Kazi na majukumu ya Meya hapa Tanzania ni nini?

Massenberg

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
1,173
1,370
Utafiti wa haraka haraka usiohitaji utaalamu utakuonyesha kuwa katika nchi nyingi meya wa mji au jiji ni mtu mwenye madaraka na majukumu yanayofahamika na kuonekana wazi. Haya ni pamoja na masuala ya uchumi na uwekezaji katika mji, afya, miundombinu, mazingira, makazi, usalama, usafiri, n.k.
Katika hali ya kushangaza mameya wa miji ya Tanzania ni watu ambao wapowapo tu na wengi wao hata hawajulikani. Mara nyingi mambo ambayo ni majukumu ya meya utakuta mkuu wa mkoa anayafanya. Kwa mfano, katika maafa ya mafuriko ya hivi karibuni mameya walitakiwa kuwa wahusika wa kwanza lakini hakuna kitu zaidi ya kupiga porojo za siasa tu.
Swali ni kwamba je, mameya wa Tanzania wana kazi tofauti na mameya wengine duniani?
 
Kwa hapa Tanzania hakuna ilipoainishwa kwa maandishi kwamba Meya anapaswa kuwa mtu wa namna gani? Uwepo wao ni kutokana na kuchaguliwa na madiwani wenzake, madiwani wenyewe nao pia upatikanaji wao ni wa kisiasa tu - wanachaguliwa na wananchi waliochoka kimaisha - ambao wakipewa chumvi kidogo tu wanachekelea kama zuzu. Kwa kuwa kuna uwezekano wa kuwa na Meya Mbumbumbu ambaye anapendwa na raia pamoja na madiwani wenzake, tusitegemee kuwabana sana hawa mameya hadi hapo tutakapoweka sheria ndogo za uchaguzi zitakazowabana wagombea kuwa na professionals.
Madiwani wengi ni form foour failer, Std VII na wengine records zao haziko wazi.
 
Na kinachowapunguzia uwezo wa maamuzi ni uwepo wa Mkurugenzi wa jiji kwani maamuzi mengi ya Halmashauri yanatolewa na Mkurugenzi ambaye ni Chaguo la Rais. Wakurugenzi wengi ndo wanarudisha maendeleo ya miji / majiji nyuma kwa kuwa wengi hawatekelezi mapendekezo ya madiwadi wa kata za mji husika; bali hutekeleza amri toka kwa Bwana wao.
 
MEYA=Mega keki na Epuka Anayekuja kama ni mwizi,hata mkurugenzi wa wilaya na mkuu wa wilaya sioni haja ya wote kuwepo ni bora awepo mmoja afanye majukumu yote
 
Nchi hii mwenye madaraka ya kueleweka ni no 1 tu,wengine wote wapo kusikiliza maagizo from him ,juzi kati mkuu wa mkoa mmoja amehamishia ofisi yake eti kusimamia ujenzi wa shule ya msingi aliyozembea kuisimamia,sasa amekurupuka baada ya kuambiwa kuwa no 1 ametoa maagizo kuhusiana na shule hiyo,pls no 1 mwagize waziri wa mawasiliano aje huku Lingusenguse
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom