Kawawa alivyomfunika kikwete wakitunukiwa PhD ya heshima!!

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Warizi mkuu wa zamani wa tanzania hayati Rashid Kawawa alimfunika kwa mbali jakaya Kikwete wakati wawili hao wakitunukiwa PhD za heshima katika mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Dodoma. Hayo yalidhihilika wakati wasifu wa mzee kawawa ulipokua ukisomwa na dean wa skuli ya sanaa na lugha prof. Joshua Madumula. Umati uliokuwa umefurika kwenye ukumbi wa chimwaga ulilipuka kwa shangwe na makofi mazito kila wasifu wa mzee huyo ulipokua ukisomwa. Shangwe zilizidi mara wasifu wa mzee kawawa uliposomwa ukielezea mapambano yake ya kutetea maslahi na haki za wafanyakazi pamoja na mchango wake katika kukuza lugha ya kiswahili, kuanzishwa kwa JKT, vita dhidi ya nduli amini, kuanzishwa kwa umoja wa vijana wa TANU (Tanu Youth League) na mengine mengi. Hali ilikua tofauti wakati wasifu wa rais jakaya kikwete ulipokua ukisomwa ambapo watu walikua kimya hadi mchango wa kikwete katika ujenzi wa UDOM uliposomwa ndipo watu wakalipuka kwa shangwe. Wasifu wa rais kikwete kwa sehemu kubwa ulitaja nyazfa mbalimbali alizowahi kushika katika chama na serikali bila kueleza ni nini alifanya katika nyazfa hizo. Wadau wengi walisema kawawa alistahili siku nyingi kupewa heshima hiyo lakin hawakushawishika sana na wasifu wa rais kikwete wakidai kwamba uongozi wa udom ulikua ulilipa fadhila.
 
Back
Top Bottom