Kauli za viongozi mbalimbali kuhusu mwanafunzi atakayepata mimba

Huyu baba Jesica aache hizo!! Mbona serikali hii hii inatoa matibabu bure kwa waliopata ukimwi!! Sasa inashindwaje kutoa elimu bure kwa wanafunzi waliopata mimba?!
 
Alitiaje hiyo mimba? Au alipewa uroda kwa hiari kabisa na wote kwa pamoja wakastarehe kwa raha zao?

Kwa nini mmoja ARDHI iwe na mmoja aendele na maisha yake kama kawaida? JE na wale waliobakwa has wajomba zao, kaka zao, jirani zao wamekosa nini? Na wale wanaodanganywa kwaajiri ya shida zao. Wengine wadanganywa na maofisa wa Magufuli, ha mawaziri munawahukuje? No wonder Tanzania we are behind kwa fikra zetu za kizamani. Tukiendelea na siasa za kupayuka hatutafika mahsli popote, matokeo yake watoto wa watoto hawa Watanzania mitaani.
 
Watu tunapigania kuondoa ujinga nchini lakini baadhi ya viongozi wetu wanapigania kuongeza ujinga nchini!!! Hivi viongozi kama hawa wana nia gani na wananchi wao?! Wanataka kuendelea kutawala wajinga???
 
SERIKALI.....


SERIKALI I
"Serikali imeweka dira itakayowawezesha wasichana kuendelea na masomo baada ya kujifungua huku wale waliowapa mimba, wakishughulikiwa kikamilifu." Paulina Mkonongo, Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari, Wizara ya Elimu - 01 Disemba 2015.
_______________________________

SERIKALI II
"Serikali imeamua kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa shuleni wasifukuzwe, bali waendelee na masomo." Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, akiwa Chuo kikuu kishiriki cha UDSM cha Elimu (DUCE), 27 Aprili 2017.
________________________________

SERIKALI III
"Serikali inaelekeza Wasichana wanaojifungua warudi na kuendelea na masomo shuleni." Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (06 June 2017- Gazeti la The Citzen).
________________________________

SERIKALI IV
"Katika kipindi changu cha utawala, mwanafunzi yeyote wa kike (shule ya msingi na sekondari) akipata mimba ni marufuku kurudi shuleni. Siwezi fanya kazi ya kusomesha wazazi." Rais John Pombe Magufuli, 22 Juni 2017, Bagamoyo - Pwani.
________________________________
Rais amekataa.Full stop.He is the boss.Hao walionunuliwa kwa bei poa hawatusumbui.
 
Magufuli yupo sahihi hii pia itasaidia kujenga nidhamu ya wanafunzi na kupunguza ngono zembe na kubwa zaidi itaondoa upendeleo kama wanamfunga mwanaume (let's say school boy) Miaka 30 kwa kumpa mimba mwanafunzi (mwenzie) ili iwe fundisho kwa mamii,je adhabu kwa mwanafunzi wa kike ni ipi sasa!?

Hili sio suruhisho, na wala halitapunguza watoto kupata mimba. Watoto wanapata mimba kwa sababu mbali mbali. Wengi wana toka kwenye familia masikini, wengi wanapata kwa kubakwa, na wengine hata na baba zao, wajomba zao, kaka zao na hata waalimu. Ni Tanzania tu haithamini shida za watoto wao, kwa kuwa wazazi wengi hatujasoma. Mzazi aliyesoma atajuwa faida ya elimu na atamuongoza mtoto wake. Mzazi asiyekuwa na elimu mtoto wake pia ataelekea kwenye maisha hayo hayo. Matamko ya Rais si kwa faida ya Tanzania, ni ya ubinafsi wa fikra na kudhohofisha elimu Tanzania. Hawa watoto wakiendelea na elimu kutapunguza ujauzito wa utotoni baadaye, kuwazuwia wasiendelee na elimu ni kufanya maisha yao na ya watoto wao, baadaye yawe duni, hawa watoto watafuata nyao za wazazi wao kwa kutokuwa na elimu. Rais magufuli anajenga taifa la umasikini na lisilokuwa na elimu, kwani watoto hawa wanaopata ujuzito ni wengi sana. Pia Kauli yake ni kuvunja sheria ya haki za watoto hawa duniani. Kwa hili amechukiza watu wengi.
 
Hakuna mtu anayetaka mtoto wake apate mimba. Shida yetu ni kuwa tumezaliwa mjini na hatuelewi chochote juu ya maisha ya wenzetu huko mashambani. Tunapoangalia tamthilia za ndani na nje, tuyaangalie yaliyomo kama somo na sio kushabikia sehemu za mapenzi tu tukaacha mafunzo.

Asilimia kubwa ya watoto wanaopata mimba wakiwa shule ya msingi, ni aidha YATIMA au, wanalelewa na mzazi mmoja...in most cases, mama. Baba amefariki, mama dhohofu wa hali na maisha inabidi yaendelee. Anatokeza anayejiita mfadhili, anasaidia familia ya mama mjane, lakini mwisho wa siku anampa mimba mtoto wa hiyo nyumba.

