Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Huyo Kamanda wa tabora bado yupo kazini tu? Only in Tanzania!

Haya Majeshi yetu nayo yamejaa majambazi wa hali ya juu. Inasikitisha sana lakini ndiyo hali halisi. Huyo Zombe leo yamemkuta lakini wanaofanya haya ndani ya majeshi yetu ni wengi tu na wanajua jinsi ya kuyamaliza bila kugundulika. Angalia ule mradi wa Meremeta uliosemekana ulikuwa wa jeshi, hakuna hata kiongozi mmoja wa jeshi aliyetoa sauti yake. Najua hawastahili kusema chochote maana ni nyeti za SIRI KALI!
 
Habari zaidi!

Zombe ageukwa

Maulid Ahmed
Daily News; Thursday,September 25, 2008 @19:58

.Ilitokea baada ya maungamo ya Rashid na Rajabu
.Awali waliandika maelezo kwa maelekezo ya kukana

MKUU wa Upelelezi wa kesi inayomkabili aliyekuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi, Abdallah Zombe na wenzake 12, ameieleza Mahakama Kuu kuwa karibu watuhumiwa wote walipotakiwa kuandika maelezo yao kwa mara ya pili, walimgeuka Zombe.

Watuhumiwa hao katika maelezo yao walionyesha kuwa wafanyabiashara watatu wa madini wa Mahenge na dereva teksi waliuawa katika Msitu wa Pande uliopo Mbezi Luisi, Dar es Salaam na si Sinza.

Mkuu huyo, Sydney Mkumbi bila kutaja idadi ya watuhumiwa hao, aliieleza mahakama kuwa wakati watuhumiwa hao wakiwa rumande, waliamriwa kuandika maelezo yao upya baada ya watuhumiwa Rashid Lema na Rajab Bakari kutoa maelezo ya maungamo yao yaliyoeleza kuwa wafanyabiashara hao, waliuawa katika Msitu wa Pande na si Sinza kama ilivyodaiwa na polisi.

Akihojiwa na Wakili wa utetezi, Majura Magafu mbele ya Jaji Kiongozi, Salum Massati, Mkumbi ambaye ni shahidi wa 36, alidai watu hao walikamatwa Sinza Palestina Block C kwa utaratibu bila mashambulizi na kwenda kuuawa katika msitu huo. Pia hawakuwa majambazi na hawajahusika na wizi wa kampuni ya Bidco.

"Watuhumiwa karibu wote walipokuwa rumande tuliwataka kuandika maelezo yao kwa mara ya pili na yote yalifanana na yaliyotolewa na Rashidi na Rajabu," alieleza katika ushahidi wake.

Rashidi na Rajabu pamoja na kudai watu hao waliuawa katika Msitu wa Pande katika maungamo yao, pia walieleza kuwa katika maelezo yao ya awali, watuhumiwa wote walipewa kikaratasi na Zombe kilichokuwa kimechapwa kwa taipureta kikiwaelekeza namna ya kuandika maelekezo yao ambayo ni tofauti na tukio halisi.

Rajabu Bakari, ambaye ni mshitakiwa wa 12, alijisalimisha polisi Julai 7, 2006 na mshitakiwa wa 11, Rashid Lema alijisalimisha Machi 6, 2006 na kutoa maelezo yao ya maungamo.

Katika kesi hiyo inayoendelea leo, Zombe na askari 12 wanatuhumiwa kuwaua wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro kwa madai ni majambazi ambao ni Ephraim Sabinus Chigumbi, Sabinus Chigumbi (Jongo), Mathias Lunkombe na dereva teksi Juma Ndugu.

Tukio hilo lilitokea Januari 14, 2006 katika msitu wa Pande, Mbezi Luisi Dar es Salaam.

Katika ushahidi wake, Mkumbi aliieleza Mahakama kuwa mshitakiwa wa nne, Konstebo Noel Leonard wa Kituo cha Polisi cha Chuo Kikuu na mshitakiwa wa sita, Nyangelera Moris wa Kituo cha Polisi Urafiki, licha ya kutokwenda katika Msitu wa Pande kushuhudia mauaji hayo, wameshitakiwa kutokana na kutoa maelezo ya uongo kwa polisi.

Askari wasiokwenda msitu wa Pande walikuwa watatu ambapo mmoja kati yao shahidi huyo alidai hamkumbuki.

"Wao waliungana na wenzao na kudanganya katika maelezo yao kuwa waliouawa walikuwa majambazi na waliiba Bidco wakati si sahihi," alidai. Hata hivyo, Jaji Massati alipomhoji shahidi kwa namna gani askari wadogo walihusika katika tukio hilo wangewezaje kuzuia matukio ya Sinza na katika Msitu wa Pande yasitokee, Mkumbi alijibu "walitakiwa baada ya kutoka katika msitu wa Pande immediately (haraka) waripoti tukio hilo kwa ofisa yeyote wa polisi."

Sehemu ya mahojiano kati ya wakili Magafu na shahidi huyo wa 36 ambaye ni Mpelelezi Mkuu katika kesi inayomkabili Zombe na wenzake 12, Sydney Mkumbi yalikuwa kama ifuatavyo: Wakili: Unafahamu washitakiwa wanakabiliwa na nini?

Shahidi: Nafahamu, kosa la mauaji Wakili: Wapi? Wakili: Katika Msitu wa Pande uliopo Mbezi Luisi.

Wakili: Zombe alikuwapo? Shahidi: Hakwenda msituni. Wakili: Zombe alikuwapo Sinza wakati marehemu wanakamatwa? Shahidi: Hakuwapo. Wakili: Imedaiwa kulikuwepo mapambano kati ya marehemu na askari katika ukuta wa Posta huko Sinza, je, Zombe alikuwepo? Shahidi: Kwenye mapambano hakuwepo.

Wakili: Ukiachilia mbali maelezo ya Rashidi kuwa Zombe aliwasiliana na mshitakiwa wa pili yaani Christopher Bageni, kuna sehemu Zombe amehusishwa? Shahidi: Mshtakiwa namba mbili aliandika barua kwa DCI akitaka Tibaigana awepo. Wakili: Unayo?

Shahidi: Sina hapa? Wakili: Jana hukusema. Shahidi: Ningeulizwa ningesema. Wakili: Umezua leo asubuhi hii. Shahidi: Wewe ndiyo umezua? Wakili: Katika upelelezi wako, kuna sehemu uligundua watuhumiwa walikaa pamoja wakasuka njama za kuwaua hao marehemu? Shahidi: Kwa mtiririko ulivyo walikuwa pamoja, walikutana Block C na wakasema ‘tumeamriwa tukachinje'

Wakili: Waliwasiliana? Shahidi: Ndiyo kwa simu ya upepo na mawasiliano ya simu ya mkononi.

Wakili: Unazifahamu simu za Zombe na Bageni? Shahidi: Nilikuwa nazijua lakini sasa sizijui tena. Wakili: Ulienda kufuatilia mazungumzo yao katika ofisi za simu? Shahidi: Nilifanya hivyo, niliagiza kwa maneno Wakili: Ulipata majibu?

Shahidi: Nilipata majibu kuwa muda ulishapita kwani Vodacom wanatunza maongezi kwa miezi sita halafu wana destroy. Wakili: Kuua ni amri halali?

Shahidi: Si amri halali. Wakili: Nikiwa na bosi wangu nikamuona anaiba nami ntakuwa nimefanya kosa? Shahidi: Utawajibika, kwa nini usizuie wizi usitendeke?

Wakili: Akiwa na silaha mimi sina je? Shahidi: Ungetakiwa uripoti ofisa fulani ametenda kosa ukinyamaza unahusika. Wakili: Kuna malalamiko askari walichukua pesa za marehemu.

Shahidi: Nilisikia, lakini hilo ni kosa la wizi Wakili: Mtu anaweza kuuawa pasipo sababu? Shahidi: Inawezekana. Wakili: Swali langu la msingi sasa linasema ili uweze kumwua mtu lazima uwe na chuki naye kama si bahati mbaya? Shahidi: Lazima sababu iwepo.

Wakili: Washtakiwa walikuwa wakifahamiana na marehemu? Shahidi: Hawafahamiani. Wakili: Unakubaliana nami kama si tukio la Bidco wasingekutana?

Shahidi: Ni kweli. Wakili: Katibu wa Tume ya Kipenka alikuambia washtakiwa walipora pesa? Shahidi: Sikumhoji.

Wakili: Hapa mahakamani imedaiwa sababu ya wale kuuawa ni askari walipora pesa, ulifahamu? Shahidi: Nilifahamu baadaye. Wakili: Hadi sasa hufahamu?

Shahidi: Nafahamu kwa sababu ya ushahidi wa kina Lunje Wakili: Si mliwapandikiza? Shahidi: Nafsi iliwasuta. Wakili: Mlipewa kazi nzuri, lakini mlikuwa biased Shahidi: Uliza swali Wakili: Uliwahi kumuuliza Bageni begi la pesa lilikwenda wapi? Shahidi: Sikumhoji.

Wakili: Rashidi na Rajabu hawakuwa wakweli, unasemaje? Shahidi: Walikuwepo katika tukio, hawakukiri kuua walishuhudia mauaji. Wakili: Nani mashahidi?

Shahidi: Wote waliamriwa kuandika maelezo yao upya, walifuatwa rumande na karibu wote isipokuwa mshitakiwa wa kwanza (Zombe) waliandika maelezo yanayofanana na Rashidi na Rajabu. Wakili: Rashidi alisema walipewa kikaratasi, ni kweli?

Shahidi: Ndiyo alipewa na akasema ‘hata mke wangu simuachii, ntakuwa nacho mwenyewe'

Wakili: Kilikuwa na saini ya mkubwa? Shahidi: Alinionyesha tu na sikuona saini Wakili: Ni mwandiko wa mtu au typing? Shahidi: Kiliandikwa kwa typewriter . Baada ya kuhojiwa na Magafu,

Mkumbi alihojiwa na wakili Longino Myovela na mahojiano yao yalikuwa kama ifuatavyo: Wakili: Kama mpelelezi unaamini Koplo Saad aliua? Shahidi: Naamini

Wakili: Ungekuwa katika Tume ungewaingiza hawa wengine (watuhumiwa 12) wakati Saad ndo ameua?

Shahidi: Uchunguzi ungeniongoza. Wakili: Kuwakamata marehemu ni kosa? Shahidi: Si kosa wanatekeleza kazi ya polisi.

Wakili: Ni lazima junior polisi atekeleze amri ya wakubwa? Shahidi: Ni sahihi kutekeleza amri ya kiongozi Wakili: Kwenda msitu wa Pande kwa amri ni sawa?

Shahidi: Ni amri halali kwenda msitu wa Pande, lakini utekelezaji wake si halali. Wakili: Zaidi ya kuona Saad akiua, Rashid alikuambia nini? Shahidi: Rashidi alisema Bageni alikuwa anawasiliana kwa simu na kiongozi wake kwa sababu alikuwa akisema ‘afande afande'.
 
ivi hii kesi itaisha lini mana naona wanapoteza hela bure tu kuweka mafuta kwenye yale magari kumpeleka mahakamani kila siku,nafikiri kuna leads nyingi tu kila ukisoma kwenye magazeti amehusika kwa namna mmoja ama nyingine sasa ya nini poteza muda!!!
 
Hata mimi naona atashinda sababu yeye wala hakuwepo eneo la tukio zaidi ya kutoa amri "isiyo halali" kwenye simu..!!
 
