Kesi Pingamizi la Wananchi Dhidi ya Tuzo ya Dowans, Kesho

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Ndugu wanajamvi,

natumia fursa hii kuwapeni taarifa kwamba ile kesi ya kupinga kusajiliwa kwa tuzo ya Dowans itatajwa mahakama kuu DSM kesho tarehe 2/3/2011 asubuhi saa tatu mbele ya Jaji Mushi.

Pingamizi hii imefunguliwa na wanaharakati watatu kwa niaba ya watz wote. Hivyo tunaomba mshikamano kwa kuhudhuria mahakama kuu hapo kesho kwa wingi. Tuoneshe kwa vitendo kwamba hatupende serikali ilipe Dowans Tshs 95bil. Inashauriwa tufike mahakamani saa mbili na nusu asubuhi ili jaji atakapo ingia saa tatu basi watu wawe wameshakaa na kuwe na utulivu.

Naomba kuwasilisha.
 
Tupo pamoja katika kuhakikisha kuwa tunajenga tanzania yenye kuwajibika .nawapa pongezi hao wanaharakati waliojitoa katika kutetea maslahi ya umma inaonyesha jinsi walivyo tayari kujituma katika kuanzisha ukombozi wa nchi yetu. kwa kuonyesha hili mie kesho nitamtaarifu mwajiri wangu kuwa nina dharura hivyo nitachelewa kufika kibaruani ili niweze kufika japo hapo mahakamani kuungana katika kutekeleza haki yangu ya kikatiba chini ya ibara ya 27 (1) ya kulinda mali asili na mali ya umma. kwa pamoja tunaweza
 
Jamani msisahau kuacha kiibodi zenu kesho asubuhi na kwenda mahakama kuu
 
Back
Top Bottom