KING COBRA
JF-Expert Member
- Nov 10, 2011
- 2,782
- 864
Kesi ya DECI imewagusa Wachache huku Wahusika Kamili kutoka Serikalini wameachwa na Viongozi wa dini wakiwemo maaskofu na Wachungaji waliohamasisha Watu kupitia TV na Radio zao wameachwa na Kwa sasa wanafanya kazi ya kunadi CCM. Wafuatao walihusika moja kwa moja lakini hadi leo wapo mitaani na wamehusika kikamilifu kuunga mkono CCM 2010: 1. Askofu Mwasota 2.Askofu Gamanywa 3.Getrude Rwakatare 4.Alphonce Temba n.k . Kesi nyingine ikifunguliwa inaweza kuwaleta wote hawa bila kujali CCM
ATTN: ASKOFU DAVID ANDULILE MWASOTA
KATIBU MKUU (TAIFA)
PENTECOSTAL COUNCIL OF TANZANIA (PCT)
P.O.BOX 62535
DAR-ES-SALAAM.
YAH: ULEZI, USHAURI, UTETEZI NA UTANGAZAJI WA KAMPUNI YA KITAPELI DECI (T) LTD.
Kichwa cha habari hapo juu chahusika. Mnamo tarehe 08/04/2009, kamati ndogo iliyoundwa na PCT ikiongozwa na Mwenyekiti Askofu Bartholomew Sheggah ilitoa tamko kuwa wao ndio waanzilishi, walezi na washauri wa Kampuni ya DECI na kwamba matatizo yote yakitokea kwenye kampuni hiyo yapelekwe kwao na si kwa viongozi wa DECI. Kabla ya tamko hilo, ofisi yako ilitoa matangazo mazito sana kwenye vituo mbalimbali vya redio, hususan RADIO PRAISE POWER, WAPO RADIO, RADIO MLIMANI, RADIO TIMES FM, UPENDO FM n.k. kwa kumtumia Mch. ALPHONCE TEMBA ambaye alijitambulisha kama Mwinjilisti wa Kimataifa. Kitendo cha kutumia radio za Kikristo na kuwatumia Wachungaji kupigia debe kampuni ya DECI kilifanya umati mkubwa kufurika kwenye mkutano huo na wengi wao wakawa wamepata imani kubwa na kampuni ya DECI. Viongozi wa makanisa wamehusika kwa kiasi kikubwa kupora fedha za wananchi kupitia mchezo huo kwa njia ya kuhamasisha. Kitendo cha viongozi wa dini kuacha kazi ya kiroho na kuhubiri ujasiriamali kwa njia ya upatu kimewafanya watu wengi kujiunga na mchezo huo wakiamini kwamba wataokoka na umaskini, na vijana wengi waliookoka waliacha kazi ya kuhamasisha mambo ya kiroho na kuihubiri DECI huko mikoani. Ajira za wengi zimepotea kwa kukimbilia ajira za DECI, ambazo sharti lake mojawapo lilikuwa lazima mtu awe ameokoka. Hii ni dalili mojawapo ya kutimia kwa Unabii ulionenwa na Nabii Daniel, kwamba Chukizo la Uharibifu Limesimama Mahali Patakatifu na ni dalili tosha kwamba siku za mwisho zimekaribia, kwa sababu kitendo cha kuchanganya Neno la Mungu na Kamari ni LAANA! Uchunguzi wetu umebaini kuwa uhamasishaji wa watu makanisani ulifanyika na Wachungaji kwa kutumia Maandiko Matakatifu na wengine walifikia kuwaambia watu kuwa Rais Jakaya Kikwete angekuwa mgeni rasmi na angetoa msimamo wa serikali kuhusu hatma ya DECI, jambo ambalo lilikuwa la uongo. Pia inaeleweka kwamba, tamko la PCT lilikuwa limekuja baada ya serikali kupitia BOT kuonya wananchi kwamba DECI ni kampuni ya kitapeli. Tamko lililotolewa katika ukumbi wa PTA Saba Saba lilikuwa linalenga kupotosha wananchi na kuongoza uvunjifu wa sheria ambao kwa sasa amani ipo mbioni kutoweka kutokana na watu wengi, wakiwemo wajane, yatima na walemavu kutapeliwa na DECI. Ikumbikwe kwamba Mch. JACKSON MTARESI ni Mwanzilishi wa kanisa la JESUS CHRIST DELIVERENCE CHURCH ambalo limesajiliwa na PCT chini ya Mwenyekiti wa kipindi hicho Askofu Sylvester Gamanywa ambaye alitumia Wapo Radio kutangaza kwa nguvu zote kampuni ya DECI. Viongozi hawa wa DECI walimtumia sana Bw. Arbogast Francis Kipilimba (Meneja Uendeshaji wa shughuli za DECI na aliyeongoza wateja wa ELIMIKA), ambaye ni mzee wa kanisa linaloongozwa na Askofu Bartholomew Sheggah ambaye ndiye aliyesimama kutoa tamko la PCT. Uchunguzi wetu umebaini kuwa Mchungaji Dakta Getrude Rwakatare (Mikocheni B Assembles Of God), Askofu Mgullu Kilimba, Askofu David Mwasota, Askofu Bartholomew Sheggah, Askofu Sylvester Gamanywa n.k walikuwa ni wadau wakubwa na wengine kupitia huduma maalumu ya ELIMIKA. Taarifa zilizothibitishwa na viongozi wa DECI zinasema kwamba wateja wote wa ELIMIKA wamesha rejeshewa fedha zao wakati maelfu kwa malaki ya walalahoi bado hawajapata na hawajui hatma yao, jambo ambalo ni ubaguzi na dhambi kubwa! Tafsiri ya upatu ya kuwarejeshea fedha vigogo hawa ni kwamba, pesa hiyo imetokana na ile iliyopandwa na watu wengine, wakiwemo wajane na yatima walioshawishika na tamko la wachungaji la PTA Saba Saba. Kamati yetu imekuwa ikipata shida kubwa sana kuwatuliza wajane na yatima waliotapeliwa kutokana na baadhi ya Wachungaji na Maaskofu kurejeshewa fedha hizo kinyemela na hivyo ubaguzi wa matabaka umeonekana ukitenda kazi kwa wazi mno! Pia imebainika kuwa Alhamisi ya wiki iliyopita (May 28, 2009), Mch. Getrude Rwakatare ameonekana akiwabeza waumini waliopanda mbegu zao DECI na kutapeliwa kwa tafsiri kwamba wamepoteza fedha zao kwa ujinga wakati yeye mwenyewe alishawishi watu kupitia RADIO PRAISE POWER. Ikumbukwe kwamba, wananchi wengi waliamua kuingia kwenye upatu huo baada ya kuona watu kama Mchungaji Rwakatare, ambaye ni Mbunge (Viti Maalum CCM) na kiongozi wa dini, pamoja na viongozi wengine wa dini, wakishiriki upatu huo na hivyo kuhisi kwamba hakukuwa na mashaka yoyote. Leo anapoibuka na kusema watu waliopanda mbegu zao ni wajinga, anawahukumu kimakosa kwa sababu walifuata mahubiri yake na washirika wake, vinginevyo aseme leo kwamba hata mahubiri ya wokovu anayoyatoa kila siku na kushuhudia umati wa watu wakiokoka, watu wasiyafuate kuanzia sasa kwa maana wakiyafuata watakuwa wajinga! Aidha, kitendo cha maaskofu wote waliohusika na DECI kujificha katika kipindi hiki kigumu kwa wanachama wa DECI, pengine wakiogopa aibu ya utapeli uliofanyika na kuitupia lawama serikali, si cha busara kwa sababu wao ndio waliokuwa mstari wa mbele kuwashawishi kondoo hawa maskini kuingia kwenye kamari hii ya DECI. Hii inaonyesha pia kwamba, huenda viongozi hawa wa kiroho hawajali madhira yaliyowakumba wananchi wengi, bila kujali tofauti zao za kiimani na kiitikadi. Ipo mikakati mikubwa ya viongozi wa DECI wakishirikiana na baadhi ya Wachungaji ambao wanajaribu kushawishi watu waliotapeliwa kuilaumu serikali ili kuepuka aibu inayokuja hivi karibuni. Napenda kuweka bayana kwamba, lawama zote zinazotokana na utapeli wa DECI zielekezwe kwa