Kero Kubwa za Watanzania - Changia

(1) Kuna uchafuzi wa Mazingira utokanao na Mifuko ya Plastiki, huu ni muda muafaka kupiga marufuku moja kwa moja Mifuko hii kwa maana hali imekuwa mbaya sana, mito imeziba, mitaro imeziba, mimea imezibwa kwa sababu ya hii mifuko, hili ni bomu kubwa linalosubiri kulipuka
 
1. Tanesco and water authority.
i. Service charge mnatukata kwasababu gani wakati tunanunua luku kwa njia ya m-pesa/tigo-p/airtel-m. ii. Kwanini mita za luku mnatukata kila mwezi wakati sisi tunahitaji kununua umeme wala si kununua mashine zenu za luku?. Mm huwa naona kero sana ninapokatwa pesa bila mpangilio/ mnakula jasho langu bila kulifanyia kazi
2. Sumatra na ujinga wao barabarani.
a). Wananchi wanachajiwa nauli kubwa kupindukia ktk safari fupi kwenye barabara ya rami, mfano; ukitoka mwanza to bunda nauli unachajiwa elfu 8, mwanza to tarime nauli unatozwa elfu 10, mwanza to musoma unatozwa elfu 8-10, (hii ni kwa mabasi yote yaani daraja la kawaida na yale mengine). Wabandikieni nauli mbele ya magari abiria wenu, mfano pale dodoma nmeona kuna basi zinabandikwa nauli abiria anakuwa anajua anachoenda kukilipa ktk safari yake.
b). traffic anapokagua gari anakuta kuna kosa la gari kukosa mikanda ya kwenye siti n.k, inatokea traffic anaiandikia gari husika faini akiisha maliza anairuhusu gari kuendelea na safari, likitokea tatizo kwenye gari nani atalaumiwa?. huwa inanishangaza sana, traffic wa Tanzania hawawatakii mema wananchi bali hutetea pesa tu. Ina kera sana; mm huwa naona ni bora abiria wakapewa usafiri mwingine na sio kuruhusu kuendelea na safari wakiwa kwenye gari ile ile yenye kasoro.

Pongezi: Watendaji wa serikalini naona wengi wenu mmeanza kuwa na hamu ya kutekeleza majukumu yenu mnapokuwa kazini. nampongeza mheshimiwa aliyeko juu, halmashauri X kila mtu yuko bize na hawaruhusiwi kuzurula nje ya ofisi pasipo sababu, naona kila mtu anaulizia kazi ya kufanya
 
Tabia iliyojengeka ya umimi na kujijenga binafsi badala ya kufanyakazi kama "team" na kujenga taasisi zilizo imara.

Pension scheme mbovu inayosababisha hofu kwa waajiriwa wengi ya "life after office" na kupelekea kutotengeneza succession plan nzuri badala yake kuendelea kutafuta justification za watu wenye umri na ambao hawana jipya kwakua umri na wakati umewapita kuendelea na ajira.

Wachumi wetu wakiongozwa na wenye dhamana ya mipango ya maendeleo kukosa ubunifu na mbinu za ku integrate production finction zetu hali inayopelekea kukosekana kwa kitu kinachoitwa "big push" hivyo kuwa traped kwenye lower development equilibrium na kuendelea kuwa uncoordinated katika njia zetu kuu za uzalishaji uchumi..... Hii implication yake ni kuongezeka kwa watu wasio na ajira zenye tija na hivyo kuwa na narow base kwenye tax payers. Matokeo ni nchi kutokuwa na uwezo wa kutoa huduma yenye quality kwa watu wake kama afya, elimu, na mipangilio katika matumizi bora ya ardhi na mazingira ikiwemo makazi yasiyo bora etc etc.....

Watu wetu wengi kutokuelimika pamoja na hao waliosoma....Wengi kwasababu ya kukosa fursa elimu zetu ni za kuunga unga na zimekosa context....
 
Siasa kuwa sehemu pekee yakujiondoa kwenye individual poverty..... Kila mtu kukimbilia kufanya siasa hadi kusababisha wataalamu ku compromise taaluma zao ili wawe promoted na wanasiasa
 
, mbona unakua mkali kama pilipili? jifunze kuzuia hasira na mind na lugha yako
mimi namaanisha mkoani kuna fursa nyingi sana kwa hiyo sio kila lazima mtu aishi dar akitembeza maji na maembe bado kuna mateso mara unabomolewa, mara mafuriko, mara nauli juu na migomo ya madereva n.k
mkoani kuna fursa kibao mtu anaweza akawa analima kilimo au akafanya ufugaji wa kisasa akatoka vizuri
watanzania tuwe wabunifu sio kung'ang'ania kitu kimoja tu wakati vingine vupo tele
mmmmmmh ngoja nipite kimya
 
Pia serikali isimamie maamuzi yake.
Tumesikia mamlaka kuvifungia vyombo kadhaa vya habari, lakini vyombo hivyo vinaendelea kurusha matangazo
hahaaaa, hii ni hasira na star tv
dah washkaji hawapendwi kabisa
 
Mgawanyiko wa kisiasa ni ajira kubwa pale Lumumba.
Kuna watu wameajiriwa kwa ajili ya kuleta chuki za kisiasa wakidhani wataua upinzani.
Njia ya mkato ya kuua upinzani ni kufuta vyama vingi, sio kupotezea muda waTZ
 
Mgawanyiko wa kisiasa ni ajira kubwa pale Lumumba.
Kuna watu wameajiriwa kwa ajili ya kuleta chuki za kisiasa wakidhani wataua upinzani.
Njia ya mkato ya kuua upinzani ni kufuta vyama vingi, sio kupotezea muda waTZ

Kweli kabisa,
Kuna watu kazi yao kujenga chuki za kisiasa.
Wengine ni mawaziri wapo bungeni.
Chama ni muhimu kwao kuliko Tanzania
 
Baa na kelele kwenye makazi ya watu.HILI NAONA NEMC LIMEWAZIDI NGUVU.wako kimya kana kwamba hawalioni,ni matumaini yetu awamu ya tano "hawatatuangusha".
 
Kero kubwa ni NHIF bima kwanini hospitali nyingi zenye uwezo mkubwa wa kutibu watu zinakataa bima hii. Tatizo ni malipo au ni inferiority complex tuu. Wahusika fanyeni kazi bima zenu zinakataliwa sana hapa mjini
 
Upatikanaji wa hati za viwanja bado ni kitendawili. Mfano nina kiwanja changu halamashauri ya.kibaha kila nikienda napigwa kiswahili wakati viwanja waliuza wenyewe na pesa zetu tushawalipa tatizo nini. Tuavhe uvivu na wivu viwanja tushanunua hati ni haki yetu hata mkijizungusha kama wilayani magomeni walivyo na.mapozi kuhusu hati. Mh Lukuvi fumua.huu mfumu wa upatikanaji wa hati
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom