Kero Kubwa za Watanzania - Changia

Kisongo Arusha ni mji mdogo unaokuwa kimakazi na kibiashara. Ajabu hakuna maji. Bomba limepita ila ni la jeshi. Sasa wameamua wale wachache waliokuwa wanapata maji kutoka jeshini sasa basi. Karibu kipindupindu
 
Kero kubwa ni NHIF bima kwanini hospitali nyingi zenye uwezo mkubwa wa kutibu watu zinakataa bima hii. Tatizo ni malipo au ni inferiority complex tuu. Wahusika fanyeni kazi bima zenu zinakataliwa sana hapa mjini
Hili ni jipu la kutumbuliwa kwa haraka sana,au tuelezwe shida iko wapi?
 
Baa na kelele kwenye makazi ya watu.HILI NAONA NEMC LIMEWAZIDI NGUVU.wako kimya kana kwamba hawalioni,ni matumaini yetu awamu ya tano "hawatatuangusha".

NEMC wanafanya kazi kwa kufuata upepo.
Hili la kelele kwenye makazi ni tatizo kubwa sana !
Linaharibu nguvu kazi ya taifa sawa na madawa ya kulevya.
Watu wanakosa amani, watoto wanaharibika kiakili nk.
NEMC wanasubiri mpaka Magufuli aongee
 
Tabia iliyojengeka ya umimi na kujijenga binafsi badala ya kufanyakazi kama "team" na kujenga taasisi zilizo imara.

Pension scheme mbovu inayosababisha hofu kwa waajiriwa wengi ya "life after office" na kupelekea kutotengeneza succession plan nzuri badala yake kuendelea kutafuta justification za watu wenye umri na ambao hawana jipya kwakua umri na wakati umewapita kuendelea na ajira.

Wachumi wetu wakiongozwa na wenye dhamana ya mipango ya maendeleo kukosa ubunifu na mbinu za ku integrate production finction zetu hali inayopelekea kukosekana kwa kitu kinachoitwa "big push" hivyo kuwa traped kwenye lower development equilibrium na kuendelea kuwa uncoordinated katika njia zetu kuu za uzalishaji uchumi..... Hii implication yake ni kuongezeka kwa watu wasio na ajira zenye tija na hivyo kuwa na narow base kwenye tax payers. Matokeo ni nchi kutokuwa na uwezo wa kutoa huduma yenye quality kwa watu wake kama afya, elimu, na mipangilio katika matumizi bora ya ardhi na mazingira ikiwemo makazi yasiyo bora etc etc.....

Watu wetu wengi kutokuelimika pamoja na hao waliosoma....Wengi kwasababu ya kukosa fursa elimu zetu ni za kuunga unga na zimekosa context....

Impressive !
 
Nyumba za serikali zilizouuzwa kifisadi zirudishwe. Aanze kudisha kwanza JPM ili awe mfano kwa wengine na akiri kama kuna makosa alifanya maana kuna madai kuwa aliwapa mpaka mahawara na nduguze. Asiuchune kama alivyofanya JK
 
Naamini timu nzima ya #WachapaKazi wa Magufuli wapo tayari kuchukua kero zetu #Watanzania na kuzifanyia kazi bila kusita.

Hivyo basi, tuweke kero za msingi hapa.

Mimi naanza na hizi;

1. Mpasuko unaosababishwa na tofauti za kiitikadi.
- Tuweke Utanzania mbele kuliko itikadi.

2. Ufisadi wa kutisha
- viporo vyote vya ufisadi vifanyiwe kazi na mfumo uimarishwe.

3. Bei Kubwa ya Umeme
- Mikataba ya umeme ipitiwe.

4. Miundombinu
- Sehemu kubwa ya Tanzania bado haina miundombinu ya barabara, maji, umeme nk.

5. Mazingira
- Mazingira yetu yanaathiriwa sana na kelele za muziki wa ma bar na vilabu, uchafu, ujenzi holela nk.

6. Mfumo wa Uchumi
- Uchumi wetu umeshikiliwa na unanufaisha tabaka fulani la wachache na wageni kutokana na serikali kutosimamia vyema fursa zinazojitokeza.

7. Madawa ya kulevya
- Madawa ya kulevya yanaua nguvu kazi ya taifa letu.

8. (Endelea ........ )
".....Hizo kero zote ziko kwenye bakuli la umasikini ambayo wengi bado wamekumbatia kwa nguvu na akili zote.. na watanzania wengi ni watu wenye busara, amani, lakini uwezo wa kuthubbutu ni tatizo la muda mrefu"
 
NEMC wanafanya kazi kwa kufuata upepo.
Hili la kelele kwenye makazi ni tatizo kubwa sana !
Linaharibu nguvu kazi ya taifa sawa na madawa ya kulevya.
Watu wanakosa amani, watoto wanaharibika kiakili nk.
NEMC wanasubiri mpaka Magufuli aongee
Mkuu nakubaliana nawe kwamba wanafanya kazi kwa kufuata upepo,manake ni kero ya wazi na kanuni na sheria za kuwaongoza kulitafutia ufumbuzi zipo lakini wanapata kigugumizi,isitoshe "citizens"wameshalalamika in vain,labda ni kweli wanasubiri mpaka "citizen number one"nae alalamike ndio wataelewa.Ila kama wanajitambua nadhani wataliangalia kwa umakini manake hakuna asiyeelewa kwamba sauti ya "citizen number one"haiendagi bure bure,ikitoka huwa inatoka na tifu tifu.
 
