Kazi ya Wakuu wa Mikoa ni nyepesi sana

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,931
31,173
Heshima sana wanajamvi,

Inafahamika Jumanne yatakuwepo maandamano hapa Jijini Arusha.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha imekuwa katika harakati kubwa za kutaka kuyazuia maandamano hayo kwa kutumia njia haramu na zinazo kiuka misingi ya katiba yetu yenye mapungufu mengi.

Mosi kamtumia mwenyekiti wa Bodaboda ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya Arusha kudai eti maandamano yataathiri kazi zao.

Pili katokea Mwenyekiti wa AKIBOA (WAMILIKI WA MABUS ARUSHA - MOSHI) kadai maandamano yatavuruga kazi zao.

Kajitokea Mwenyekiti wa Utalii wazawa ambaye pia ni kada maarufu wa CCM kadai maandamano yakifanyika watalii wataacha kuja Tanzania.

Misafara yote iliyopangiliwa na kupangika inaratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Mkoa.

Inasikitisha gharama kubwa zinatumika kuwahonga baadhi ya watu wenye akili ndogo kutaka kuvuruga Maandamano ambayo yanafanyika katika utaratibu wa kufuata katiba yetu.
 
Kwa kifupi hayo matembezi ya cdm yamekosa mvuto.
Hiyo ni mbinu ya viongozi hili waendelee kulipana posho kwa zile bil. 2 za ruzuku walizopewa.
 
Kwa kifupi hayo matembezi ya cdm yamekosa mvuto.
Hiyo ni mbinu ya viongozi hili waendelee kulipana posho kwa zile bil. 2 za ruzuku walizopewa.
Hizo 2b ni nyingi kiasi gani Hadi haziishi? Naona Kila kada anayejitokeza anaongelea 2b. Kama 2b zingekuwa nyingi, ccm Leo hii ingekuwa ni chama chenye viwanda na Kila mradi wa hali ya juu maana inapata zaidi ya 1b@month.
 
Ndio maana unaona mtu yupo tayari kupigana kwa ajili ya CCM maana CCM kuna pesa za kila namna madili, marupurupu, rushwa, ufisadi, kutakatisha pesa ni wewe tu.
 
Back
Top Bottom