Kazi kubwa anayo swaiba wangu livingstone lusinde kwa wapigakura wake 2015

ludende

Member
Jun 18, 2012
21
0



Home » Members »Contributions

email.gif
E-mail this to a friend
print.gif
Printable version
[h=2]Contributions[/h]
1694.jpg
Lusinde, Livingstone Joseph[CCM]

Mtera Constituency
Session NoSeating NoContribution DateContribution To
218 February 2011 Hoja ya Kujadili Hotuba ya Mheshimiwa Rais
Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupata nafasi hii ambayo nimeisubiri kwa muda mrefu sana na nitakuomba Mheshimiwa Spika, pamoja na Waheshimiwa Wabunge wanivumilie kwa sababu kama kujaa Roho Mtakatifu nimejaa muda mrefu sana lakini nimechelewa kupata hii nafasi.

Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia, nianze kwa kumshukuru Mungu kwa ajili ya wapigakura wa Jimbo la Mtera kwa kura nyingi walizonipatia na kuniwezesha kuingia hapa, lakini zaidi nimshukuru mke wangu mama Edina Lusinde kwa namna alivyokuwa akinituliza nilipokuwa nikipandwa na jazba wakati wa kampeni za uchaguzi.

Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Rais katika hotuba yake alifafanua mambo makubwa ambayo Serikali imefanya na mambo ambayo inategemea kuyafanya na ndani ya hotuba yake alizungumza kwa kirefu sana juu ya masuala ya msingi yanayogusa amani, mshikamano na maendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, inavyoonekana kwenye suala la amani ninavyotazama mimi ni kama vile wengine tumechoka. Wamechoka, tumeshiba sana neno hili sasa tunataka ivurugike na ndiyo maana tunaweza kuona baadhi ya viashiria vinatokea. Kwa bahati mbaya sana mimi kama Mbunge kwenye suala la amani sioni kama kuna umuhimu sana waku-provoke jamii yetu ili iumie, isipokuwa kama kweli tunadhani tunayo nafasi ya kuvuruga amani ni vyema tungeanza kuvuruga humu kwanza.

Mheshimiwa Spika, hebu siku moja tupigane wenyewe humu ili watu wajue kwamba kweli hawa wanaotaka imani ivurugike na wao wana uwezo huo. Sio kwenda kuwasakizia watu waumie halafu sisi tuko salama tunataka umaarufu kupitia damu za watu wengine. Hili halikubaliki.

Kwa hiyo, ni vyema kama kuna Mbunge anaona anaweza haya akaanzisha humu na mimi Lusinde niko tayari tukafunga mlango tukapigana humu halafu tukatoka tukawaambie wananchi jamani madhara ya haya ni haya tuliyoyaona kuliko kwenda kuwatumia watu wengine wafe, wengine waumie, halafu sisi tuwe maarufu kisiasa. Naona hili si sawa.

Mheshimiwa Spika, halafu jambo la pili, Serikali ya Awamu ya Nne wamekuwa wavumilivu mno. Imefika mahala wanapakwa matope ambayo si ya kweli. Mtu anatamka hadharani kwamba Serikali hii imetupiga mabomu. Mimi mwenyewe katika maisha yangu nimepata kupigwa na gesi za machozi nikiwa upande wa upinzani na Mheshimiwa Augustino Lyatonga Mrema akiwa Waziri. Lakini sikuita bomu kwamba kwa bahati mbaya sasa Serikali inapakwa matope kwamba inapiga wananchi mabomu.

Mimi nataka niseme Serikali ya Tanzania haijawahi kupiga wananchi mabomu, bomu si jambo la mchezo. Kwa bahati mbaya sana mabomu yalilipuka pale Mbagala, yale ndiyo mabomu kwa wale ambao hawayajui mabomu yale ya Mbagala ndiyo mabomu. Bomu likilipuka halina masihara. Hizi zingine ni gesi za machozi si bomu.

Mheshimiwa Spika, nilitaka niweke sawa hilo kwamba ndani ya nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijapata kutokea Serikali ikatumia mabomu dhidi ya raia wake kwa sababu bomu si kitu cha masihara. Nampongeza sana Rais kwa uvumilivu, amekuwa mvumilivu sana, wapo watu wamepitiliza mipaka sana, wametufikisha mahali ambapo mimi mpaka najiuliza hivi Kikwete uanajeshi wake kumbe haujamuathiri.

Mheshimiwa Rais yule hajaathiriwa na uanajeshi, yule ni mwanajeshi, lakini amevumilia, amepitiliza mpaka imefika mahali watu wanamtoa kikatuni, wanamweka kwenye mtandao wanafanya vitu vibaya kabisa ambapo viongozi wengine wasingeweza kuvumilia. Lakini yeye ameendelea kuvumilia, tunataka tuchukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anazofanya za kukuza demokrasia kuhakikisha kwamba nchi yetu inaendelea.

Mheshimiwa Spika, kuna mambo mengi yamezungumzwa na wenzangu, kwenye suala la kilimo tunahitaji kulitazama upya. Sisi wengine tulioingia humu ni watoto wa wakulima kweli kweli na tushukuru sana Serikali kwa Sheria ile ya Rushwa imesababisha hata akina Lusinde tumekuwa Wabunge tunawashukuruni sana kwa sababu tusingeweza kudhibiti hata kidogo na Ubunge sisi wengine tungeusikia kwenye ndoto, maana mkitaja watoto wa maskini waliongia humu msiponitaja mimi wote mtachomwa moto nyie, maana mimi ni miongoni mwa watoto hawa maskini kabisa wa nchi hii ambaye nimefanikiwa kuwa Mbunge kwa Sheria hii. Kwa hiyo, suala la kilimo ni suala la kufa na kupona. Hatuwezi kila siku tunazungumzia njaa, tunazungumzia kilimo.

Ningeishauri Serikali hivi tunawezaje kupeleka maboksi ya kura kila kona ya kijiji lakini tunashindwa kupeleka mbolea kila kona ya kijiji? Hebu tupeleke mbolea karibu na wananchi na ikiwezekana tujikusulu kujitoa mhanga. Tuweke nchi yetu katika kanda za kilimo, tuwape mbolea bure, kuna shida gani ili tuondoe tatizo la njaa? Kwa hiyo, mimi nina maoni hayo kwenye suala la kilimo.

Mheshimiwa Spika, lakini suala lingine ambalo nataka nimpongeze Rais na kwa hili nataka niipongeze Serikali ya Awamu ya Nne. Nimpongeze Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu aliyepita Mheshimiwa Edward Lowassa kwa shule za sekondari za Kata. Mmefanya kazi nzuri sana. Myonge mnyongeni haki yake mpeni.

Mheshimiwa Edward Lowassa umefanya kazi nzuri sana pamoja na wenzako, sisi tunawapongezeni sana pamoja na changamoto zilizopo. Changamoto nyingine na sisi wenyewe Wabunge lazima tujifunze, tumepata Waziri Mkuu aliyejiuzuru mwenyewe, kuwajibika kwa ajili ya makosa ya watendaji wake. Wengine hapa hata kujiuzuru kwa makosa ya chama tu hawawezi, wengine hata kujiuzuru kwa timu kufungwa hawawezi, lakini wakisimama hapa hadharani wanazungumzia demokrasia.

Mheshimiwa Spika, leo Bunge lako Tukufu limefanya kazi ambayo haikutakiwa kufanywa. Wabunge wa CCM wanastahili pongezi kwa kuinusuru Kambi ya Upinzani iwe timu mmoja. Tungewaacha wavurugane, lakini leo tumekaa hapa tumewatengeneza wawe kitu kimoja bado wanatuona sisi wabaya. Ndugu zangu nataka niwaambie viongozi katika nchi yetu asiyekubali kuongozwa hata yeye kuongoza hafai.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja.

1 2 3 > Last ›







speakerz.png

polis.png

members.png
Hon.Ndugai Yustino Job
1199.jpg
Kongwa Constituency
CCM
Questions(0)
Supplementary Questions (0)
Contributions(292)
All members
Comitee-email.png

searchmp.png
Enter your MP name or constituent

event.png

«««July 2012»»»
SunMonTueWedThuFriSat
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30 31





About ParliamentMandateFunctionsVision & MissionsStructureAdministrationHistoryCompositionContact
DocumentActsBillsHansards
Parliamentary CommitteeCommittee typesCommittee FunctionsCommittee Time tableCommittee CompositionCommittee reports
GlossaryThe SpeakerBillAmendments By-elections More...
Resources links Parliamentary Resources National Website Prime Minister's Office website National Electoral Commission website Africa4All project
Copyright © 2003-2012 Tanzania Parliament. All rights res
 
Back
Top Bottom