Ni kweli kabisa hili la nauli huku kwetu kanda ya ziwa nadhani sumatra hawapo kabisa kwa mfano kuna kampuni za mabasi.zakaria express.batco.j4 na nyingine nyingi nauli kutoka mwanza city mpaka kituo kingine ni 8000.kwa watu wa mikoa ya Mwanza na Mara nadhani watanielewa yaani kutoka stendi ya Buzuruga mpaka nyanguge.kahangara.magu.lamadi,bunda bei ni 8000 hiyo hiyo haipungui yaani huku Sumatra nafikiri haipo na serikali haipo pia watu wanajipangia bei wao kisa wana mabasi ya kichina zhongtong na yu thong upuuzi mtupu inauma sana,yaani siku ukisafiri kuja musoma ukifika Mwanza stendi ya buzuruga utakutana na nauli tofauti wakati mabasi ni yaleyale kwa mfano Mwanza to nyanguge ni 2000 unatozwa 8000,mwanza magu 3000,unatozwa 8000,mwanza to Lamadi 5000,unatozwa 8000 inauma sana
 
Kero kubwa kwangu serikali kuwatharau walimu kuwafanya kama sio chochote katika nchi hii kuwalipa mishahara duni kutowapandisha madaraja kwa wakati hatakama umeenda kusoma wanatia huruma hawa watu washule ya msingi ndokabisa wamefanywa daraja tu
 
Ujenzi wa maghorofa kila kona bila kuzingatia miundo mbinu ya maji taka matokeo yake mji una nuka Haja zote kila kona.
 
1. Huduma za jamii; Elimu. Maji, Afya very poor
2. Viwanda, kilimo na ufugaji vimekufa
3.vyombo vya fedha vimepoteza mwelekeo
4.Rushwa kwa watumishi wa serikali
5.uchumi umemilikiwa na wageni
6.utalii haisaidii nchi
7. Madini
8. NK
 
Suluhisho ni mfumo endelevu wa maisha ya watanzania wote. e.g ninapoanza shule niwe na uhakika wa ajira na baada ya kuajiriwa niwe na uhakika wa maisha bora baada yakustaafu. mambo yakiwa hivo ina maana hata watoto wangu watasoma na kutibiwa bila shida hivo sitakuwa na haja ya kuiba ninapokuwa utumishini na pia mtoto awapo shuleni hatakuwa na tamaa ya kupata kazi zenye dili ili aibe kwani tayari haoni sababu ya kufanya hivo kwa kuangalia mzazi anavyoishi. Lakini kwa sasa tunaishi maisha ya ajabu ajabu tu. Yaani tunaishi inchi moja lakini wengine wanaishi kwa kula viwavi jeshi unategemea huyu mtoto aliyelelewa kwa mlo wa viwavijeshi mapigo yake ni nini akibahatisha nafasi ya kusoma na kupata kamwanya ka kupiga dili.
 
NEMC wanafanya kazi kwa kufuata upepo.
Hili la kelele kwenye makazi ni tatizo kubwa sana !
Linaharibu nguvu kazi ya taifa sawa na madawa ya kulevya.
Watu wanakosa amani, watoto wanaharibika kiakili nk.
NEMC wanasubiri mpaka Magufuli aongee
Kweli kabisa !
 
Hii kufungia simu bandia ni jibu .kwa huko tulikotoka utawala Wa JK kwa ufisadi uliokuepo ni kwamba simu karibu zote zilio ingizwa nchini ni bandia.sasa hii kutangaza kuzifungia ni dhuluma kubwa kwa wananchi Wa Tanzania. Hili agizo litatia hasara ya Manilioni ya fedha za wananchi..naomba Raisi Magufuli aingilie kati.uzembe wa TBS na Tcra .na wezi Wa makontena bandarini isigeuzwa adhabu kwetu RAIA tulio nunua simu dukani tukijua ni simu halali .chonde chonde Magufuli usiachie HAWA mafisadi .majipu .yaka adhibu RAIA wako wasio na hatia.kwa uzembe na ufisadi wao .
 
Hii kufungia simu bandia ni jibu .kwa huko tulikotoka utawala Wa JK kwa ufisadi uliokuepo ni kwamba simu karibu zote zilio ingizwa nchini ni bandia.sasa hii kutangaza kuzifungia ni dhuluma kubwa kwa wananchi Wa Tanzania. Hili agizo litatia hasara ya Manilioni ya fedha za wananchi..naomba Raisi Magufuli aingilie kati.uzembe wa TBS na Tcra .na wezi Wa makontena bandarini isigeuzwa adhabu kwetu RAIA tulio nunua simu dukani tukijua ni simu halali .chonde chonde Magufuli usiachie HAWA mafisadi .majipu .yaka adhibu RAIA wako wasio na hatia.kwa uzembe na ufisadi wao .

Simu feki zina madhara kwa watumiaji
 
hamna tutakochoandika hapa ccm hawakijui, malalamiko yamejaa kwenye ofisi za wakurugenzi, wakuu wa mikoa, wilaya, watendaji, mabalozi wanjua fika kero za nchi hii, waanze kufanyia kazi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom