Kazi ya mungu!

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,845
...hii kila janga linaloikumba jamii kusingizia ni kazi yua mungu maana yake nini? Serikali imefikia kikomo cha kufikiri?


Hivi haki za mwananchi mfano upatikanaji wa Umeme, barabara nzuri, huduma za hospitali, elimu bora, maji safi nk pia ni suala la kufumbiwa macho sababu tu Mungu hajapenda?


Hii Kero ya Umeme Inaudhi! :mad::mad::mad:

Kero kero kero, usiku joto feni haziwaki, usipojifunika mbu! Mabarabarani foleni kwakuwa taa haziwaki, homework hazifanyiki sababu hakuna taa, vitoweo vinaharibika, maharusi na tafrija zimedoda kwa kukosekana umeme...keroooo kerooo!

Nchi gani hii umeme wa mgao kila kukicha? Hayo mabwawa ambayo kila mwaka tunajua wakati wa kiangazi kina kitapungua, ...ni ukomo gani huo wa akili za hii serikali kiasi kwamba hawajafikiria hatua mbadala? ...au ndio zinasubiriwa siku zaa kampeni umeme kuwashwa masaa24? si ajabu mwakani patakuwa na suluhisho la muda!

Imefikia wakati sasa CHADEMA, CUF na wengineo kukifanya CHAMA CHA MAPINDUZI chama cha Upinzani.
 
Back
Top Bottom