Kero za wananchi Jimbo la Kigamboni na majibu ya mbunge...

Precise Pangolin,

Nashukuru kwa mtazamo wako. Kwa mwezi huu wa Septemba nimekuwa Mbagala siku zifuatazo:

2/9 - Mwaliko Ibada Mbagala KKKT. Mchana nilitembelea miundombinu ya barabara na madaraja inayohitaji maboresho.
6/9 - Nilikutanana kusikiliza kero za wananchi katika Ofisi yangu iliyopo Mbagala Kizuiani.
13/9 - Nilishiriki katika ukaguzi wa barabara ya Kilwa pamoja na Waziri Magufuli katika eneo la Kizuiani.
21/9 - Nilitembelea miundombinu na miradi ya maendeleo katika maeneo ya Mangaya na Moringe. Siku hiyo nilitembelea kata ya Kiburugwa maeneo ya Kingugi, kwa Dumbarume na kufanya mkutano wa hadhara Kingugi.

Kata ya Mbagala ina mitaa mitano, ni mtaa upi unaouongelea wewe? Kuhusu Toangoma nilikuwa na mkutano na wadau wa maendeleo wa sekta ya elimu juzi siku ya Jumamosi 22/9.

Nilaumiwe kwa mengine lakini si kwa ziara za kata na kuongea na wananchi.
 
Kuna ukweli wa mambo yanayozungumzwa na Janjaweed.

Huyu mbunge si yeye tu hata madiwani na watendaji wa serikali za mitaa kana kwamba hawajawahi kuwepo. Barabara za kuingilia maeneo ni mbovu hata kwa kiwango cha greda bila kushindiliwa wameshindwa.

Maji ni tatizo kila mahali ukiacha wananchi wenzetu wazalendo wenye visima vyao wanaotuokoa. Kweli huu ni mzigo wetu. Angalia barabara zote za kuingilia ukitokea Kilwa road, hakuna hata moja iliyo nzima hata kwa kuchimbwa kwa grader tu. Nimesikia watajitokeza uchaguzi wa Udiwani kwenye kata moja ukirudiwa kuja kutudanganya kuwa wanafanya mambo.

Mvua zimekaribia tunasubiri siasa zingine.
 
Mh. Dr F. Ndugulile tunashukuru kuwa unaweza kujibu hoja hata kwenye mtandao.

Naomba sasa utueleze umefanya nini juu ya barabara ambazo hazipitiki ambazo wananchi wamekuwa wakizipigia kelele mara kwa mara. Aidha tueleze hapa juu ya mkakati ulio nao wa kuleta maji kwa wananchi wa Mbagala kwa ujumla wao. Angalia mfano kata ya mianzini na barabara zake. Unafahamu juu ya kutokuelewana kwa Mtendaji wa Kata na Mwenyekiti wa Serikali za mitaa wa kata ya kitongoji cha Mponda Charambe na jinsi ugomvi wao unavyorudisha nyuma maendeleo, umechukua hatua gani?

Ulifahamu juu ya M/kiti wa serikali za mitaa wa mtaa uliotajwa kuwa hawakuwa wakiiva na marehemu diwani mama Macha mpaka anafariki na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya wakazi wa huko. Kumbuka suala la ulinzi wa eneo lilianza likaishia njiani na sasa wezi wamejaa kila mahali na hatuna hata wa kutuhamasisha kulinda wenyewe kwa sababu uko mbali na watendaji nao wako mbali pamoja na wenyeviti wetu.

Tunaomba basi kama huwezi kuzungumzia mambo kwa ujumla basi angalau zungumzia suala la Mianzini ili tujisikie angalau tuna mwakilishi wetu.

Naomba usichukulie jambo hili kama mashambulizi binafsi bali uchukulie kama unaongea na wapiga kura wako wanaotaka maendeleo kwenye maeneo yao.
 
Last edited by a moderator:
Dr F. Ndugulile

Nilikupa assignment umfikishie rafiki yako waziri mama Tibaijuka, kuna watu kigamboni wanafuga mapori tu mfano kuna muarabu anaitwa akbaru nadhani ushamsikia huyu jamaa anamiliki karibia nusu ya kigamboni na cha kushangaza hayo maeneo hayaendelezi sasa kama mbunge wa kigamboni utafanya nini kumuadabisha huyu akbaru?

Maeneo anayomiliki ni kuanzia kisalawe I, Kisalawe II, Mwasonga, Lugwadu nk
 
Last edited by a moderator:
@Dr F. Ndugulile muda mrefu ukiwa bungeni unatumia muda mrefu kutetea wananchi wa Kigamboni ambao wanapitiwa na mji mpya lakini huku mbagala unaona ni sehemu yako ya kuokotea kura
 
DR.FAUSTINE
profesa tibaijuka alisema bungeni kuwa umeshapewa fidia yako kwa watakaobomolewa kigamboni kupisha mji mpya,...huoni kuwa tayari umeshatusaliti?
 
Naogopa kuwa Mheshimiwa Ndugulile hajafanya jukumu lake kiasi cha kutosha pamoja na kuzingatia majimbo ya Dar in Rahisi ki-miundombunu. Unalalamikiwa sana kutowatembelea wapiga kura wako. Sijui utaanzia wapi katika mikakati yako 2015. Ni vizuri kupata maoni ya wananchi wako. Waheshimiwa wengine wamekwishatembelea vijiji vyao vyote.

Tokea amechaguliwa 2010 sijawahi kumuona Huku Mbagala kuja kusikiliza Kero za wapiga kura wake Kama wanavyofanya wakina Mdee na Mnyika kwenye majimbo Yao yeye kutwa ni kufungua Album za miziki ya kwaya tuu.

Vilevile asifikirie ujenzi wa daraja la kigamboni atautumia kujinufaisha kisiasa kwamba amehusika kufanikisha ujenzi wake kwa michango yake bungeni tunajua hausiki hata chembe.

Huku mbagala, kongowe Pamoja na Toangoma wananchi wanaapa kutompa mbunge mvivu Kama Dr F. Ndugulile kura tena bora wangempa Komu wangepata uwakilishi mzuri Kama ilivyo ubungo na kawe.

2015 huyu mbunge wetu mvivu atakuwa kwenye wakati mgumu sana

MAJIBU YA MBUNGE:
 
Naogopa kuwa Mheshimiwa Ndugulile hajafanya jukumu lake kiasi cha kutosha pamoja na kuzingatia majimbo ya Dar in Rahisi ki-miundombunu. Unalalamikiwa sana kutowatembelea wapiga kura wako. Sijui utaanzia wapi katika mikakati yako 2015. Ni vizuri kupata maoni ya wananchi wako. Waheshimiwa wengine wamekwishatembelea vijiji vyao vyote.
Mkuu aende ubungo akaone mwenzake anavyochacharika kutatua kero za wananchi. sisi hatutaki hela yake ila anachotakiwa ni kutimiza majukumu yake kupitia mikutano kukusanya kero zetu aziwakilishe bungeni
 
Jana alikuwa anafungua album ya nyimbo za dini Kama mgeni rasmi huyo tapeli mkuu tena ilikuwa ni gezaulole. Sehemu Kama kisota na kibada lazima aje kwasababu wanaishi watu wenye hela ndefu

kaweka na picha kabisa, kwahiyo ungekuwa muwazi zaidi

sijui kama kufungua nyimbo za dini inachukua masaa 24 au labda kuna jingine mie silijui........... maana hadi kumuita tapeli yawezekana mmeshararuana

pesa na shetani ni marafiki sana mkuu
 
Mkuu aende ubungo akaone mwenzake anavyochacharika kutatua kero za wananchi. sisi hatutaki hela yake ila anachotakiwa ni kutimiza majukumu yake kupitia mikutano kukusanya kero zetu aziwakilishe bungeni

mie kila nikisoma thread hapa jamvini huwa zinalalama kuhusu mnyika kuhangaikia nchi na kusahau ubungo, the same kwa Halima na the sasa faustine...

sisikii mkilalama ya zungu, mkakongoro, na zungu mwingine ambao kwangu mimi ndio useless kabisa.......... unless mko kwenye payroll za watu, because wabunge watatu wanaojitahidi (kwa maoni yangu ni halima, mnyika na faustine) na ni vijana;

vijana mtaishia kunyeana midomoni badala ya kuendelea mbele.........
 
Dr F. Ndugulile

Nilikupa assignment umfikishie rafiki yako waziri mama Tibaijuka, kuna watu kigamboni wanafuga mapori tu mfano kuna muarabu anaitwa akbaru nadhani ushamsikia huyu jamaa anamiliki karibia nusu ya kigamboni na cha kushangaza hayo maeneo hayaendelezi sasa kama mbunge wa kigamboni utafanya nini kumuadabisha huyu akbaru?

Maeneo anayomiliki ni kuanzia kisalawe I, Kisalawe II, Mwasonga, Lugwadu nk
huyo jamaa alimchangia mkulu wakati wa kampeni pesa nyingi........ hataguswa labda serikali ya ccm iondoke madarakani; na hata wakati wa uchaguzi naskia alikimbia kabisa kwa muda
 
mie kila nikisoma thread hapa jamvini huwa zinalalama kuhusu mnyika kuhangaikia nchi na kusahau ubungo, the same kwa Halima na the sasa faustine...

sisikii mkilalama ya zungu, mkakongoro, na zungu mwingine ambao kwangu mimi ndio useless kabisa.......... unless mko kwenye payroll za watu, because wabunge watatu wanaojitahidi (kwa maoni yangu ni halima, mnyika na faustine) na ni vijana;

vijana mtaishia kunyeana midomoni badala ya kuendelea mbele.........
Mkuu Janjaweed tokea asubuhi unamtetea huyu mtu mimi nipo mbagala mkuu nafikiri ndio tunaoongoza kwa kuwa wengi dsm na tanzania kwa ujumla huyu jamaa ametufanya sisi kama machine zake za kumpa kura anaonyesha upendeleo kwa wananchi wa Kisota, Mjimwema, Gezaulole sisi huku katuacha kama wakiwa bora tungempa Komu
 
Precise Pangolin,

Nashukuru kwa mtazamo wako. Kwa mwezi huu wa Septemba nimekuwa Mbagala siku zifuatazo:

2/9 - Mwaliko Ibada Mbagala KKKT. Mchana nilitembelea miundombinu ya barabara na madaraja inayohitaji maboresho.
6/9 - Nilikutanana kusikiliza kero za wananchi katika Ofisi yangu iliyopo Mbagala Kizuiani.
13/9 - Nilishiriki katika ukaguzi wa barabara ya Kilwa pamoja na Waziri Magufuli katika eneo la Kizuiani.
21/9 - Nilitembelea miundombinu na miradi ya maendeleo katika maeneo ya Mangaya na Moringe. Siku hiyo nilitembelea kata ya Kiburugwa maeneo ya Kingugi, kwa Dumbarume na kufanya mkutano wa hadhara Kingugi.

Kata ya Mbagala ina mitaa mitano, ni mtaa upi unaouongelea wewe? Kuhusu Toangoma nilikuwa na mkutano na wadau wa maendeleo wa sekta ya elimu juzi siku ya Jumamosi 22/9.

Nilaumiwe kwa mengine lakini si kwa ziara za kata na kuongea na wananchi.
aiseeeeee
 
Sijawahi kuona jimbo lenye barabaa mbovu kama hili . ukiongelea barabara yeye lami ni hii ya kilwa tu hivi nyinginendogo ndogo ni vumbi tu mwanzo mwisho haafu hata hii bara bara inayojengwa huyu mbunge hana huruma na wananchi wake kwani ei kashindwa kupitisha gari liwe linamwaga maji barabarani kutoa vumbi. dr ni kweli eti hata hili unashindwa? kutoa gari kwenda kuchota maji tena maji yenyewe ya bure ? ni kweli unajiita mbunge kitu kidogo kama hicho unashindwa? CCM must wake up or go
 
muheshimiwa dr mbunge ndugulile unaweza kutuwekea orodha ya ahadi zako wakati wa kampeni na wapi umefikia kwa sasa?
 
mie kila nikisoma thread hapa jamvini huwa zinalalama kuhusu mnyika kuhangaikia nchi na kusahau ubungo, the same kwa Halima na the sasa faustine...

sisikii mkilalama ya zungu, mkakongoro, na zungu mwingine ambao kwangu mimi ndio useless kabisa.......... unless mko kwenye payroll za watu, because wabunge watatu wanaojitahidi (kwa maoni yangu ni halima, mnyika na faustine) na ni vijana;

vijana mtaishia kunyeana midomoni badala ya kuendelea mbele.........
Zungu he is doing fine, Jimbo la Ilala hakuna mwenye shida ya Maendeleo, kazi Mbunge na kutoa Ubwabwa kwa kila msiba jimboni kwake, viti vya kukalia waombolezaji maturubai na ubani wa Shilling 50,000/=

Hili ndilo jukumu kubwa la Mbunge wa Ilala ndugu Mussa Zungu, kuhusu Segerea Makongoro Mahanga anawajuwa watu wote wa majungu na walafi wa bia, ana special days zake za kumwaga bia kwa walafi wote.

Kwahiyo hapa nakubalina na wewe Dar es salaam ndio Bongo yetu, vijana wanaojituma ndio wamekalia kupigiwa majungu kila kukicha, na hii si kwa Wabunge tu hata kijana mtaani maisha yako yakiwa yanakwenda vizuri utashangaa chuki bila sababu.
 
muheshimiwa dr mbunge ndugulile unaweza kutuwekea orodha ya ahadi zako wakati wa kampeni na wapi umefikia kwa sasa?

Pamoja na alizoweka kikwete ama zake tu? kwa sababu kama ni pamoja na za Kikwete basi huyu muheshimiwa sitashangaa akilikimbia jamvi
 
Back
Top Bottom