Kawambwa Futa Shule hii: Bunju Girls Secondary School

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Nikiwa Mdau wa Elimu ninayomasikitiko yangu kwa kuona shule ya Bweni na Kutwa Bunju Girls secondary school haina walimu wala kiongozi, tangu kuanza kwa mwaka huu, watoto wapatao 500 hawajapatiwa huduma yoyote ya kimasomo pamoja ali mbaya ya lishe. Nikiwa muumini wa Bunju Catholic tulipokea watoto wa bunju girls ambao walikuwa wamekuja kwa ajili ya kusali wanafunzi hao walipatwa na mshutuko na kuanguka hovyo jambo ambalo lilitushutua sana, tuliwauliza kuwa je hamkuja na matroni wenu? Wakasema "matroni Hayupo anashughulikia wagonjwa shuleni sisi ametupa masai atusindikize kanisani Masai alipofika karibu na kanisa akatuacha akaondoka zake, hivyo tupo wenyewe, tuliskitika sana na kuanza kuwapa msaada. Hatuishia hapo tulienda mpaka shuleni tukakuta kuna secretary peke yake ambaye alidai mkuu wa shule yuko mahututi alipata ajari yupo Moi Muhimbili na hatujui anarudi lini, na nini hatima yetu, walimu wote wamekimbia nimebaki mimi kama mnavyonionavyo. kuulizia zaidi ni kuwa Mwenye shule hana uzoefu ndiye mwenye maamuzi amulete yupi hamtoe yupi, sasa kuulizia zaidi watu waliokaribu naye wanasema walimu huwa anawadhulumu mishahara, hata wanaomjengea huwa anawadhulumu, wengine wamefikia hatua wanamuhita mwalimu alimaarufu Kichefuchefu, nawaomba wote walioguswa hasa waandishi wa habari wafike pale Bunju a watafute shule inayotangazwa sana kuliko zote wakati ni bomu wajionee hali hii, nawaomba wazazi wazingatie usalama wa watoto wao kwani vidume vinawanyemelea kufuatia njaa walionayo kwa hiyo kudanganyika ni rahisi
 
Kwa ambaye hajui shule hii ilipo, Ni pale USALAMA, unaingia ndani kama kilometa mbili hivi, iko Bondeni, shule hii, haina huduma ya maji, wala nishati kama umeme wanatumia taa za mkonono. Generaotr some times yes.
 
Kama serikali ya CCM ingekuwa kwa ajili ya wananchi ingefanya elimu kuwa huduma badala ya biashara kama ilivyo sasa. Iongeze usimamizi, kusiwe na kodi yoyote dhidi ya mapato ya shule, mmiliki afuatiliwe kwa karibu, kama ni faida anayopata iwe ni ndogo kwa ajili ya hamasa na shukrani kwake kuchangia elimu, kama lengo lake ni biashara ya kutajirika afanye biashara nyingine na sio kuanzisha shule.

Bahati mbaya CCM na serikali yake ni kwa ajili ya mafisadi, wananchi wasubiri fulana, kofia, vitenge na tu- elfu mbili, elfu kumi kila baada ya miaka mitano kwa ajili ya kutafutia kura. Fumbuka eeh Mtanzania.
 
Back
Top Bottom