Wababa na wamama wenye mihemko, hapa namzungumzia MTOTO ambaye uelewa wake ni mdogo...mbona tunamtwisha lawama nzito kuliko uwezo wake? Nyie wanaume msiyo na haya, mara ngapi mmemtongoza mwalimu wa sekondari na mkafanikiwa? Kama mtu mzima na ndoa yake anadanganywa na mwanaume, hukumu hizi dhidi ya watoto wasiojiweza hata kujinunulia pedi zinazingatia mazingira yao?

Tutafakari tukizingatia tunazungumzia watoto wa Taifa zima na sio wa Dar na Arusha wanaojua simu na TV. Tunahukumu lakini hata siku moja hatujawahi kuwajali hawa watoto wala kuwasaidia lolote. Tusijawe ubinafsi tukajisahau. Siku moja utakufa na wanaume hawa hawa wakware watampa mimba binti yako wamfanye tambala la deki. Dunia ni kubwa na ina mengi. Tutubu na kumuomba Mungu atuepushe na tusiyoyamudu.
Tatizo unaongea kwa hisiiiiia halafu hakuna hoja ya msingi.....Kama mtoto ameamua kudanganyika na huyo mfadhili or anyone else, akubali pia kubeba results za hiyo choice yake...Mbona simple tu...

Kama maisha magumu na njia pekee ni kujiuza uwasaidie wazazi sawa...But shule ndo usahau tena
 
Huyu baba Jesica aache hizo!! Mbona serikali hii hii inatoa matibabu bure kwa waliopata ukimwi!! Sasa inashindwaje kutoa elimu bure kwa wanafunzi waliopata mimba?!

Hapa baba Jesica aneniudhi kweli kweli. Anasema anatetea masikini, njia ya kutowa umasikini ni elimu. Ameungana na Mama Kikwete kuwaadhibu hawa watoto kuwapa umasikini kizazi na kizazi. Kwani Watanzania tumemkosea nini MUNGU? pamoja na Kenya Uganda watoto wote wabaoewa nafasi ya elimu na elimu yao inasifika kote duniani. Siasa mpaka kwenye maisha ya watoto wetu masikini..
 
Ningeweza kusema baba yako kapata hasara kwa kushindwa kutimiza majukumu yake ya kuhakikisha unapata elimu nzuri iingie ndani ya ubongo wako na kukupa uwezo wa kufikiri kwa kina au niafadhali (baba yako) angefuga njiwa ili ale nyama baade kuliko kuwa na mtoto kama wewe lakini nitakuwa namkosea sana kumlaumu yeye kwa matendo yako ya kipumbavu.

Kwa kuwa elimu imeshindwa kufanya kazi kwako kilichobaki nitakuombea kwa Mungu na tusubiri miujiza tu sababu kichwani hakiko sawa kina mapungufu makubwa. Pia kwa akili hizi inaonyesha nchi hii inashida kubwa sana sababu haziendani kabisa na sera ya viwanda ya sasa/kilimo kwanza.
Nashukuru kwa dua yako....Sadly siwezi kumuombea dua mama yako aache uchangudoa...Aendelee tu lakini hao dada zako mliotiana mimba kawatafutie shule itakayoruhusu ufedhuli wenu
 
Kwanza hili suala la kutia mimba wanafunzi, yule aliyetia mimba mwanafunzi hafungwi?
Inatokea aliyempa mimba mwanafunzi anafungwa, mwanafunzi mwenyewe kazuiliwa kuendelea na masomo.

Je mtoto atakayezaliwa atakua kwenye mazingira gani sasa? Hapo si ndio tutakuwa tunarudi kwenye mzunguko ule ule.
 
ANAYETOA RUSHWA NA ANAYEPOKEA RUSHWA WOTE NI WAKOSAJI.
WALIOTENDA TENDO LA NDOA KWA RIDHAA YAO WENYEWE NA MSICHANA KUPATA MIMBA, WOTE NI WAKOSAJI.
SHERIA HUWA HAINA DOUBLE STANDARD.
ILA KAMA MSICHNA KABAKWA NA AKAPEWA UJA UZITO BASI KOSA NI LA MWANAUME.
NI MAKOSA KUWARUDISHA WASICHANA SHULENI BAADA YA KUJIFUNGUA NA KUWAFUNGA/KUWAFUKUZA SHULE WAVULANA KWA KUWAPA UJA UZITO.
KIDINI HASA YA KIISLAMU MSICHANA ANATAKIWA KUPIGWA MAWE HADI AFE NA MVULANI HANA ADHABU YOYOTE.
TUNACHOFANYA TANZANIA SIJUI TUMEIGA WAPI.
ADHABU IWE SAWA KWA WOTE WAWILI YAANI ALIYETIWA MIMBA NA ALIYETIA MIMBA KAMA IKIDHIHIRIKA KUWA MSICHANA HAKUBAKWA.
 
