Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Zombe aelemewa Mahakamani

*Mashahidi 50 kueleza alivyoua

Na Grace Michael

SHAHIDI katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Morogoro inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Dar es Salaam Bw. Abdallah Zombe na wenzake ameieleza mahakama namna marehemu hao walivyokamatwa na askari polisi na kuchukua simu zao pamoja na begi lililokuwa kwenye gari lao.

Hayo yalisemwa na shahidi wa pili wa upande wa mashitaka Bi. Bernadetha Lyimo (35) wakati akitoa ushahidi wake katika Mahakama Kuu ya Tanzania mbele ya Jaji Kiongozi Salum Masati.

Akiongozwa na wakili wa upande wa mashitaka, Bw. Jasson Kishozi ilikuwa kama ifuatavyo;

Swali; Shahidi unaishi wapi?

Jibu; Naishi Sinza Palestina.

Swali; Unakumbuka Januari 14 mwaka juzi ulikuwa wapi na nini kilitokea?

Jibu; Nilikuwa nyumbani kwangu na mida ya jioni walikuja shemeji zangu (marehemu) ambao tayari nilikuwa na taarifa nao kutoka kwa mume wangu.

Swali; Walikukuta wapi?

Jibu; Nilikuwa barazani nje na walipofika nilinyanyuka na kwenda kuwapokea lakini walikataa kuingia ndani kwa madai kuwa walikuwa na haraka hivyo nilimwomba marehemu Sabinus Chingumbi niongee naye pembeni.

Tulichepuka kidogo na shemeji yangu ambaye alinipa sh. 30,000 kama alivyokuwa ameagizwa na mume wangu na kuagana nao lakini kitendo cha kuingia mimi ndani na kutoka tayari walikuwa wamezingirwa na askari polisi ambao walikuwa na silaha.

Niliwaona shemeji zangu wakiwa wamenyoosha mikono juu na wale askari niliwaona 'wakiwasachi' na kuchukua simu zao za mikononi na marehemu Chingumbi alikuwa na bastola nayo waliichukua japo nilimsikia akiwaambia anaimiliki kihalali.

Baada ya muda kidogo lilikuja gari dogo lililokuwa na wanaume wawili na mwanamke mmoja ambapo mmoja kati yao alikwenda kwenye gari ya marehemu na kufungua nyuma ambako kulikuwa na 'brifikesi' nyeusi na baada ya kuifungua kulikuwa na mfuko mweusi.

Walichukua begi lile na kulihamishia kwenye gari la askari na kuwapandisha watu hao wakiwa wamefungwa pingu mikononi na kuondoka nao na gari la marehemu lilikuwa likiendeshwa na askari mmoja kati yao.

Swali; Je ulifanya nini?

Jibu; Nilikwenda ndani na kumjulisha mume wangu kilichotokea ambaye aliniambia atafuatilia kwa marafiki zake na angenipa taarifa zaidi.

Katika ushahidi wa shahidi wa kwanza Bw. Methew Ngonyani ambaye ni mume wake na Bi. Lyimo aliiambia mahakama kuwa baada ya kupewa taarifa na mkewe, alianza mawasiliano na watu mbalimbali ili waweze kufuatilia kituo walichopelekwa rafiki zake.

Bw. Ngonyani ambaye alikuwa akiongozwa na Bw. Kaitila Mutaki alieleza kuwa anafahamiana vizuri na marehemu kutokana na kazi ya uchimbaji madini anayoifanya.

Alisema kuwa taarifa ya safari ya kuja Dar es Salaam alikuwa nayo na marehemu aliondoka na madini ambayo yalikuwa na thamani ya sh. milioni 150 hadi milioni 200 ambayo kidogo yaliuzwa Arusha na mengine walitarajia kuyauza Dar es Salaam.

Bw. Ngonyani aliieleza mahakama kuwa marehemu hawajawahi kupatikana katika matukio ya uhalifu hivyo walikuwa ni watu safi wakifanya biashara zao.

Katika kuwasiliana na watu mbalimbali ili kujua marehemu wako kituo gani Bw. Ngonyani hakufanikiwa, badala yake alipata taarifa kuwa rafiki zake wameuawa na askari polisi na alipoagiza mtu kwenda Muhimbili kuangalia maiti hizo naye alikamatwa na polisi.

Alieleza kuwa marehemu walikuwa wamefikia katika Hoteli ya Bondeni iliyoko Magomeni na tangu walipokamatwa hawakurudi tena hotelini hapo.

Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa mashahidi hao upande wa utetezi ukiongozwa na wakili, Bw. Majura Magafu aliiarifu mahakama kuwa washitakiwa wote hawakuwa kwenye tukio ambako mauaji hayo yalitokea.

Upande wa mashitaka ulisema kuwa unatarajia kuwa na mashahidi 50 ambao wataeleza namna walivyokamatwa marehemu na namna walivyopelekwa katika msitu wa Pande kuuawa na vielelezo vingi ambavyo vilipatikana katika eneo la tukio akiwemo daktari bingwa atayethibitisha vifo vya marehemu hao.

Upande huo pia ulisema kuwa katika usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo unathibitisha kuwa marehemu walipigwa risasi. Washitakiwa hao wanatetewa na jopo la mawakili sita.

