nyangasese
Senior Member
- Aug 21, 2011
- 129
- 22
kama wabunge wa kenya wanalipwa zaidi,basi ndio halali kwa wabunge wa Tanzania kujiongezea mishahara na posho hali watumishi wengine wa umma pamoja na walimu na madaktari ambao kipato chao ni kidogo wakipuuzwa.Ifike kipindi sasa viongozi wetu wamwogope Mungu na waache uwongo na waone aibu.siku za nyuma tuliambiwa kuwa serikali imeamua kukomesha suala la malimbikizo ya malipo ya watumishi wake,cha ajabu leo mamia ya walimu ktk halmashauri ya jiji la mwanza wanasotea kulipwa malimbikizo ya mishahara yao kwa miaka 4 sasa bila mafanikio wakati wabunge wakikohoa tu wanalipwa.wafanya biashara na wakulima hivi sasa wana hali ngumu, lkn serikali imeamua kuwajali zaidi wabunge kwa kigezo kuwa Dodoma kuna maisha magumuKikwete mnaumuonea buree; wabunge Kenya walipwa zaidi ya wabunge wa Marekani; kwenye huo mswaada pamoja na kujiongeza mishahara, bado kuna kipengele ukiwa mbunge ukishindwa utaendelea kulipwa kwa muda wote wa maisha yako; yaani jamaa ni noma