Kazi ya Ubunge ingekuwa ni wito, je tungepata Wabunge?

Likwanda

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
3,910
1,131
Kwasasa tumefunikwa na sakata linalohusu posho za Wabunge. Wapo wanaodai ziondolewa na wengine wanataka ziendelee. Kwa uchunguzi usio rasmi ni kwamba kazi ya Ubunge imekuwa ikiwavuta watu wengi sana kutokana na Mishahara, posho na kiinua mgongo kikubwa kila bada ya miaka mitano.

Hali hii imepelekea watu wengi sana kuacha kazi zao nyeti na kuingia ktk vuguvugu la kutafuta ubunge. Vilevile wafanyabiashara wakubwa nao wamejiingiza ktk Ubunge ili kuwa salama zaidi kutoka ktk sheria mbalimbali za Serikali zikiwemo za kodi.

Wadau naomba tusaidiane mawazo ktk hili "Je kazi ya Ubunge ingekuwa ni wito kama vile kazi za Ualimu, Unesi nk tungepata Wabunge" tujadili sote bila kujari itikadi za vyama.
 
binafsi ningegombea nafasi ya ubunge..hata hapa nilipo nasubiria maslahi yafekwe na maposho yasiyo na mantiki kisha nijitose humo! kwa sasa napiga kelele huku nje na kupiga magoti Mungu asikilize maombi yangu!. Inshallah tutafika
 
Kwasasa tumefunikwa na sakata linalohusu posho za Wabunge. Wapo wanaodai ziondolewa na wengine wanataka ziendelee. Kwa uchunguzi usio rasmi ni kwamba kazi ya Ubunge imekuwa ikiwavuta watu wengi sana kutokana na Mishahara, posho na kiinua mgongo kikubwa kila bada ya miaka mitano.

Hali hii imepelekea watu wengi sana kuacha kazi zao nyeti na kuingia ktk vuguvugu la kutafuta ubunge. Vilevile wafanyabiashara wakubwa nao wamejiingiza ktk Ubunge ili kuwa salama zaidi kutoka ktk sheria mbalimbali za Serikali zikiwemo za kodi.

Wadau naomba tusaidiane mawazo ktk hili "Je kazi ya Ubunge ingekuwa ni wito kama vile kazi za Ualimu, Unesi nk tungepata Wabunge" tujadili sote bila kujari itikadi za vyama.

Hawa jamaa tulionao sasa hivi kama wabunge WASINGEITIKA
 
Subiri wawakilishi wa CAG wakianza na kukagua matumzi ya zile pesa za mfuko wa jimbo CDF.
 
Back
Top Bottom