Mnatumia nguvu kubwa sana kutetea hili jambo.....As if mwanafunzi kuacha ngono ni jambo lisilo epukika.....Nguvu hizi zitumieni kuwahamasisha watoto wenu na dada zenu wasijihusishe na ngono hali ni wanafunzi
Lengo la uzi huu siyo kutetea jambo hilo bali i kuonyesha jinsi serikali ilivyokuwa disorganized, complete disarray...
Watu wanatoa kauli wakidai ni za serikali kumbe ni za kwao wenyewe?
Hapo sasa kat ya serikali I-III na serikali IV, ipi hasa ndiyo SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA?
 
Hili sio suruhisho, na wala halitapunguza watoto kupata mimba. Watoto wanapata mimba kwa sababu mbali mbali. Wengi wana toka kwenye familia masikini, wengi wanapata kwa kubakwa, na wengine hata na baba zao, wajomba zao, kaka zao na hata waalimu. Ni Tanzania tu haithamini shida za watoto wao, kwa kuwa wazazi wengi hatujasoma. Mzazi aliyesoma atajuwa faida ya elimu na atamuongoza mtoto wake. Mzazi asiyekuwa na elimu mtoto wake pia ataelekea kwenye maisha hayo hayo. Matamko ya Rais si kwa faida ya Tanzania, ni ya ubinafsi wa fikra na kudhohofisha elimu Tanzania. Hawa watoto wakiendelea na elimu kutapunguza ujauzito wa utotoni baadaye, kuwazuwia wasiendelee na elimu ni kufanya maisha yao na ya watoto wao, baadaye yawe duni, hawa watoto watafuata nyao za wazazi wao kwa kutokuwa na elimu. Rais magufuli anajenga taifa la umasikini na lisilokuwa na elimu, kwani watoto hawa wanaopata ujuzito ni wengi sana. Pia Kauli yake ni kuvunja sheria ya haki za watoto hawa duniani. Kwa hili amechukiza watu wengi.
Nilivyomuelewa mie Raisi hajawazuia kusoma wanaweza kuendelea kusoma nje ya mfumo anaousimamia yeye kwa sasa (elimu bure) kwingine wanaruhusiwa kuendelea na masomo, na hili halijaanza Leo toka zama zetu ilikua hivyo
Wazazi tusitumie umasikini kutetea uchafu wa watoto wetu hao wanaobakwa wanajulikana. Wazi wamebakwa na hata familia nyingi huwasaidia ila kuna watoto fyatu wanatembea mpaka na waume za watu hawana hata chembe za aibu na hapo ndio mimba zinakatazwa wakiruhusiwa je si itakua balaa!!? Kama wanajijua ni masikini ndio wafunge mikanda wasome waache macho juu
 
Tatizo unaongea kwa hisiiiiia halafu hakuna hoja ya msingi.....Kama mtoto ameamua kudanganyika na huyo mfadhili or anyone else, akubali pia kubeba results za hiyo choice yake...Mbona simple tu...

Kama maisha magumu na njia pekee ni kujiuza uwasaidie wazazi sawa...But shule ndo usahau tena


Mawazo kama haya ya Watanzania kama nyinyi ni ukosefu wa elimu, na ndiyo linalotutesa sisi `Watanzania. Viongozi wetu wammetufikisha hapa kwa kututawala kama ng'ombe hatuna usemi, hata Wabunge wetu tungoje watasema nini. Mawazo yao ya visasi na ukosefu wa elimu ya mawazo ndizo zimetufikisha hapa tulipo. Ninapenda Rais Nagufuli hatuwa zake anazozichukuwa, lakini kwa hili anahitaji awe polished ajuwe mawazo ya watu duniani yamebadilika. Watoto hawa hwaitaji adhabu wanahitaji kuelimishwa ili wawaelimishe watoto wao wanaowapata utotoni. Hawa ni watoto.
 
Ili kutenda haki kwa pande zote ni vema pia kubadilisha hili: ikiwa mtoto wa kike ataruhusiwa kuendelea na masomo baada ya kujifungua basi inabidi ile sheria inayomtaka mtu yeyote atakayetembea na binti wa chini ya miaka 18 kutumikia kifungo cha miaka 30 jela nayo ibadilike.
Hakuna haki kumfunga kijana wa kiume kwa miaka 30 hali ya kuwa umehalalisha binti kuzaa akiwa mwanafunzi. Kwa hiyo kijana aliyempa mimba naye aruhusiwe kumhudumia mtoto na aendelee na maisha yake kama kawaida badala ya kufungwa; hapo tutakua tumetend haki. Ila kama adhabu kwa mwanaume itabaki pale pale lakini kwa mwanamke ikawa ni halali kufanya hivyo hapo hakuna haki yoyote.
 
Back
Top Bottom