Kauli za Viongozi wa Tanzania Zinakera

Peter Stephano 809

Senior Member
Feb 29, 2020
120
162
"Tozo za miamala na simu ziko palepale, ni Sheria ya bunge siwezi kuzifuta, anayeona hakuna unafuu ahamie Burundi"

Hii ni kauli yenye kukumbukwa iliyotolewa na Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba tarehe 19, julai 2021 akihojiwa na ITV kwenye kipindi cha dakika 45.

Maneno makali na ya kuudhi yaliyo kwenye nukuu hii yaliwaumiza watanzania wengi waliokuwa na hamu ya kujua hatma ya serikali katika maamuzi ya kuanza kutoza tozo kwenye miamala ya simu.

Mwigulu alitoa kauli hiyo bila wasiwasi na kwa kutojali lolote mithiri ya mhubiri mbele ya Waumini.

Roger Carbajal Afisa rasilimali watu kutoka Texas Marekani aliwahi kusema miongoni mwa kauli ambazo kiongozi hapaswi kuzitamka ni zile zinazobagua watu, zinazoleta chuki, na zile zenye kuchochea uhasama katika jamii husika.

Viongozi wa kiafrika hasa Vijana wamekuwa na kasumba ya kujiona miungu pale wanapopata madaraka.

Kwao kila kauli inatamkwa pasipo kujali madhara yake ya baadae.

Kauli za Viongozi vijana zimekuwa sumu mioyoni mwa watu wengi na kufanya waone serikali ni kero na haifai hata kidogo.

Tabia hii ya Viongozi kutoa lugha za hovyo haijaanza leo ni mwendelezo usiokoma kwani hata aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam aliwahi kutamka.

"Ningewaona Ile siku ya mei mosi mmebeba mababango mnataka nyongeza ya mshahara ningewacha viboko msingeamini" akiwaambia Wafanyakazi mwaka 2018.

Kuli Kama hizi hazifai kutamkwa na viongozi kwakuwa zinaumiza na zinakwaza na zipo kinyume na sheria na maadili yetu.

Tuachane na hii mifuno ya zamani kidogo tuje kwenye hii kauli iliyotolewa na naibu waziri wa ofisi ya Waziri mkuu vijana, ajira na Kazi Patrobas katambi.

Namnukuu serikali imetoa mikopo kwa vijana wote nchini hivyo Kama Kuna kijana hajapata mkopo sio mtanzania bali mkenya, mwisho wa kunukuu.

Kauli hii ya naibu waziri katambi haijawakwaza wananchi tu bali hata Spika wa bunge nae amekwazika na kumtaka aache kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu na ya msingi.

Ukijiuliza kwa kina unaweza kupata ukakasi kuwa ni sababu gani hufanya Viongozi kutoa kauli kama hizi zinazoumiza?

Mwenyekiti wa UVCCM Iringa, Mapesa Makala alipoulizwa sababu zinazopelekea Viongozi vijana kuboronga wanapopata madaraka alisema Kuna sababu nyingi.

Mosi Vijana wengi wakipata madaraka huanza kujiona wapo juu hivyo kuanza kupandisha mabega na kupuuza wengine.

Pili vijana wengi hawapikwi ipasavyo kuwa Viongozi wema ndani ya familia na vyama vya siasa hivyo wakipewa madaraka makubwa hushindwa kuyamudu, Alisema Makala.

Sababu hizi zilizotolewa na Makala Zina mashiko katika muendelezo wa utendaji wa viongozi wengi nchini hasa vijana.

Kwa kiongozi aliepikwa vizuri ni vigumu kutamka kauli za hovyo kama hizi za akina Katambi ambazo zinaleta kero kwa wananchi wengi wanaoelewa mambo kwa uwazi.

Ni matumaini yangu kuwa shule ya Uongozi iliyozinduliwa hivi karibuni pale kibaha itarejesha mafunzo ya Uongozi wa kimaadili ndani ya nchi yetu na kuondoa matatizo madogo Kama haya ambayo hayavumiliki.

Peter Mwaihola

#Picha Kwa hisani ya Mtandao

1653037909266.jpg
 
Viongizi wengi nchi za africa hawana utu na wala hakuna kiongozi ambae yupo kwa ajili ya maslahi ya nchi wengi wapo kimichongo kujitengenezea maisha yao ya baadae ndio maana ajira nyingi ni za kujuana na za kifamilia.We shukuru MUNGU hakuna vita nchi hii pambania tumbo lako na watoto wako hayo makelele ya bungeni potezea tu.
 
Kuna ukweli kuwa kauli nyingi zimekuwa na lugha za sintofahamu

Kwa mfano sioni au sijui ni kwanini wahalifu wanaitwa "Panya Road" hili neno au msamiati huu unaendaje kutumiwa na Viongozi wakuu? ...wa Kiafrika

Unafikiri huyo Afisa Roger Carbajal angesema yapi kuhusu kauli zinazotolewa kuhusu panya road?
 
"Tozo za miamala na simu ziko palepale, ni Sheria ya bunge siwezi kuzifuta, anayeona hakuna unafuu ahamie Burundi"

Hii ni kauli yenye kukumbukwa iliyotolewa na Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba tarehe 19, julai 2021 akihojiwa na ITV kwenye kipindi cha dakika 45.

Maneno makali na ya kuudhi yaliyo kwenye nukuu hii yaliwaumiza watanzania wengi waliokuwa na hamu ya kujua hatma ya serikali katika maamuzi ya kuanza kutoza tozo kwenye miamala ya simu.

Mwigulu alitoa kauli hiyo bila wasiwasi na kwa kutojali lolote mithiri ya mhubiri mbele ya Waumini.

Roger Carbajal Afisa rasilimali watu kutoka Texas Marekani aliwahi kusema miongoni mwa kauli ambazo kiongozi hapaswi kuzitamka ni zile zinazobagua watu, zinazoleta chuki, na zile zenye kuchochea uhasama katika jamii husika.

Viongozi wa kiafrika hasa Vijana wamekuwa na kasumba ya kujiona miungu pale wanapopata madaraka.

Kwao kila kauli inatamkwa pasipo kujali madhara yake ya baadae.

Kauli za Viongozi vijana zimekuwa sumu mioyoni mwa watu wengi na kufanya waone serikali ni kero na haifai hata kidogo.

Tabia hii ya Viongozi kutoa lugha za hovyo haijaanza leo ni mwendelezo usiokoma kwani hata aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam aliwahi kutamka.

"Ningewaona Ile siku ya mei mosi mmebeba mababango mnataka nyongeza ya mshahara ningewacha viboko msingeamini" akiwaambia Wafanyakazi mwaka 2018.

Kuli Kama hizi hazifai kutamkwa na viongozi kwakuwa zinaumiza na zinakwaza na zipo kinyume na sheria na maadili yetu.

Tuachane na hii mifuno ya zamani kidogo tuje kwenye hii kauli iliyotolewa na naibu waziri wa ofisi ya Waziri mkuu vijana, ajira na Kazi Patrobas katambi.

Namnukuu serikali imetoa mikopo kwa vijana wote nchini hivyo Kama Kuna kijana hajapata mkopo sio mtanzania bali mkenya, mwisho wa kunukuu.

Kauli hii ya naibu waziri katambi haijawakwaza wananchi tu bali hata Spika wa bunge nae amekwazika na kumtaka aache kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu na ya msingi.

Ukijiuliza kwa kina unaweza kupata ukakasi kuwa ni sababu gani hufanya Viongozi kutoa kauli kama hizi zinazoumiza?

Mwenyekiti wa UVCCM Iringa, Mapesa Makala alipoulizwa sababu zinazopelekea Viongozi vijana kuboronga wanapopata madaraka alisema Kuna sababu nyingi.

Mosi Vijana wengi wakipata madaraka huanza kujiona wapo juu hivyo kuanza kupandisha mabega na kupuuza wengine.

Pili vijana wengi hawapikwi ipasavyo kuwa Viongozi wema ndani ya familia na vyama vya siasa hivyo wakipewa madaraka makubwa hushindwa kuyamudu, Alisema Makala.

Sababu hizi zilizotolewa na Makala Zina mashiko katika muendelezo wa utendaji wa viongozi wengi nchini hasa vijana.

Kwa kiongozi aliepikwa vizuri ni vigumu kutamka kauli za hovyo kama hizi za akina Katambi ambazo zinaleta kero kwa wananchi wengi wanaoelewa mambo kwa uwazi.

Ni matumaini yangu kuwa shule ya Uongozi iliyozinduliwa hivi karibuni pale kibaha itarejesha mafunzo ya Uongozi wa kimaadili ndani ya nchi yetu na kuondoa matatizo madogo Kama haya ambayo hayavumiliki.

Peter Mwaihola

#Picha Kwa hisani ya Mtandao

View attachment 2231570
Mwingine huyo
IMG-20220520-WA0056.jpg
 
Back
Top Bottom