Kesi hiyo ina mvuto kwa wananchi wengi ambao walifurika kwenye mahakama hiyo kusikiliza mwenendo wake mzima wakiwemo ndugu wa marehemu.

Washitakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa kuwa Januari 14, mwaka juzi wakiwa katika msitu wa Pande Luis ulioko Mbezi, Dar es Salaam walimuua kwa makusudi Bw. Ephraim Chigumbi, Bw. Sabinusi Chigumbi, Bw. Juma Ndugu na Bw. Mathias Lukombe.

Washitakiwa hao ni Bw. Zombe, Bw. Bageni, Bw. Makele, F5912 Noel, YP4513 Jane, D6440 Nyangerella, D1406 Mabula, E6712 Felix, D8289 Michael, D2300 Abeneth, B1321 Rashid, D4656 Rajab na D1367 Philipo. Kesi inaendelea leo.
 
Ushahidi kesi ya Zombe watisha

na Asha Bani

SHAHIDI wa tatu katika kesi ya mauaji inayomkabili aliyewahi kuwa Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe na wenzake 12, jana alitoa ushahidi uliowaacha midomo wazi watu wanaofuatilia kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa katika Mahakama Kuu juzi.

Akiongozwa na wakili, Angaza Mwaipopo, shahidi huyo, Venance Mchami, alidai mahakamani hapo kuwa, Zombe alikuwa mmoja wa watu waliomtesa wakati alipokamatwa na polisi kwa tuhuma za ujambazi.

Mchami aliieleza mahakama hiyo kuwa, alikamatwa wakati akienda kutambua miili ya wafanyabiashara wenzake waliouawa, iliyokuwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Mchami, ambaye ni mfanyabiashara ya madini wa Mahenge kama walivyokuwa jamaa zake waliouawa, alitoa ushahidi huo mbele ya Jaji Mkuu Kiongozi, Salum Masati, na kuongozwa na jopo la mawakili wanne wa serikali ambao ni Jasson Kaishozi, Alexander Mzikila, Mwaipopo na Mugaya Mtaki.

Sehemu ya mahojiano baina ya shahidi huyo na Mwaipopo yalikuwa kama ifuatavyo:

Wakili: Unaweza kuielezea mahakama una uhusiano gani na marehemu na mlianza kufahamiana lini?

Shahidi: Marehemu watatu ambao ni Ephraim Chigumbi, Sabinus Chigumbi au Jongo na Mathius Lunkombe ni wafanyabiashara wenzangu ambao tunamiliki mgodi mmoja Mahenge.

“Nilianza kufahamiana nao tangu mwaka 1990 wakati huo kina Chigumbi walikuwa kama vibarua katika migodi ya wafanyabiashara wengine, lakini hadi wanafariki Sabinus Chigumbi alikuwa anamiliki mgodi wake.”

Wakili: Unakumbuka Januari 14 mwaka juzi ulikuwa wapi na ni nini kilitokea?

Shahidi: Nakumbuka nilikuwa nyumbani kwangu Ubungo, ghafla nikapokea simu kutoka kwa Mathew Alex Ngonyani, ambaye alikuwa ananitaarifu kuwa kina Sabinus na wenzake watatu wamekamatwa na polisi wakiwa wanatoka nyumbani kwake kupeleka fedha za matumizi kwa mke wake.

Wakili: Baada ya hapo nini kilitokea?

Shahidi: Nilianza kumpigia simu Mathias Lunkombe lakini iliita na kuzimwa baada ya muda mfupi, nikaanza kumpigia simu Jongo, ikapokewa na mtu mwingine ambaye alinijibu wako Arusha.

Shahidi huyo aliendelea kuieleza mahakama kuwa, baada ya kuona hawapati kwa njia ya simu, ndipo alipoamua kwenda kuwatafuta katika vituo mbalimbali vya plisi, akianzia katika Kituo cha Urafiki, Mabatini na Kituo Kikuu cha Polisi, ambapo kote walijibiwa kuwa hawakuwaona watu kama hao.

Shahidi alieleza baada ya kushindwa kufanikiwa katika vituo vyote vya polisi Dar es Salaam, waliamua kwenda Muhimbili, ili aweze kuzitambua maiti zilizokuwepo katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Alidai aliambatana na ndugu wa marehemu watatu, ambao yeye hakuwafahamu majina yao hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti na alipofika nesi aliyekuwa zamu siku hiyo aliwaambia wasubiri kwa muda, ili aweze kuwapunguza watu waliokuwa wamefurika sehemu hiyo.

Alieleza kuwa alisubiri kwa muda wa dakika 20, ndipo nesi aliporejea na kuanza kumwambia aandike majina ya marehemu hao kama kweli anawatambua, ili aweze kumruhusu kuangalia.

Venance alieleza aliwatambua wafanyabiashara wenzake ambapo aliwakuta wakiwa na majeraha sehemu mbalimbali.

Akifafanua, alisema kuwa maiti ya Jongo ilikuwa imekatwa sehemu zake za siri, na kuongeza kuwa, alikuwa na alama za risasi katika kichwa sehemu ya kisogoni na katika paji la uso.

Alieleza kuwa maiti ya Lunkombe ilikuwa imekatwa vidole vyake vyote vya miguuni pamoja na nguo alizokuwa amevaa zilikuwa zimechanika.

Alisema marehemu Ndugu, ambaye alikuwa dereva wa teksi waliyoikodi wafanyabiashara wenzake, alikuwa amechinjwa sehemu ya koo, huku akiwa na majeraha ya risasi kwenye paji la uso na kisogoni, na marehemu Ephraim Chigumbi, alikuwa amekatwa sehemu ya kifuani na kulikuwa na matundu ya risasi katika paji la uso na kisogoni.

Mara baada ya shahidi huyo kumaliza kuelezea jinsi alivyokuta majeraha katika mwili wa marehemu, baadhi ya wasikilizaji waliokuwa mahakamani humo, ambao wanadhaniwa kuwa ni ndugu wa mmoja wa marehemu hao, walisikika wakipiga kelele za mishangao, kiasi cha kumlazimu wakili kunyamaza kwa muda, hadi hapo wananchi hao waliponyamaza.

Akiendelea kutoa ushahidi, Mchami alisema kuwa, alipatwa na huzuni kubwa alipowaona rafiki zake wakiwa katika hali hiyo, huku ndugu za marehemu alioongozana nao wakiangua vilio.

Alidai baada ya kuona marehemu wakiwa katika hali ya utupu aliamua kutoa sh 5,000 kwa nesi wa zamu, ili aweze kupatiwa shuka na kuwahifadhi.

Alieleza wakati anaanza kuwafunika, ghafla walitokea polisi wanne ambao walipiga teke mlango wa chumba hicho na kuanza kuwapiga vibao huku wakisema kuwa ni majambazi wenzao, ambao wanamtandao mkubwa Dar es Salaam.

Mchami aliieleza mahakama kuwa awali aliwabishia askari hao, lakini walimkamata kwa nguvu na kumfunga pingu mikononi na miguuni na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi.

Alipofikishwa kituoni hapo, alisema kuwa aliingizwa katika chumba cha maabusu ambamo aliwekwa peke yake huku wenzake wakiwa wamewekwa katika mahabusu za kawaida.

Alisema akiwa chumbani humo, aliwasikia maofisa mbalimbali wa polisi wakiwa wanabishana na kuelekezana kwamba wampeleke kwa Zombe, kwani yuko juu ofisini.

Alieleza baada ya muda walimchukua na kumpeleka kwa Zombe, ambapo askari mmoja aliyekuwa karibu yake alimnyang’anya dola 500 alizokuwa nazo pamoja na simu, huku akitishia kumpiga.

Alieleza kuwa wakati hayo yanatokea, alimweleza askari huyo kuwa ana wakili wake, ambaye anaweza kumtetea na aliposema hivyo, askari huyo alionekana kuwa mwoga na kuacha kumpiga.

Venance alidai baada ya hapo walimchukua na kumpeleka kwa Zombe, ambapo alielezwa na Zombe kuwa yeye (Mchami) ni mwanamtandao na kwamba atamuua, kwa kuwa yuko pamoja na marehemu ambao Zombe alidai kuwa ni majambazi.

“Zombe aliniambia na wewe lazima uuawe kwa kuwa unawafahamu hawa wenzako huku akiwa ananionyesha silaha na kuipiga katika vyuma vilivyokuwepo karibu yake,” alieleza.

Alieleza kuwa Zombe alikuwa anatoa vitisho huku akiwa anapiga piga miguu yake chini na kufoka huku akimuonyesha bastola na kumtishia kila mara kuwa atamuua.

Alisema wakati akiwa ofisini humo, aliwasikia wenzake aliokamatwa nao Muhimbili, ambao walikuwa wamehifadhiwa katika chumba kingine, wakipiga kelele huku wakilia kutokana na maumivu.

Alisema baada ya kutolewa kwa Zombe, alirudishwa mahabusu na siku iliyofuatia alifika baba yake aitwaye William Mchami, ambaye ni mwanajeshi mstaafu pamoja na mke wake aliyemtaja kwa jina la Jane.

Alieleza baada ya kufika kwa ndugu zake hao, Zombe alipomuona baba yake alishtuka na kumuuliza iwapo aliyekamatwa alikuwa mwanawe.

Alisema kuwa baada ya baba yake kumweleza kuwa ni mwanawe, Zombe aliamuru afunguliwe pingu huku akiwafokea askari wa chini yake kwa nini walimfunga pingu wakati yeye si mtuhumiwa.

Mchami alisema kuwa, Zombe aliamuru apelekwe katika Kituo cha Polisi Oysterbay, ili kuhojiwa zaidi, na alipofika aliambiwa akaonane na Polisi Christopher Bageni, ambaye alimtambua mahakamani kama mtuhumiwa namba mbili.

Aliieleza mahakama kuwa alipokuwa Polisi, Bageni aliandika maelezo yake na ndipo alipodhaminiwa na baba yake.

Naye shahidi wa nne katika kesi hiyo, ambaye ni mdogo wa marehemu Mathias Lunkombe, Protas Lunkombe, alieleza mahakama jinsi alivyokimbia Dar es Salaam, kwa kuhofiwa kuuawa kutokana na kukosa imani ya polisi, baada ya kuuawa kwa ndugu zake ambao hawakuwa majambazi.

Awali, Protas aliithibitishia mahakama kuwa, aliongozana na ndugu zake kwenda Arusha kutafuta soko la madini Januari 9, lakini yeye alirudi Mahenge baada ya kutoka Arusha kutokana na dada yake kulazwa hospitali.

Aliendelea kuielezea mahakama kuwa ndugu zake walikuwa na madini yenye thamani ya sh milioni 200, ambayo pia yalitoweka baada ya ndugu zake kuuawa.

Akielezea kuhusu kumtambua Zombe, alidai kuwa anamtambua kutokana na kumuona katika luninga akiwa anajigamba kuwa wamefanikiwa kuua majambazi wanne.

“Namtambua sana Zombe kwa kuwa nilimuona mara ya kwanza katika televisheni akisema kuwa waliouawa ni majambazi na kwamba walipambana nao,” alieleza Protas.

Alieleza alifanikiwa kuwaaga ndugu zake wakati wa mazishi na kuwaona wakiwa na majeraha ya risasi sehemu za mdomoni.

Mara baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake, wakili wa upande wa utetezi, Majura Magafu, alimuuliza shahidi kama aliwahi kuandika maelezo sehemu yoyote au kwenda kulalamika katika kituo chochote cha Polisi.

Protasi alieleza kuwa aliwahi kuandika maelezo katika kituo cha Polisi na katika Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Mussa Kipenka.

Wakili Magafu alimuuliza shahidi kama aliwahi kulipwa posho yoyote wakati wa mahojiano na tume, na Protas alieleza kutopewa chochote.

Hata hivyo, kabla ya kuanza kwa mahakama, shahidi huyo alionekana kuwashtua baadhi ya watuhumiwa, ambao walianza kunong’onezana na kuandikiana ujumbe kwenye vikaratasi.

Baadaye ilifahamika kuwa hali hiyo ilisababishwa na shahidi huyo kufanana sana na marehemu Mathias Lunkombe, lakini ilielezwa kuwa ni pacha wake.

Huku akiwa anaficha sura, shahidi huyo alisema anafahamu askari hao wanashangaa nini.

“Wanadhani mimi ni marehemu nimefufuka, lakini mimi yule ni pacha wangu, tumefanana sana,” alisema nje ya mahakama.

Wengine wanaoshitakiwa katika kesi hiyo pamoja na Zombe na Bageni ni F. 5912 Konstebo Noel Leornad, WP. 4593 Konstebo Jane Andrew, D. 6440 Koplo Nyangelera Moris na D. 1406 Koplo Emmanuel Mabula.

Wengine ni E. 6712 Koplo Felic Sandsy Cedrick , D. 8289 Konstebo Michael Shonza, D. 2300 Koplo Abeneth Saro, D. 4656 D/Koplo Rajabu Bakari na D. 1367 D/ Koplo Festus Gwabisabi.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa leo ambapo mashahidi wawili watatoa ushahidi wao.
 
Kesi ya Zombe: Shahidi: Askari wa kike aling'ang'ania fuko la pesa

Na Grace Michael

SHAHIDI wa sita wa upande wa mashitaka katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Dar es Salaam, Bw. Abdallah Zombe na wenzake Bw. Mjata Kayamba (30) amedai siku ya tukio mshitakiwa WP 4513 Jane Andrew aling'ang'ania kubeba begi lililokuwa na mamilioni ya fedha za marehemu.

Bw. Kayamba alidai hivyo jana alipokuwa akitoa ushahidi Mahakama Kuu mbele ya Jaji Salum Masati wakati akiongozwa na Wakili wa Serikali, Bw. Jasson Kaishozi.

Alidai Januari 14, 2006 akiwa maeneo ya nyumbani kwake Sinza Palestina, muda wa jioni aliona gari aina ya Toyota Mark II iliyokuwa na abiria watatu ambao ni marehemu ikiegeshwa na wale abiria walishuka na kuelekea kwa Bi. Benadetha Ngonyani ambaye walizungumza naye wakiwa barazani.

Alidai marehemu hao aliona wakimkabidhi Benadetha kitu ambacho hakufahamu kilikuwa ni kitu gani kisha kuagana, mama huyo alirudi ndani na wale walipanda gari ambalo lilianza kugeuza kuondoka.

Likiwa katika harakati za kugeuza ghafla ilitokea gari la askari Toyota Pick up ya bluu ambayo ubavuni iliandikwa Polisi na lilikuwa na askari wasiopungua watano, watatu walikuwa na sare na silaha.

Alidai gari hilo la Polisi lilizuia gari walilokuwa wamepanda marehemu, askari walishuka na kufungua mlango wa gari la marehemu na kuwashusha abiria na kuwaambia ni majambazi, muda huo huo walianza kuwapekua.

Upekuzi huo ulifanyika katika maungo yao, kati yao mmoja alikuwa na bastola ambaye ni marehemu Sabinus Jongo, wakati wakiwapekuwa hakuna risasi yoyote iliyopigwa na marehemu wengine walikutwa na simu selula.

Askari wakiendelea na kazi hiyo waliwatahadharisha raia wajihami kwani hao walikuwa ni majambazi, waliamuru kufunguliwa kwa buti ya gari la marehemu ambapo walikuta begi ambayo ndani ilikuwa na mfuko mweusi wenye fedha.

Shahidi aliendelea kudai kwamba baada ya kutolewa mfuko wenye fedha alisikika askari mmoja akiuliza ndani ya ule mfuko kuna nini, marehemu alijibu kuna sh. milioni 5, askari huyo alibeba mfuko huo wenye fedha ghafla ilifika gari aina ya Toyora Corola iliyokuwa na askari watatu akiwemo mwanamke mmoja.

Walipofika askari wa kike aliomba kubeba mfuko wenye fedha, askari wenzie hawakukubali maombi yake hivyo waliamuru abebe aliyekuwa nao awali na wakati huo marehemu wakiomba mfuko huo wabebe wenyewe na kama wana hatia wapelekwe kituoni.

"Niliona marehemu wakifungwa pingu na kupakizwa ndani ya gari, gari la marehemu liliendeshwa na askari mmoja aliyekuwa na sare za polisi, gari zote ziliondoka," alidai.

Shahidi alidai mahakamani kwamba anaweza kuwatambua askari aliowaona siku ya tukio ambao ni aliyekuwa Mratibu wa Polisi Ahmed Makelle na Jane Andrew aliyekua aking'ang'ania akabidhiwe mfuko wenye fedha.

Alidai hadi marehemu wanaondoka na Polisi hawakuwa na majeraha hadi kesho yake alipopata taarifa kutoka kwa jirani yake, Benadetha kuwa waliuawa.

Shahidi wa tano akitoa ushahidi mahakamani hapo akiongozwa na Wakili wa upande wa Mashitaka Bw. Mugaya Mtaki, Bi. Jane Awino (42) alidai alipata shida kubwa kumtoa kwa dhamana mumewe aliyeingizwa katika kesi hiyo kimakosa.

Shahidi huyo alidai mumewe alienda mochwari kwa ajili ya kutambua marehemu, alimpigia simu kumfahamisha mahali alipo na kumtaka asimpigie simu hadi atakapomfahamisha kinachoendelea.

Alidai alisubiri bila kupata taarifa yoyote hadi kesho yake alipoamua kumpigia simu, Bw. Mathew Ngonyani kumuulizia taarifa za mumewe, alimwambia asubiri kidogo atamjulisha.

Shahidi alidai baada ya muda alifahamishwa na Ngonyani kwamba mumewe anahojiwa mahali, aliogopa na kuamua kumfahamisha baba mkwe wake ambaye alimtaka aende nyumbani kwake.

Alidai walishauriana kwenda Kituo cha Polisi Muhimbili, walipofika hawakumpata, askari mmoja alimshauri aende Kituo Kikuu cha Kati akamuone Zombe ataweza kumsaidia.

Walikwenda kituoni hapo na kuuliza mapokezi, hakukuta jina la mumewe katika kitabu, aliendelea kuchanganyikiwa, wakati akishuka alikutana na askari ambaye alimfahamisha tatizo lake, alimjibu kwa kumtaka amsubiri Zombe amsaidie.

Shahidi alidai hakuwa akimfahamu Zombe, baba mkwe wake alimuona Zombe akija, alizungumza naye na aliwajibu kwamba hajui.

Askari mwingine alimuongoza amtafute askari aitwaye Andrew ili amsaidie, walimpata kwa simu, aliwataka waende nyumbani kwake, walipofika aliwajulisha kuwa Venance ambaye ni mumewe yuko pale pale kituoni.

Alidai walipofuatilia siku ya pili, walijibiwa kuwa washitakiwa walipelekwa Kituo cha Polisi cha Kati kwa ajili mapumziko, suala lao lilipaswa kushughulikiwa na Christopher Bageni ambaye ni mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo.

Baada ya kushindwa kumpata mumewe, walishauriana na mkwewe waende Makao Makuu ya Polisi, walionana na aliyekuwa Msemaji wa Jeshi la Polisi, Bw. Aden Mwamunyange ambaye aliwapa askari Samson waongozane naye hadi kwa Zombe na wakifika wampigie simu, walipofika walifukuzwa wote, baba mkwe wake alifahamishwa kwamba mwanaye ni jambazi aondoke hatakiwi kuonekana kituoni hapo.

Shahidi alifahamishwa kwamba mumewe ni jambazi, atasikilizwa hadi hapo atakapomtafutia mama Ngonyani, waliagizwa kushuka chini na kupata msaada kutoka kwa askari wengine ambao walimpa barua ya kupeleka kwa Bageni.

Bageni alimsaidia kwa kumpa dhamana mumewe pamoja na wengine wote waliokamatwa katika utambuzi wa marehemu. Shahidi aliwatambua mshitakiwa Zombe na Bageni, baada ya kufanya hivyo washitakiwa hao waliinamisha vichwa chini na kucheka.

Kesi inatarajia kuendelea kusikilizwa leo ambapo shahidi wa saba atatoa ushahidi wake.

Washitakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa kuwa Januari 14, mwaka juzi wakiwa katika msitu wa Pande Luisi ulioko Mbezi, Dar es Salaam walimuua kwa makusudi Bw. Ephraim Chigumbi, Bw. Sabinusi Chigumbi, Bw. Juma Ndugu na Bw. Mathias Lukombe.

Washitakiwa hao ni Bw. Zombe, Bw. Bageni, Bw. Makele, F5912 Noel, WP4513 Jane, D6440 Nyangerella, D1406 Mabula, E6712 Felix, D8289 Michael, D2300 Abeneth, B1321 Rashid, D4656 Rajab na D1367 Philipo.
 
Zombe atoa kioja kortini

* Anukuu Biblia, adai wakili amefuata posho

Na Grace Michael

ALIYEKUWA Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abdallah Zombe anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini,jana alitoa mpya kortini baada ya kunukuu vifungu vya Biblia na Katiba huku akimshambulia kwa maneno Wakili wa Serikali, Bw. Mugaya Mutaki kwa madai kwamba ametoka Arusha kuja Dar es Salaam kufuata posho.

Tukio hilo la aina yake lilitokea jana Mahakama Kuu ya Tanzania mbele ya Jaji Salum Masati wakati akiwasilisha hoja binafsi ambapo pia alimshutumu Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) na Jeshi la Polisi kwa madai kuwa wamemfikisha mahakamani bila kosa .

"Mtukufu Jaji hapa Katiba inatakiwa itumike ili kufikia haki kwani ni marufuku kumkamata mtu kinyume cha sheria, kitendo cha DPP na Polisi kunileta hapa mahakamani sikielewi kabisa, kushitakiwa kwangu ni kwa chuki za watu binafsi !" Alilalamika.

Huku akiendelea kulalamika, Bw. Zombe alinukuu vifungu mbalimbali vya Katiba ya nchi na mstari wa Biblia kutoka Kitabu cha Yohana 7:51 unaosema "Usimhukumu mtu bila kumsikiliza na ibara ya 13 na 15 ya Katiba.

Alisema upande wa mashitaka unao mashahidi wengi hususani askari polisi ambao wanapatikana kwa urahisi zaidi hivyo kinachofanywa na upande huo kuleta mashahidi wachache sio sahihi kwani kesi hiyo ni kubwa na ina hisia kubwa kwa jamii.

Akijibu hoja hizo , Bw. Mutaki alisema hoja ya Bw. Zombe ingekuwa sahihi zaidi endapo ingewasilishwa na mawakili wake ambao amewaajiri kwa kazi hiyo lakini hata anacholalamikia si sahihi kwani kesi iko mahakamani na inaendelea kusikilizwa hivyo awe mvumilivu.

Pia alisema kuwa suala la kuita mashahidi wengi halina tatizo na kama mahakama itakuwa tayari, upande huo upewe muda wa nusu saa ili uweze kuleta shahidi mwingine.

Bw. Zombe, alisema ameshitakiwa kwa chuki ndio maana mpaka sasa hajaandika maelezo yoyote kuhusiana na kosa hilo. Akijibu hoja hiyo, Bw. Mutaki alisema suala la maelezo si la msingi sana kwani upande huo hauzuiliwi kumshitaki kwa kutokuwa na maelezo hivyo kuwa nayo au kutokuwa nayo ni hiari ya mtu na sio kikwazo cha kesi.

Wakati Bw. Mutaki akiendelea kueleza hayo, ghafla Bw. Zombe aliingilia kati na kumrushia maneno makali akisema "Wewe si umetoka Arusha huko, unatafuta night (posho) tu !"

Baada ya kauli hiyo ya mshitakiwa huyo, Bw. Mutaki alimtaka kuondoa hoja hiyo mara moja na kumwambia kuwa hayuko hapo kwa ajili ya posho bali kazi.
Wakili wa mshitakiwa huyo, Bw. Jerome Msemwa aliomba radhi kutokana na kauli ya mteja wake.

Akiahirisha kesi hiyo Jaji Masati, alisema kwa malalamiko hayo kama anaona haki imekiukwa, ana haki ya kufungua kesi ya kikatiba na hapo sio mahali pake.

Baada ya Jaji kuondoka katika chumba cha mahakama hali ya kurushiana maneno iliendelea kati ya Bw. Zombe na baadhi ya mawakili wa upande wa mashitaka ambao walisikika wakisema kuwa hawako hapo kwa ajili ya posho kwani wao ni waajiriwa wa serikali.

Hatua hiyo ilikuwa gumzo nje ya mahakama ambapo watu wengi waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo walisikitishwa na kauli ya Bw. Zombe kutokana na kuwa yeye alikuwa ni askari polisi ambaye naye alikuwa akikamata watuhumiwa na kati yao hawakuwa na makosa.

"Tunamshangaa sana anavyolalamika mbona wapo wengine aliokuwa akiwakamata hata wale waliokwenda kutambua maiti mochwari hawakuwepo hata kwenye vitabu vya Polisi ? Alihoji mmoja wa wasikilizaji wa kesi hiyo.
 
"Mtukufu Jaji hapa Katiba inatakiwa itumike ili kufikia haki kwani ni marufuku kumkamata mtu kinyume cha sheria, kitendo cha DPP na Polisi kunileta hapa mahakamani sikielewi kabisa, kushitakiwa kwangu ni kwa chuki za watu binafsi !" Alilalamika.

Huku akiendelea kulalamika, Bw. Zombe alinukuu vifungu mbalimbali vya Katiba ya nchi na mstari wa Biblia kutoka Kitabu cha Yohana 7:51 unaosema "Usimhukumu mtu bila kumsikiliza na ibara ya 13 na 15 ya Katiba.

source; http://majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=6833

naam huku kesi ikieendelea bw zaombe anaonekana kutaka watu tuamini kuwa kesi dhidi yake ni chuki tu.

kama ni chuki iwe juu ya nn? na watu gani? au wenyewe huko wamedhulumiana na kumtoa kafara?
 
Hapa mkuu kuna kitu.......yeye alishika bunduki aliwaua hao jamaa??au alitoa amri ya kuuawa kwa hawa jamaa?
 
hii kesi jamani mbona mie nashangaaa huku iko on de low profile??!as natamani sana kujua ukweli wa mambo as sikwepo huko wakati yatokea na basi hata hizo tetesi sina...guys jamani wa huko ufisadini tupeni more mamboz basi on this case
 
senx alot mtoa habari yaan guys kip on up2date us more on this kesi as nasikia itakua yasomwa kila day sina uhakika abt weekends si mwajua tena JF ndo kama gazeti kwa wengine?kila siku yabidi ujipatie nakala yako...actually kila majira as asubuhi mchana na jioni bila kusahau usiku
 
Zombe asitake kudanganya watu. Tunamjua vizuri...Huyu ni mtu ambaye alikuwa anatumia vijana wake kunyanyasa wafanyabiashara mbalimbali na kuwapora hela zao.

Ilikuwa ngumu kuprove case nyingi lakini Mungu si Athumani akajilengesha...
 
Mtu ambaye hakuwahi kufika mikononi mwa zombe na kundi lote lile atasema zombe anaonewa lakini kama uliwahi kufika mikononi mwa zombe na kundi lake hasa yule mwanamama Jane anajua wale marehemu walipitia wakati gani.

Kipindi kile nchi ilikuwa imeoza kwani polisi ndo walikuwa majambazi, mchana mkiona TZR imepita jioni jiandaeni kwani wanasurvey na kurudi usiku, walikuwa wanaiba mtaa kwa kufuata mfulilizo wan nyumba zilivyojipanga leo wakiishia hapa kesho wanaanzia hapo kama hawajapumzika kwa wiki moja.
 
kesi hii imeamsha hisia kali sana za wana jamii hasa waliowahi kupata kipigo na mateso makalitoka kwa bw Zombe....jamani huyu baba alikuwa jasiri na katili hasa....majambazi walikuwa wanamhara sana huyu bw...ila hata...wanyonge alikuwa anawakandamiza maana alizoea sana kudaka...cha juu....hata kwa kuwakandamiza wanyonge.....alizoea sana rushwa kubwa kubwa........na ubabe...time itatuambiaa.....
 
mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mchungu!yeye kucheleweshwa tu anaona soo!na alivyowatoa innocent people uhai wao!hata nafasi ya kujieleza hakuwapa!na hadi leo yale madini waliyokuwa nayo hayajulikani yalipo!Na bado.Cha kushangaza anakoti mistari ya bible si mchezo leo anajua kuwa kuna MUNGU?
 
wewe jaji jamani mbona hivyo si MHKUMU KIFO HUYO JAMANI MNAWAPOTEZEA MUDA WA NINI WANANCHI KUHANGAIKA MAHAKAMANI KILA SIKU JAMANI ADHABU IKO WAZI
CHINJA HUYO JAMANI....NYIE MAJAJI MBONA HIVYOOOOOOOO HUYO MUUWAJI NJE NJE CHINJA HUYO MPELEKENI DODOMA AKFIE UKO AONE UCHHUNGU WAKE NA HII NI KWA TAARIFA YENU TU....WALE WATU WALIPELEKWA SEHEEMU KULE MBEZI YULE ASKARI WA KIKE AKAWATUPIA MADINI KWA MBELE HUKU AMEWAFUNGA MIKONO AKASEMA NENDENI MKAOOKOTE MADINI WAKATI WANAYAFYATA WAKAJUA WAMEACHIWA MASKINI WAKASIKIA BASTOLA NYUMA YAO OOOHHHH MA GOD ....MAHITA HAWA WATU ULIKUWA UKIWALINDA KWASABABU YA TEN PEC ZA MAJAMBAZI UNAONA WANAKUAIBISHA MASIHARA USISHANGAE KUJA HUMO NDANI S
 
kwa jinsi alivyodata inaonyesha kuwa jamaa anaamini kuwa atashinda kesi au kuna uwezekano wa kutoka.Miezi hiyo kidogo aliyokaa korokoroni bado ana picha ya Tanzania aliyoiacha, angejua kuwa Tz na Watz wamebadilika sana ktk kipindi kifupi cha miezi michache aliyokaa ndani asingetoa malalamiko ya kibwege hivyo. Jamaa hajui kuwa hata BWM naye huenda wakakutana huko huko kwa pilato !!!!!!!
 
"Mtukufu Jaji hapa Katiba inatakiwa itumike ili kufikia haki kwani ni marufuku kumkamata mtu kinyume cha sheria, kitendo cha DPP na Polisi kunileta hapa mahakamani sikielewi kabisa, kushitakiwa kwangu ni kwa chuki za watu binafsi !" Alilalamika.

Huku akiendelea kulalamika, Bw. Zombe alinukuu vifungu mbalimbali vya Katiba ya nchi na mstari wa Biblia kutoka Kitabu cha Yohana 7:51 unaosema "Usimhukumu mtu bila kumsikiliza na ibara ya 13 na 15 ya Katiba.


Zombe hana jipya,kama kafara kajitoa mwenyewe,na anavyojifanya ana hasira anaweza akapata kesi nyingine
 
zombeafoka.jpg

mkuu anaonesha jinsi alivyokuwa akitekeleza kazi zake.


ukimuangalia tu utajua hili ni jambazi
 
Zombe hizi sheria na maonevu ameanza kutajua lini ? Je wale waliokuwa anawakamata na kuwatesa wakati ule hakuwa anajua Katiba ama ndiyo madaraka tena ?
 
Niliposoma maelezo ya yule shahidi wa kwanza kwenye kesi ya Zombe basi nikajua kweli hawa jamaa nao walikuwa ni victims wa uhuni roho mbaya aliyokuwa nayo Zombe.

Kila kitu alichoelezea kilichowapata marehemu hao ni kama ambao yalishawahi kunipata mimi kwa amri za aina hiyo hiyo za Zombe.

Nilikuwa Post Office Moshi siku hiyo sitakaa nisahau.
Kuna mtu nilikuwa nimempa ride na mimi nilikuwa nimebaki kwenye gari nikimsubiri jamaa yangu huku nikila mziki laini ndani ya gari lenye namba za kigeni za SA.

Wakati bado nikiwa ndani ya gari mawazo yangu yakiwa mbali ghafla nikaona gari (through side mirror) Ghafla lime block nyuma yangu.

Gari aina ya defender ikiwa na maaskari wengine kanzu na wenye mavazi yao ya kipolisi huku waiwa na misilaa kama vile ni raid flani hivi ya majambazi.

Maajabu ni kwamba nilikuwa nikiwafahamu zaidi ya wawili ama watatu wa hao maaskari kanzu.

Ghafla mmoja wao akaingiza mkono na kuchomoa funguo za gari...Na kufungua mlango huku wakiniamrisha kushuka kutoka kwenye gari.

Nikamwambia mmoja wa wale niliokuwa nikiwafahamu..Ni nini tena ndugu yangu kuvamiana kama majambazi?

Yeye mwenyewe alikuwa akinieleza kwa masikitiko kuwa ni amri kutoka kwa Zombe.

Baada ya jamaa yangu naye kurudi kutoka Posta...Tukajumuishwa wote ndani ya gari na mmoja wa wale waliovalia kiraia akawa ndiye mwendeshajiwa gari lile nilolokuwa nalo...Baada ya kufikishwa kituoni ndio nikakutana na Zombe mwenyewe kwa mara ya kwanza!
Na ndugu zangu story ya shahidi yule ni kama yale yaliyonipata hivyo hivyo..Amri ilitoka kwa Zombe aliyekuwa upastairs ofisini kwake na kufoka walete wa*** huku juu.

Vitisho kama alivyosema yule bwana ni the same..Tofauti ni kwamba hakuwa na bunduki kama yule shahidi mwingine alivyokuwa akisema..Bali alikuwa na kamera...Na bastola moja ikiwa mezani nahuku akivuta midroo yake kwa vurugu nyingi..Na kuikamata bastola yake mara kwa mara..Huku tukiwa tumekalishwa chini ofisini kwake kama vile tayari sisi ni majambazi ama vibaka!

Huku akiongea kwa vitisho na mara nyingine kejeli..Huku akitupiga mipicha ya kila namna na kudai kuwa sisi ni majambazi na huku akitisha kutukanyaga usoni!

Jamaa yangu alikuwa akifikiri ni kama masikhara vile akatabasam...Jamaa akamtukana matusi ya nguoni na huku akisema jambazi mkubwa we na maneno kede kede.
Baada ya vitisho na unyanyasaji mwingi ndio tukapelekwa chini lock up kusubiri wadhamini.
Huyu bwana kusema kweli alikuwa anajuwa kabisa kuwa wale watu walikuwa innocent!

Na mimi huwezi kujuwa labda ni Mungu alisaidia kukawa na maafisa wengine waliokuwa wakijuwa kabisa kuwa amri ya bosi wao ilikuwa na walakini kwani mimi si jambazi na wao walikuwa wakifahamu kuhusu gari hilo.
Huu unyanyasaji wake naona umefikia kikomo na ni malipo ya Mungu kwa unyama wote aliwahi kuufanya dhidi ya raia wema huku akiwalinda majambazi!

Yeye ndiye mmojawapo aliyekuwa akitoa amri za kuwanyanyasa raia huku ujambazi ukishamiri akiwa in charge wa upelelezi.
Mabilioni waliyojivunia wakiwa na kina Mahita ni mtandao wa kigaidi uliokuwa ukiwalenga raia wema specifically na kuwa wasindikizaji wa majambazi kwenye matukio yao ya uamabazi!
Wewe unaweza kuona polisi wametokea ukadhani kuwa ni msaada ukaja ukashangaa wanakumalizia wao wenyewe!
Na hayo ndiyo yaliyotokea kwenye kesi hii ya Zombe!
Na asijidahi kuongea maneno ya dini sasa hivi!
Labda atakuwa amegeuka na kuwa mlokole akiwa huko jela...Kitu ambacho mke wake ambaye ni mlokole alikuwa akimlimlilia sana afanye hivyo !

Ama kweli Mungu si Zombe!
 
Back
Top Bottom