Hata mimi naona atashinda sababu yeye wala hakuwepo eneo la tukio zaidi ya kutoa amri "isiyo halali" kwenye simu..!!

Practically hakushiriki. or tuseme hakushiriki direct but indirect. Ila kosa analo la ku engineer mauaji na akawa mjanza hata sehemu ya mauaji hakwenda. Kisheria atachukuliwa hatua either kufungwa kwa muda fulani but not life imprisonment or sentensed to death. Katika utetezi wote actual killers through Zombes Instructions are at large (huyo afande Saadat na mwingineo).

Ila generally Zombe amehusika katika crimes nyingi sana ila tu ni kwamba hakuweza kukamatwa kwa ushahidi. Ushahidi wa exhibit ndiyo tu unaweza kumtia mtu hatiani kisawasawa. Ule wa maneno mara nyingi hata hakimu anaweza kuuchezea rafu hasa kwa Tanzania where njaa ni iissue.

Pesa vipambe 30 vilinunua vaza la Yesu, ni hatari ni kifo ni laana tosha. Watu wanatafuta fedha kwa njia haramu mno, ndiyo maana utasikia mara EPA, Richmond, Dowans, Agreko, you name all na list hutaimaliza.

Wanasheria tusaidieni hapa au tuseme ndo mko buss kutafuta mihela ya uwakili. Njooni jamvini.
 
ivi akishinda alafu hao askari wengine wakahukumiwa nafikiri lazima wataongea tu mana hapo lazima kuna kutegeana tu mana kama mission ilikua moja basi wote lazima wakutwe na hatia sio huyu na huyu wafungwe na wengine wawe huru
 
Hivi sheria za kiafande si ni kutekeleza unayo ambiwa na bosi bila kuhoji, hapo itakuwaje kwa hao subordinate wa Zombe? nadhani kosa lao wao ni kule kushirki kuficha hiyo siri ya amri potofu, but walitekeleza amri halali ya bosi wao.
 
Hilo neno "Masikini" lingeondolewa kwenye heading maana mtu kama Zombe hata kama hajahukumiwa hastahili kuonewa huruma
 
True obedience is to refuse doing what is wrong
-Confucius
 
kWELI KABISA MASIKINI YA NINI HAPO?SI TUACHE MAHAKAMA IFANYE KAZI YAKE...MBONA KAMA MNATOA HUKUMU MAPEMA?
 
Hata mimi naona atashinda sababu yeye wala hakuwepo eneo la tukio zaidi ya kutoa amri "isiyo halali" kwenye simu..!!

Atashinda kwasababu alitowa amri "Isiyo Halali" Iliyopelekea mauwaji ya raia wema na uporaji wa mali zao....
Kweli wewe ni yebo yebo...Yani unaamuwa hii kesi kama huko sokoni unauza vitumbua ama nyanya na vitunguu.
Tumia ubongo kabla huja type....Hakuwepo kwenye tukio kwasababu hakuwa na haja ya kuwepo kwenye tukio.
Hata Saddam Hussein hakuwepo kwenye matukio yaliyopelekea yeye kunyongwa...Lakini alitowa amri "Isiyo halali" ya Mauwaji hayo.
Tuna kazi kama wanamtandao ndio hivi na wananchi hawana haja ya kulaumiwa...Nini hiki?
 
JMushi1,

Sasa kashfa za nini?

Maoni yangu yametokana na hiyo habari hapo mwanzo; mimi sikuwepo mahakamani labda wewe ulikuwepo au ni mmoja wa wapelelezi wa kesi hivyo unajua zaidi yangu.

Unalinganisha kesi ya Saddam Hussein (iliyotokea Iraq kwa shinikizo la USA) na hii ya Zombe, Tanzania..!! Nitawaachia wasoma wachuje nani anayefikiri kabla ya kuandika.

Hiyo habari imeweka taarifa zifuatazo ambazo mimi nimezitumia kutoa kutoa mawazo yangu:

- Zombe hakuwepo maeneo yote ya tukio.

- "Inasemekana" (kwa mujibu hiyo habari; sababu hakuna ushahidi Vodacom walishafuta) kuwa alitoa amri wafanyabiasha wauwawe.

- Muuwaji mwenyewe hajapatikana mpaka leo hivyo ushahidi wake haujulikani ungekuwaje - Pengine yeye alikuwa anawajua hao watu aliowaua na aliwaua kwa sababu zake - hatujui.

- Inasemekana (again, hakuna ushahidi) kuwa wafanyabiashara waliuwawa kwa nia ya kuporwa hela. Hela zilizoporwa hakuna aliyeziona wala hakuna alithibitisha wakati wanakamatwa walikuwa na fedha. (hakuna motive)

- Inasemekana (Zombe alitoa waraka wa maelezo, ulioandikwa na Type Writer - sio mkono wake) na kuwapa marehemu waandike upya maelezo yao.

- Ukiondoa "TUHUMA" ya kuwa Zombe alitoa amri kwenye simu na huo waraka ambao hakuandika kwa mkono wake: hakuna pengine ambapo Zombe amehusishwa kwa mujibu wa hiyo habari.

- Maadili ya polisi ni ukipewa amri unatekeleza lakini baadae unalalamika au kutoa taarifa kwa ofisa wa juu; hao polisi wa vyeo vya chini sio tu kwamba walitekeleza amri bila kutoa maalezo walipopata nafasi ya kufanya hivyo, lakini pia walitoa ushahidi wa uwongo.

Ndio maana nikafupisha na kusema amri isiyo halali na Zombe hakuwepo eneo la tukio.

Iwapo una sababu za kupinga hoja yangu iweke hapa kwenye baraza bila kashfa.
 
Kama kichwa cha habari kinavyosema....Zombe ageukwa na mashahidi...Sasa hapo waliopewa amri si ndio mashahidi?

Ama nimeelewa tofauti?

Kwasababu wewe umesema with confirmation kama alivyofanya Masatu...Kuwa Zombe anashinda kesi..At the same time wewe unadai kuwa sijui kinachoendelea kwenye kesi...Mimi nachangia kutokana na mada ilivyoletwa...Kuwa hao sasa ni mashahidi waliokuwa upande wa Zombe ama waliokuwa wamesukwa ili kuficha ukweli...Kama umesahahu walisema wameambiwa wakachinje...Na wao wamepokea amri ya kuchinja kutoka juu....Sasa wewe unakurupuka na kutaka kujustify kiurahisi kuwa atashinda....Just kwa sababu hakuna saini yake na ni type writer tu.

Nyundo huanzia juu na si chini.

NB:Nimeambatanisha quote hii hapo chini...Kuna ushahidi wa amri hiyo kutolewa na kama kuna mashahidi wa kudhibitisha kuwa simu ya upepo ilitumika kusambaza habari hizo....Waliwasiliana kwa simu ya upepo na cellphones wakakutana Sinza...Na dili lilisukwa na ndio maana kuna logic na cause...Haikutokea kwa bahati mbaya...There was intetion and a probable cause...Pia hata kama ni maandishi ya type writer na ni ya ofisini kwake pia bado yuko responsible..Pia aliyepeleka kikaratasi hicho alipewa amri na ni shahidi madhubuti sana tu....Hao watu wamepokea amri na aliyetowa amri yuko responsible.

Shahidi: Sina hapa? Wakili: Jana hukusema. Shahidi: Ningeulizwa ningesema. Wakili: Umezua leo asubuhi hii. Shahidi: Wewe ndiyo umezua? Wakili: Katika upelelezi wako, kuna sehemu uligundua watuhumiwa walikaa pamoja wakasuka njama za kuwaua hao marehemu? Shahidi: Kwa mtiririko ulivyo walikuwa pamoja, walikutana Block C na wakasema ‘tumeamriwa tukachinje'

Wakili: Waliwasiliana? Shahidi: Ndiyo kwa simu ya upepo na mawasiliano ya simu ya mkononi.
 
twategeme haki sasa itatendeka.
ushahidi uliokwishwa kukusanywa unatosha saana, tafadhali sana mh massati fanya kweli
 
Kama kichwa cha habari kinavyosema....Zombe ageukwa na mashahidi...Sasa hapo waliopewa amri si ndio mashahidi?
Ama nimeelewa tofauti?

Kwasababu wewe umesema with confirmation kama alivyofanya Masatu...Kuwa Zombe anashinda kesi..At the same time wewe unadai kuwa sijui kinachoendelea kwenye kesi...Mimi nachangia kutokana na mada ilivyoletwa...Kuwa hao sasa ni mashahidi waliokuwa upande wa Zombe ama waliokuwa wamesukwa ili kuficha ukweli...Kama umesahahu walisema wameambiwa wakachinje...Na wao wamepokea amri ya kuchinja kutoka juu....Sasa wewe unakurupuka na kutaka kujustify kiurahisi kuwa atashinda....Just kwa sababu hakuna saini yake na ni type writer tu.

Nyundo huanzia juu na si chini.

NB:Nimeambatanisha quote hii hapo chini...Kuna ushahidi wa amri hiyo kutolewa na kama kuna mashahidi wa kudhibitisha kuwa simu ya upepo ilitumika kusambaza habari hizo....Waliwasiliana kwa simu ya upepo na cellphones wakakutana Sinza...Na dili lilisukwa na ndio maana kuna logic na cause...Haikutokea kwa bahati mbaya...There was intetion and a probable cause...Pia hata kama ni maandishi ya type writer na ni ya ofisini kwake pia bado yuko responsible..Pia aliyepeleka kikaratasi hicho alipewa amri na ni shahidi madhubuti sana tu....Hao watu wamepokea amri na aliyetowa amri yuko responsible.

1. Hao mashahidi ambao leo wanasema Zombe alitoa amri si ndio hao ha na wao wanashitakiwa pamoja na Zombe? Sasa hapo huoni kuwa ili kuondoa conflict of interest kutatakiwa wapepo mashahidi ambao “hawakuhusika” kwenye hii kesi?

2. Kwenye hiyo habari ni wapi wamesema kuna mashahidi waliothibisha Zombe alitoa amri zaidi ya hao anaoshitakiwa nao?

3. Kama hao mashahidi walikuwa upande wa Zombe na sasa wamemgeuka bado unategemea mahakama inayosimamia haki kuyapo uzito ushahidi wao huo wa kindumila kuwili?

4. Sijasema ilitokea kwa bahati mbaya: Hiyo imeeleza vizuri kuwa hakuna ushahidi unaonyesha zipo hela zilizoibiwa?

5. Tuonyeshe kwenye hiyo habari panapobainisha kuwa wauwaji walikuwa na “intention” ya kuua kwa sababu ya hela.
 
Naona jamaa mpaka next year ndio wanaweza kumhukumu....kwa sasa kesi imefungwa na moderator wanaweza ku imove this topic kwenye closed topic....ili tuwe na nafasi ya kujadili mengine....nini cha kufanya before the end of the year...if is not end the year ukiwa huna madeni....au ukiwa nayo....na what to do next year...ni miezi 3 kabla hatujamaliza mwaka we need some focus on that.....

Good evining.
 
Hilo neno "Masikini" lingeondolewa kwenye heading maana mtu kama Zombe hata kama hajahukumiwa hastahili kuonewa huruma

Dada yangu Naima, hakuna binadamu (mwenye mwili na damu na Nyama / "aliye zaliwa na mwanamke") ambaye hastahili kuonewa huruma.

Hakuna binadamu asiyefanya kosa.

Hakuna binadamu asiyejutia kosa alilofanya hata kimoyomoyo

Lakini mshahara wa Dhambi ni Mauti.
 
Back
Top Bottom