washauri, walezi, waanzilishi na wapambe wa kampuni hiyo kwa sura ya tamko la PTA Saba Saba sawasawa na Andiko la kitabu cha Mithali 11: 18, 21. Mungu amekuwa akionya Kanisa lake kupitia BOT na Waziri Mkuu lakini PCT imekuwa ikikaidi na kumwinua mungu wa DECI, jambo ambalo linamhuzunisha Mungu. Kitendo cha viongozi wa DECI kuchukua fedha kwa watu kwa kisingizio kwamba wanachangia chama ambacho hakipo wala kusajiliwa kinahatarisha imani ya Ukristo nchini na dunia nzima. Pia napenda wananchi watambue kwamba viongozi wa DECI hawakuwa wakweli tangu mwanzo, kwani walijua kabisa kwamba shughuli zao hazijasajiliwa na kwamba ni kinyume na sheria za nchi, lakini walithubutu kuidanganya PCT ambapo sasa Wakristo wengi ndio waathirika. Hii ni kwa sababu wanajamii ni wepesi sana kuamini kile kinachohubiriwa na viongozi wa kiroho kuliko hata wanasiasa. Nakushauri uitishe mkutano wa dharura wa Maaskofu na Wachungaji ili kueleza bayana hali inayokabili PCT kwa sasa kwani waathirika wanaelekeza lawama kwako na kamati yako. Tunaiomba serikali ichukue hatua haraka kuwakamata viongozi na kupelekwa mbele ya vyombo vya kisheria bila kujali itikadi za kidini ili kuepusha machafuko yanayoweza kutokea kama Kenya endapo viongozi wa DECI wataachwa wakitembelea magari ya kifahari mitaani, huku wananchi wakihaha kusaka mbegu zao!; Yapo baadhi ya mawazo yaliyotolewa hivi karibuni na Wabunge yakilenga kuishauri serikali kuacha kuishughulikia DECI kwa kuhofia uchaguzi 2010, tunasema mawazo hayo yanalenga kujinufaisha matumbo yao na sio maslahi ya Wananchi waathirika. Hatua ya viongozi wa DECI kumtuhumu Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo, kwamba anawakandamiza Wakristo si ya kweli kwa sababu DECI si chombo cha Kikristo wala Ufunuo kama wanavyodai wao, bali ni chombo cha kitapeli. Tunaamini kwamba, hata haya maandamano ambayo wadai wanataka kuyafanya inabidi yaelekezwe PCT na siyo serikalini, kwa sababu PCT ndio waliowaita mkutano na kuwahubiria kuhusu DECI, leo wanakwenda serikalini kufanya nini? Mwisho, nachukua fursa hii kuvishukuru sana vyombo vya habari, hususan magazeti ya KULIKONI, THISDAY, NIPASHE, MAJIRA, MWANANCHI, TANZANIA DAIMA, ITV, TBC1 na mengineyo kwa kufichua uozo huu wa upatu wa DECI na kubainisha kwamba kumbe ilikuwa ni kamapuni ya kitapeli ambayo ilishindwa huko Kenya na kuamua kukimbilia Tanzania. Hakika mchango wa vyombo vya habari katika suala hili ni mkubwa sana na sisi wananchi hatuna budi kuvipongeza kwa sababu vinaendelea kufichua uovu wa DECI ya Kenya ambayo ni sawa na Kaka na Dada na DECI hii ya Tanzania. Pia tunapongeza viongozi wa kidini,vyama vya siasa pamoja na wa serikali waliokemea utapeli huu na kuwaonya wananchi wasiendelee kupanda mbegu zao kwani hivi sasa kilio kingekuwa kikubwa zaidi ya hapa tulipofikia. . MAKAMU MWENYEKITI NA MSEMAJI WA KAMATI. Nakala: Ofisi ya Rais (IKULU) Spika wa Bunge Waziri Wa Fedha Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) DECI Makao Makuu Vyombo vya habari Mtandao wa Makanisa
P.O.BOX 9937,
DAR-ES-SALAAM.
6 Juni, 2009