Keren-Happuch: My new Year Messege

Ms Judith

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
2,563
918
wapendwa

heri ya mwaka mpya 2012!

napanga kufanya safari moja muhimu sana nyumbani Tanzania katika kipindi cha wiki moja ijayo. wakati nikitafakari yote yatokanayo na safari hiyo, ndipo nilipokumbuka simulizi maarufu la Ayubu 42:9-17 ambalo nataka tutafakari kwa pamoja wakati huu tunapoukaribisha mwaka mpya. kifungu hicho ni kama ilivyo hapo chini;

Kwa hiyo Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi na Sofari Mnaamathi wakafanya kama BWANA alivyowaambia, naye BWANA akayakubali maombi ya Ayubu. Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, BWANA akamfanikisha tena naye akampa mara mbili kama yale aliyokuwa nayo hapo kabla.
Ndugu zake wote waume kwa wake na kila mtu aliyemfahamu kabla wakaja wakala pamoja naye katika nyumba yake. Wakamfariji na kumtuliza moyo juu ya taabu yote BWANA aliyoileta juu yake, nao kila mmoja akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu. BWANA akaibariki sehemu ya mwisho ya maisha ya Ayubu kuliko ya kwanza. Alikuwa na kondoo 14,000, ngamia 6,000, jozi za mafahali 1,000 na punda wa kike 1,000.
Tena alikuwa na wana saba na binti watatu. Binti wa kwanza aliitwa Yemima, wa pili Kesia na wa tatu Keren-Hapuku (Keren-Happuch). Hapakuwepo mahali po pote katika nchi ile yote palipopatikana wanawake wazuri kama binti za Ayubu, naye baba yao akawapa urithi pamoja na ndugu zao. Baada ya hili Ayubu akaishi miaka mia na arobaini, akawaona wanawe na wana wa wanawe hata kizazi cha nne. Hivyo Ayubu akafa, mzee sana naye ameshiba siku.

nimekazia jina la Keren-Hapuku (Keren-Happuch) kwa makusudi ili wale ambao walikuwa hawakijui chanzo cha jina hili linalotumiwa na mmoja wa mwana JF mwenzetu aliye maarufu hapa jamvini, basi wakijue. lakini nilichoazimia kushirikiana nanyi leo ni mamabo matatu.

MOJA
tunaambiwa kuwa ayubu alipowaombea wale marafiki zake watatu na hapo ndipo ndipo Bwana alipomfanikisha tena naye akampa mara mbili ya yale aliyokuwa nayo kwanza (42:10).

ikumbukwe kwamba hawa marafiki zake waligeuka mara kuwa kama adui zake kwani mara tu walipomuona ayubu na machungu yake waligeuka kuwa washitaki wake na watu wa kumuudhi na kumzidishia machungu yake badala ya wafariji wake (angalia majibizano kati yao na Ayubu kati ya sura ya 4-25). na ayubu hakuwaombea mara tu walipoanza kumshitaki na kumshutumu kwa kile walichoamini kuwa ni "maovu ya siri ya Ayubu" na kwamba kwa mapigo yale, anavuna alichopanda, anakula jeuri yake, bali aliwaombea baada ya kuagizwa hivyo na Mungu!

kwa hiyo wapendwa siri ndiyo hiyo, tuwaombee adui zetu ili Bwana atufanikishe na kutuzidishia katika mwaka huu mpya 2012. na pia atawaleta wafariji toka kila mahali na hawatakuja mikono mitupu kwani "Bwana mwenyewe atawaleta" (42:11)!

MBILI
tunaambiwa kuwa Bwana alimpa ayubu wana wa kiume saba na wa kike watatu (Yamima, Kesia na Keren-Hapuku (au Keren-Happuch)) na mali za wanyama. inakaziwa kuwa katika dunia yote wakati huo, hapakuwepo wanawake wazuri kushinda hao mabinti watatu wa ayubu(42;12-15)! kwa maana nyingine ni kwamba kama yangeandaliwa mashindano ya urembo wa dunia (miss world) wakati ule kama yanavyoandaliwa leo, basi, binti za ayubu (kama wangeshiriki) wangekabana!! yaani nafasi za kwanza hadi tatu zote zingetoka kwenye familia ya ayubu!!

kali zaidi ni kwamba, kutokana na uzuri wao, baba yao ayubu alijikuta anakiuka mila na desturi za wakati ule za kutowapa urithi watoto wa kike na kuwapa urithi mabinti zake pamoja (na sawawa) na watoto wake wa kiume!

kumbe basi, uzuri na mvuto wa maumbile na sura za mabinti ni baraka kamili za Mungu na kila avutiwaye na uzuri wa binti/kijana yoyote wa jirani yake, amuogope Mungu na kufanya maombi kuwa kama ni mapenzi yake (Mungu), basi na amuoe/aungane naye na awe mke/mume wake! na sio kama ilivyo sasa ambapo uzuri wa mabinti/vijana ni moja ya vichocheo vikubwa vya zinaa!!

wakaka na wadada wenye tabia za uasherati, muogopeni Mungu mwaka huu 2012, mtubu na mdhamirie kuacha tabia hizo mbaya na zinazomuudhi Mungu, naye atawasamehe na kuwasaidia kuziacha kabisa kwa kadiri ya wingi wa rehema zake na uaminifu wake udumuo vizazi hata vizazi!

