanza kumchomoa huyo jamaa,na kushika kitu kama nyoka, hakuishia hapo akajipa moyo na kiuendelea na zoezi lake,akaingiza tena mkono mfukoni ili aichukue na kisha kumshika NYOKA LIVE,Na hapo hapo kibaka huyo akapiga kelele,"dereva simamisha gari kuna mtu kabeba NYOKA".
Dereva bila hiyana akapaki gari pembeni,ndipo kibaka kuulizwa akampoint jamaa,ikabidi jamaa asachiwe,zoezi likafanyika na jamaa akakutwa hana nyoka....ndipo jamaa akaanza kufunguka kwamba ana dawa na kuionyesha live ambayo ukijaribu tu kumuibia kitu kinageuka kuwa nyoka na akamwambia kibaka,we si umejaribu mara ya kwanza kuiba ukakuta nyoka na bado ukaendelea kuiba...kibaka akakubali huku akitetemeka na kukili kuacha tena wizi.hahahahaha nawasilisha
 
iko siku atakuta kunguru kabisa! shenzi wezi wasiokuwa na huruma! maisha magumu kwa wote so sio wengine wafanye kazi wengine wavizie japo hicho kidogo wakiibe
 
Kwa jinsi nijuavyo mimi huyu jamaa hakuwa kibaka labda alikuwa anajifunza kuwz kibaka, kwani angekuwa kibaka najua angeuchuna kwa kuogopa kupigwa tairi na angesepa zake bila watu kugundua
 
Kwa jinsi nijuavyo mimi huyu jamaa hakuwa kibaka labda alikuwa anajifunza kuwz kibaka, kwani angekuwa kibaka najua angeuchuna kwa kuogopa kupigwa tairi na angesepa zake bila watu kugundua
mkuu usifanye mchezo kabisa,nilikuwa sijawah kuona kibaka anatetemeka hadi meno...mwenyewe hakuamini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom