Kesi ya Mahanga dhidi ya Msemakweli Kainerugaba Yafutwa

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
Dk. Mahanga aingia mitini sakata la vyeti feki
Makongoro-Mahanga.jpg

Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Makongoro Mahanga

NAIBU Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Makongoro Mahanga, ameshindwa kufika mahakamani kuthibitisha kwamba kashfa ya kughushi vyeti ilikuwa ya uongo.

Hayo yamebainika baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuifuta kesi ya madai ya kashfa ya kughushi vyeti iliyokuwa imefunguliwa na Dk. Mahanga dhidi ya Mwanaharakati, Kainerugaba Msemakweli na wenzake.

Kesi hiyo ilifutwa jana na mahakama hiyo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa Dk. Mahanga alishindwa kutokea siku ya kesi yake.

Dk. Mahanga alifungua kesi hiyo ya madai namba 145/2009 dhidi ya Mwanaharakati, Kainerugaba Msemakweli na wenzake kwa madai kuwa walimtuhumu kuwa ameghushi vyeti vya elimu.

Mbali na Msemakweli wadaiwa wengine ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe, Muhibu Saidi, Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo na Kampuni ya The Guardian Limited waliokuwa wanatetewa na Wakili wa kujitegemea, Michael Ngaro.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Salvatory Bongole ambaye alisema amefikia uamuzi huo kwa sababu Wakili wa mlalamikaji, Kennedy Fungamtama na mlalamikaji wamekuwa hawafiki mahakamani bila kutoa taarifa na kwamba kuna ushahidi unaonyesha wito wa kuitwa mahakamani ulikuwa ukiwafikia kwa wakati.

Jaji Bongole alisema ametumia amri ya tisa kanuni ya nane ya Sheria ya Madai ya mwaka 2002 na kwamba ameifuta kesi hiyo kwa gharama.

Kwa mujibu wa hati ya madai, Dk. Mahanga alikuwa akiomba wadaiwa wamlipe Sh bilioni tatu ambazo ni fidia ya madhara aliyoyapata kutokana na habari ya uongo iliyochapishwa na wadaiwa katika Gazeti la Nipashe la Oktoba 19, mwaka 2009 iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho, ‘Vyeti vya Elimu: Mawaziri sita wanasa'.


Chanzo: Mtanzania
 
Mwenye vyeti vya mahanga atupie hapa tuvifanyie assessment.
[h=2]Member of Parliament CV[/h]
GENERAL
SalutationHonourableMember picture
1133.jpg
First Name: Dr. Milton
Middle Name: Makongoro
Last Name:Mahanga
Member Type:Constituency Member
Constituent: Segerea
Political Party: CCM
Office Location: P.O. Box 1422, Dar es Salaam
Office Phone: +255 753 806 018/+255 712 196 272/+255 683 119 999
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail: mmahanga@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Date of Birth 3 April 1955
EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start DateEnd DateLevel
Washington International UniversityPhD19982000PHD
Strathclyde University (UK)MSc. Finance19971998MASTERS DEGREE
National Board of Accountant & Auditors -NBAA(T)CPA (Professional Degree)19771983ADV DIPLOMA
Institute of Finance Management(IFM)Taxation Course19781979DIPLOMA
National Board for Material Management, Dar es SalaamProcurement & Supply Course19781980DIPLOMA
Tambaza Secondary SchoolA-Level Education19771978HIGH SCHOOL
Mara Secondary SchoolO-Level Education19711975SECONDARY
Kyambai (Matare) Primary SchoolPrimary Education19651968PRIMARY
Mugumu Primary SchoolPrimary Education19691970PRIMARY
Bukama Ikizu Primary SchoolPrimary Education19711971PRIMARY
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From To
Ministry of Labour, Employment and Youth DevelopmentDeputy Minister5/12/2008Todate
The Parliament of TanzaniaMember - Segerea Constituency20102015
Ministry of Infrastructure DevelopmentDeputy Minister20065/12/2008
The Parliament of TanzaniaMember - Ukonga Constituency20002010
National Housing Co-operation(NHC)Director of Finance & Administration19942000
University of Dar es SalaamBursar19911994
NIC Motors LtdChief Accountant19851991
Air Tanzania Corporation(ATC)Senior Accountant19841985
Nyegezi Social Training InstituteSenior Lecturer19801983
Ministry of FinanceAssistant Finance Officer19761979
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position FromTo
CCM-Chama Cha Mapinduzi Member - National Executive Committee20072010
CCM-Chama Cha MapinduziMember of Parliament20002015
CCM-Chama Cha MapinduziMember - Ilala District Executive Commission20002010
CCM-Chama Cha Mapinduzi/TANUCadre1969Todate
 
Back
Top Bottom