Massenberg
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 1,173
- 1,370
Utafiti wa haraka haraka usiohitaji utaalamu utakuonyesha kuwa katika nchi nyingi meya wa mji au jiji ni mtu mwenye madaraka na majukumu yanayofahamika na kuonekana wazi. Haya ni pamoja na masuala ya uchumi na uwekezaji katika mji, afya, miundombinu, mazingira, makazi, usalama, usafiri, n.k.
Katika hali ya kushangaza mameya wa miji ya Tanzania ni watu ambao wapowapo tu na wengi wao hata hawajulikani. Mara nyingi mambo ambayo ni majukumu ya meya utakuta mkuu wa mkoa anayafanya. Kwa mfano, katika maafa ya mafuriko ya hivi karibuni mameya walitakiwa kuwa wahusika wa kwanza lakini hakuna kitu zaidi ya kupiga porojo za siasa tu.
Swali ni kwamba je, mameya wa Tanzania wana kazi tofauti na mameya wengine duniani?