Kauli za Viongozi zinazojenga halalisho la uwizi wa Kura katika chaguzi

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Kumekuwa na tabia ambayo ilianza kuota mizizi hasa wakati wa kuanzia Kwa utawala wa Magufuli.

Kuna mambo yanayofanywa na viongozi waandamizi wa kiserikali Kwa makusudi na Kwa lengo baya wanalolijua wao, nazungumzia kauli za Uchawa zinazotaka kutoa kila sifa Kwa Raisi aliyepo madarakani, kauli ambazo zilitumika wakati wa utawala wa Magufuli na baadae zilikuja kusababisha utakatishashaji wa Kura za uwizi.

Haya ni matendo na kauli za Viongozi wanazofanya makusudi Ili wajenge mazingira ya utakatishaji wa uwizi wa Kura katika uchaguzi

1. Kauli za Rais anaupiga mwingi na anatosha hivyo haina haja ya kufanya uchaguzi, Kuna kauli za utani viongozi wanaongea na kuisifia kuwa kazi inayofanyika ni kubwa hivyo hata uchaguzi c lazma kwakuwa anatosha amefanya mengi.

2. Kauli ya kila kizuri amefanya mtu mmoja, Feza flani ndo ametoa, barabara flani ameleta, kauli hizi ndo zinawapa confidence ya kuiba Kura, kauli hizi huwezi kuzisikia Kenya.

Hizi ni kauli zinatolewa makusudi Ili wakiiba Kura wajifiche kwenye kivuli Cha kauli hizi
 
Back
Top Bottom