Kauli za viongozi mbalimbali kuhusu mwanafunzi atakayepata mimba

In the bottom line, Rais ndio ana kauli ya mwisho! A student choose between the two, raising family or raising her brains...
The luxury to have kids and studies altogether is reserved only for college students as well as University students...
Dah ila nchi yetu hii bwana ssa chuoni ndio hasomi ama??? Na je akianza kutumia condom au akitoa mimba si ataendelea kusoma huku akiwa mzinzi au shida yenu mnaona tabia inaporomoka akiwa na mtoto pekee??? Ssa kma kila mwaka mamia wanaacha shule kutokana na janga hili ambalo linachangiwa na umbali wa mashule yenyewe na usafiri duni vijijini ssa kivp mimba muwaadhibu huku changamoto hamjazisolve????

Serikali ya ajabu sana hii na nyie wachangiaji nawashangaa sana
 
Unaomba ushauri wa nini!!! hujioni kwamba umekurupuka!?

Hayo maneno ya Mama Samia kama ni hayo hayo hakuna lililotofautiana.

Kwani si kasema wanawaadhibu sasa kutokurudi shule ya bure si ndio kayasema JPM.

Wana uhuru wa kwenda shule zingine kusoma zisizo zile za bure wakisha jifungua.
Kujaribu kutetea kila jambo kwa kujitoa ufahamu unaweza kujiweka uchi na kuonekana mpumbavu mbele za watu pasipo sababu za msingi. Hizo kauli mbili HAZIFANANI ASILANI.

Ninavyofahamu mimi, tunalo bunge kwa ajili ya kutunga sheria na kuboresha sera za serikali kwa kila jambo la maslahi ya taifa. Suala la elimu ni suala la kisera zaidi na sio matakwa ya mtu mmoja. Kuna mara nyingine tukubali kuwa kukurupuka ni tatizo na kuwa msikivu si udhaifu bali ni ukamilifu.

Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa serikali hii kujisahaulisha majukumu yao na kudhani hii ni Kingship. Unajifanya umesahau Waziri mmoja alitangaza kuwa hakutakuwa na ndoa kwa mtu yeyote asiye na cheti cha kuzaliwa lakini siku chache tu baadaye mamlaka yake ya uteuzi wake ikasema otherwise.

Hakuna anayetaka watoto wapate mimba, lakini ni jambo linahitaji umakini hata katika kulizungumza.
 
Mimi namuunga mkono raisi magufuli ili iwe fundisho kwa watoto wanaojiingiza kwenye mahusiano
Sasa changamoto mnazijua au mnafkiri watoto wanapenda kurubuniwa kirahisi tu?? Hivi mkijenga shule za bweni nyingi huko vijijini na pia mkasolve changamoto kma za maji umbali wa shule pia walimu muwape motisha na wawepo wa kutosha ili kusimamia vzuri hta makuzi ya watoto unafkiri tatizo hili halitoisha ssa nyie mnasolve impact/matokeo badala ya kutibu chanzo

Eti hoja ni mahusiano??? Ssa kma mazingira ya kusomea ndio kma haya ya sasa hamuoni tutakuwa nchi ya watu wa ajabu sana baada ya miaka 50?? Watajaaa single parents iliterate eti mahusiano sasa wakitumia condom wasipate mtoto bado si atabaki shule ssa ndio mmesolve nni hapo????

Kma haya ndio mawazo ya wananchi wote basi itachukua miaka 100 kufkia maendeleo ya kweli
 
SERIKALI I
"Serikali imeweka dira itakayowawezesha wasichana kuendelea na masomo baada ya kujifungua huku wale waliowapa mimba, wakishughulikiwa kikamilifu." Paulina Mkonongo, Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari, Wizara ya Elimu - 01 Disemba 2015.
______________________________________________

SERIKALI II
"Serikali imeamua kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa shuleni wasifukuzwe, bali waendelee na masomo." Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, akiwa Chuo kikuu kishiriki cha UDSM cha Elimu (DUCE), 27 Aprili 2017.
______________________________________________

SERIKALI III
"Serikali inaelekeza Wasichana wanaojifungua warudi na kuendelea na masomo shuleni." Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (06 June 2017- Gazeti la The Citzen).
______________________________________________

SERIKALI IV
"Katika kipindi changu cha utawala, mwanafunzi yeyote wa kike (shule ya msingi na sekondari) akipata mimba ni marufuku kurudi shuleni. Siwezi fanya kazi ya kusomesha wazazi." Rais John Pombe Magufuli, 22 Juni 2017, Bagamoyo - Pwani.
______________________________________________
Mwenye nchi kazungumza bila kumung'unya maneno!namuunga mkono, huwezi kuchanganya wazazi na watoto
 
Unaomba ushauri wa nini!!! hujioni kwamba umekurupuka!?

Hayo maneno ya Mama Samia kama ni hayo hayo hakuna lililotofautiana.

Kwani si kasema wanawaadhibu sasa kutokurudi shule ya bure si ndio kayasema JPM.

Wana uhuru wa kwenda shule zingine kusoma zisizo zile za bure wakisha jifungua.
Mkuu cocochanel labda nkuulize.... kwa yale mazingira ya kusomea hasa vijijini ambapo shule zipo distance ya kilometre 20, unasomba maji kilometre 10 tokea ulipo, kushindia mlo moja kutokana na hali duni ya maisha afu ukifika shuleni hakuna walimu na kma wapo hawana motisha hta ya kuwasimamia wanafunzi kimaadili unategemea adhabu hizi zitasaidia nni kma chanzo kipo palepale?????

Kwanni serikali wakati inatoa adhabu hizi na yenyewe isijikite kujiuliza changamoto na kwenda kuzishughulikia ili matukio haya yasijirudie???

We kma mwanamke unaona hii ni sawa kwa kuzingatia 70% ya matukio hya ni vijijini
 
ndio tatizo la kuwa kila mwanasiasa ni msemaji wa serikali,kila mmoja anaongea lake kutegemeana na wasikilizaji wake,ni mihemko tu,hili ni suala linalogusa taifa ilibidi litolewe kauli moja nini msimamo wa serikali kuhusiana na hili.
 
Hii nchi bila kutumia lugha ngumu watu hawawezi kujifunza. Nadhani JPM anatufundisha namna watu wanavyoweza kuchukua tahadhali, kwamba mtoto akipewa mimba ndo basi tena. Hapa jamii, viongozi, wazazi na mtoto mhusika lazima wawe makini.
 
Hujui kitu. Sheria ipi inayosema mwanafunzi akijifungua anarudi shuleni kuendelea na masomo? Kama hujui sio lazima uchangie.
Mkuu kila mtu ana haki ya kupata elimu hyo ni haki ya kibinadamu kabisa ambayo kila serikali inasimamia kma ilivyoazimiwa umoja wa mataifa sasa kivp hiyo haki ipokwe????
 
Hii nchi bila kutumia lugha ngumu watu hawawezi kujifunza. Nadhani JPM anatufundisha namna watu wanavyoweza kuchukua tahadhali, kwamba mtoto akipewa mimba ndo basi tena. Hapa jamii, viongozi, wazazi na mtoto mhusika lazima wawe makini.
Ndio mjadala unakuja kwamba hao watoto walizaliwa wahuni ama factors za maisha hasa vijijini ndio zinapelekea hayo

Maji km 10

Shule km 20

Akifika shule Walimu hamna

Nyumbani extended family hakuna muda wa ufuatiliaji wa mwenendo wa mtoto

Maisha magumu hali duni hta akihongwa mia tano analegea

Sasa suluhisho ni kufuta hizo changamoto au kutimua mwanafunzi??? Lets be serious watanzania
 
Tupo pamoja mdau,wachaguwe sebene(ngono)au masomo huwezi kuchanganya vitu viwili wakati mmoja
Ndio mjadala unakuja kwamba hao watoto walizaliwa wahuni ama factors za maisha hasa vijijini ndio zinapelekea hayo

Maji km 10

Shule km 20

Akifika shule Walimu hamna

Nyumbani extended family hakuna muda wa ufuatiliaji wa mwenendo wa mtoto

Maisha magumu hali duni hta akihongwa mia tano analegea

Sasa suluhisho ni kufuta hizo changamoto au kutimua mwanafunzi??? Lets be serious watanzania
 
In the bottom line, Rais ndio ana kauli ya mwisho! A student choose between the two, raising family or raising her brains...
The luxury to have kids and studies altogether is reserved only for college students as well as University students...
Ni ujuha kabisa kufikiri kwamba maamuzi,utashi au fikra za mtu mmoja zinapaswa kuamua hatma ya mtu katika hatua yoyote ile ya maisha yake.

Huyo Magufuri mwenyewe kama anadhani ana hoja ya msingi atoe maelezo kutushawishi na sio kutumia nguvu za kimadaraka kulazimisha mambo.

Kwanza kuwa na fikra za namna hiyo ni kumkufuru Mwenyezi Mungu.
 
Back
Top Bottom