Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,061
- 16,751
Hizi ndizo mbinu zinazo taka kusukwa hapa, uzuri wa Dk.Magufuli hawezi kubabaishwa na ujinga wa watu wachache wenye wivu wa kijinga na roho mbaya,Dk.Magufuli ata appoint mtu yeyote ambae atamuona anafaa bila ya kujali fitina za watu wachache.Ninaona historia akienda kujirudia tena!
Kama Magufuli atafanya makosa na kumteuwa Mwakyembe kuwa Waziri Mkuu. Basi yale yaliyomkuta Judge Warioba 1990 yanaweza kujirudia tena.
Judge Warioba alishinda ubunge wa Bunda na hatimaye kuwa Waziri Mkuu wa SJMT.
Mshindani wake wakati huo chama kimoja akafungua kesi mahakamani ya kupinga ushindi wa Judge Warioba.
Mahakama ikatengua ubunge wa Judge Warioba na automatically akavuliwa u-Waziri Mkuu.
Ikabidi Mzee Rukhusa achague tena waziri mkuu mwingine.
Nahisi Magufuli na Mwakyembe wanakwenda kuandika tena historia hiyo.