TATU
baada ya hayo yote ya juu, ayubu aliishi miaka 140 na akaona wanawe na wajukuu zake hadi kizazi cha nne! maana yake aliona hadi wajukuu wa wajukuu! na hatimaye akafa mzee sana aliyeshiba siku (42:16-17)! Glory to God!

sote tuombe Mungu kwamba mwaka huu mpya 2012 uwe ni muendelezo wa miaka tele aliyotujaalia Mungu kuishi hapa duniani na hatimaye tutakapoyafikia mauti, basi tufe kifo kilicho chema na chenye furaha!

kwa haya machache, nawatakia heri na fanaka za mwaka mpya 2012.

Mungu awabariki sana

Glory to God!

dada yenu awapendaye sana;

Judith
 
Dah.....mwaka mpya na ujumbe mzuri kama huu! Mbarikiwe nyote akiwemo mtoa maada na Kerren_Happuch mwenyewe!!! HAPPY NEW YEAR...
 
kumbe upo?
umetukimbia kwa mtando ukiwa nje ndio rahisi kuwa ktk mtandao unapokuwa idle
nashukuru kwa neno mwaka mpya bado saa kama 2 hivi ndio nasi tuuone natumai wanyumbani wameshauona tayari.
 
kumbe upo?
umetukimbia kwa mtando ukiwa nje ndio rahisi kuwa ktk mtandao unapokuwa idle
nashukuru kwa neno mwaka mpya bado saa kama 2 hivi ndio nasi tuuone natumai wanyumbani wameshauona tayari.

Heri zangu za mwaka mpya ziwe nawe Lokissa japo nyie huko bado hamjasherekea!!! Happy New Year again broda....
 
Miss Judith.... Nimefurahi kujua chanzo cha Happuch (for I Love that Lady)
Nimefurahi pia kukuona maana kama ulipotea fulani hivi. Huu Ujumbe waashiria
u mzima (I hope) na kwamba tupo Pamoja huu mwaka mpya.

HAPPY NEW YEAR Dear.... Pamoja Saaana.
 
Haapy new year dada Judith

amen mpendwa

Dah.....mwaka mpya na ujumbe mzuri kama huu! Mbarikiwe nyote akiwemo mtoa maada na Kerren_Happuch mwenyewe!!! HAPPY NEW YEAR...

amen, amen mpendwa

kumbe upo?
umetukimbia kwa mtando ukiwa nje ndio rahisi kuwa ktk mtandao unapokuwa idle
nashukuru kwa neno mwaka mpya bado saa kama 2 hivi ndio nasi tuuone natumai wanyumbani wameshauona tayari.

sijawakimbia mpendwa,

ni mihangaiko tu ndio imebadili ratiba yangu ila tutaendelea kuwa pamoja .

ubarikiwe sana

Miss Judith.... Nimefurahi kujua chanzo cha Happuch (for I Love that Lady)
Nimefurahi pia kukuona maana kama ulipotea fulani hivi. Huu Ujumbe waashiria
u mzima (I hope) na kwamba tupo Pamoja huu mwaka mpya.

HAPPY NEW YEAR Dear.... Pamoja Saaana.

asante sana dada AshaDii, asante sana kwa maneno mazuri. huyo Keren-Hapuku (Keren-Happuch) alikuwa msichana mrembo sana wakati ule. nadhani member mwenzetu alipata mahali picha yake na anaitumia kama avatar manake nayo ni ya mwanamke mzuri sana (joke). hata mie nampenda sana Keren-Happuch na kwa michamgo yake hapa Jf anaonekana ni mwanamke mtulivu na mcha Mungu. Mungu amzidishie sana.

kweli nilipotea lakini ni mzima kabisa. mipangilio tu ya majukumu yangu ndo imebadilika kidogo lakini bado tuko pamoja na natumaini mwaka huu utatuweka pamoja zaidi.

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God
 
dada judith umenena vema nami nakutakia heri ya mwaka mpya. point of correction: WHAT IF YOUR BODY BELONGS TO ME (ANY ADAM) AND YOUR HEART BELONGS TO GOD?
 
Nice msg! Umenikonga sana miss J,kuona nimfuatiliaji wa visa vya bible! Now dayz watu wengi tumetekwa na mambo ya ulimwengu mpaka tunasahau kufungua vitabu vyetu vitakatifu kuona vinatuonya nini! Thanks nd be BLESSD CCTA! Happy New year!
 
MJ,
Heri na fanaka kwa mwaka 2012.
Asante kwa kutujuza kuhusu jina la Kerren, binafsi nilishausoma huo mstari but I never noticed the name.
Nikukosoe kidogo, uchambuzi wako unaongelea tusiache kuombea adui (huu ni mstari tofauti, kama sikosei kwenye mathayo, kuwa tuwaombee adui zetu na wanaotuudhi kwa maana kwa kufanya hivyo tunawapalia makaa). Ayubu aliombea marafiki. Kwa hilo tunakumbushwa kuombea both adui na rafiki, asante kwa combination. Niliwahi kumsikia mtu akisema kuombea wengine ni kama kuweka deposit bank. Na kwa kuombea wengine ni kama unamstua Mungu akuone na wewe.
Kila ndoto yako, ambayo Mungu anaona inakufaa akupatie kwa wakati, si kwa kuchelewa wala kwa kuwahi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom