Kauli za Rais Magufuli zionyeshe uhalisia kwa vitendo

andy90

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
270
105
Kauli za Mh. Rais Magufuli zionyeshe Uhalisia

“Tanzania hii ilikuwa shamba la bibi … watu walikuwa wanafanya ya hovyo, ninaposema ya hovyo ni ya hovyo kweli.”

“Mimi nimekuwa waziri kwa miaka 20, mambo ya mateso kwa wananchi hayana chama- ukikosa dawa hospitalini utakosa tu uwe CHADEMA au CCM, kwa hiyo, hatua tunazochukua ni kwa ajili ya wananchi wote bila kujali itikadi zao,”

“Tumefika hapa tulipo (kilele cha ufisadi) ni lazima atokee mmoja wa kuyafanya na ndiyo maana nasema ndugu zangu, nimeamua kuwa sadaka ya Watanzania, kazi hii ni ngumu, kila mmoja anajitahidi kuzuia tunayofanya, endeleeni kutuombea lengo letu ni kuwasaidia ninyi (wananchi).

“Ni lazima tufanye haya (kufuta ufisadi) tusipofanya hakuna sababu ya mimi kuitwa rais, nasema kwa dhati kutoka moyoni hakuna sababu ya mimi kuitwa rais, ndiyo maana tunaamua kufukuza, na tunafukuza baadaye watapelekwa mahakamani. Kwenye hili sitaangalia sura,”

“Ni lazima tufike mahali tuache kuvumiliana, kuoneana aibu, haiwezekani nchi yetu iendelee kuwa maskini.” - Rais Magufuli​
 
Uhalisia unakuja kama na wewe unashiriki katika kuhakikisha kuna uhalisia wa hicho kilichozungumzwa, mind you hakuna mtu atakayebadili maish ayako isipokua wewe mwenyewe, huo ndio ukweli mchungu. Shiriki katika shughuli za kimaendeleo utakutana na uhalisia wenyewe.
 
Mwanzoni baada ya MCC kujitoa nilimsikia akisema kuwa 'Tanzania ni nchi tajiri na tunaweza kujitegemea wenyewe'
Juzi nimemsikia wakati akiongea na wana magamba wenzake kuwa 'tumeonyesha juhudi ya kusimamia nchi na sasa wafadhili wameanza kumwaga misaada', huku akitolea mfano daraja la TAZARA, barabara ya Chalinze - Ubungo, reli ya Kigoma mpaka Kigali nk.
Kwangu mimi ni miluzi mingi tu!
 
Jitihada za watu za kimaendelewa ikiwa watu wanaiba serikalini Nonsence bro. zjaleta uzi kishabik
 
nzoni baada ya MCC kujitoa nilimsikia akisema kuwa 'Tanzania ni nchi tajiri na tunaweza kujitegemea wenyewe'
Juzi nimemsikia wakati akiongea na wana magamba wenzake kuwa 'tumeonyesha juhudi ya kusimamia nchi na sasa wafadhili wameanza kumwaga misaada', huku akitolea mfano daraja la TAZARA, barabara ya Chalinze - Ubungo, reli ya Kigoma mpaka Kigali nk.
Kwangu mimi ni miluzi mingi tu!
yeah kimsing nakubaliana na wewe big up
 
Kauli za Mh. Rais Magufuli zionyeshe Uhalisia

“Tanzania hii ilikuwa shamba la bibi … watu walikuwa wanafanya ya hovyo, ninaposema ya hovyo ni ya hovyo kweli.”

“Mimi nimekuwa waziri kwa miaka 20, mambo ya mateso kwa wananchi hayana chama- ukikosa dawa hospitalini utakosa tu uwe Chadema au CCM, kwa hiyo, hatua tunazochukua ni kwa ajili ya wananchi wote bila kujali itikadi zao,”

“Tumefika hapa tulipo (kilele cha ufisadi) ni lazima atokee mmoja wa kuyafanya na ndiyo maana nasema ndugu zangu, nimeamua kuwa sadaka ya Watanzania, kazi hii ni ngumu, kila mmoja anajitahidi kuzuia tunayofanya, endeleeni kutuombea lengo letu ni kuwasaidia ninyi (wananchi).

“Ni lazima tufanye haya (kufuta ufisadi) tusipofanya hakuna sababu ya mimi kuitwa rais, nasema kwa dhati kutoka moyoni hakuna sababu ya mimi kuitwa rais, ndiyo maana tunaamua kufukuza, na tunafukuza baadaye watapelekwa mahakamani. Kwenye hili sitaangalia sura,”

“Ni lazima tufike mahali tuache kuvumiliana, kuoneana aibu, haiwezekani nchi yetu iendelee kuwa maskini.” - Rais Magufuli​
Hatuwezi kuona mazuri ya haya Magufuli anayofanya sasa hivi overnight. Itachukuwa muda baada ya maisha kuwa magumu kwa muda.
 
Mwanzoni baada ya MCC kujitoa nilimsikia akisema kuwa 'Tanzania ni nchi tajiri na tunaweza kujitegemea wenyewe'
Juzi nimemsikia wakati akiongea na wana magamba wenzake kuwa 'tumeonyesha juhudi ya kusimamia nchi na sasa wafadhili wameanza kumwaga misaada', huku akitolea mfano daraja la TAZARA, barabara ya Chalinze - Ubungo, reli ya Kigoma mpaka Kigali nk.
Kwangu mimi ni miluzi mingi tu!
Hapo mkuu ndio unatakiwa kuamini hakuna mwanasia anayesemaga ukweli.Tanzania tajiri inaweza kujitegemea baada ya siku mbili tumefanya juhudi wafadhili wameanza kumwaga misaada na unaona anafuraha usoni anacheka.Tulisema Tanznaia kuanza kujitegemea sio leo wala kesho hayo yalikuwa maneno ya wanasiasa.
 
Hatuwezi kuona mazuri ya haya Magufuli anayofanya sasa hivi overnight. Itachukuwa muda baada ya maisha kuwa magumu kwa muda.
Ukiona kizuri kinafanyika halafu hukioni na unategemea utakiona baada ya muda ujue una tatizo la kuona au hauna uelewa.Nyota njema huonekana mapema. Uongozi mzuri huonekana mapema.Haiwezekani kila jambo unavurunda halafu utegemee kuja kufanya vizuri mbeleni hio haitokaa kamwe itokee.
 
Mkuu neno "kuona na uhalisia" hapa unalitafsiri vipi?
 
Mwanzoni baada ya MCC kujitoa nilimsikia akisema kuwa 'Tanzania ni nchi tajiri na tunaweza kujitegemea wenyewe'
Juzi nimemsikia wakati akiongea na wana magamba wenzake kuwa 'tumeonyesha juhudi ya kusimamia nchi na sasa wafadhili wameanza kumwaga misaada', huku akitolea mfano daraja la TAZARA, barabara ya Chalinze - Ubungo, reli ya Kigoma mpaka Kigali nk.
Kwangu mimi ni miluzi mingi tu!
We ni fara Na mpumbavu kama unasikia ya Magufuri Na kuyaita miluzi , nadhani ukapimwe akili uchizi unakunyemelea
 
Wezi wa mali ya umma ndio pekee yao watakaomlaumu JPM;
Tena ole wenu, ole wenu nyie mliokula Tanzania mkaifikisha hapa;
Dr. JPM usiache hata mmoja, watumbue tena bila ganzi, wakomeeee;
 
Kati ya wewe na yeye nani uchizi unamnyemelea?
Huna kazi ya kufanya mburula weye ukashinde kwwy luninga ?
Misukule kama wewe hamuishi, na jinsi ccm inavyovuruga tena hii elimu yetu basi watu kama nyie mnazalishwa kwa wingi. Umekunywa maji ya bendera?
 
Wezi wa mali ya umma ndio pekee yao watakaomlaumu JPM;
Tena ole wenu, ole wenu nyie mliokula Tanzania mkaifikisha hapa;
Dr. JPM usiache hata mmoja, watumbue tena bila ganzi, wakomeeee;
Kwani watanznai 40+millioni anaotaka kufikiri kwa niaba yao wote ni wezi? Subiri jinsi siku zinavyozidi kwenda kama wanaopiga kelele kumkosoa kelele zao zitagonga mwamba utakuja mwenyewe kwenye hili jukwaa kumkana na kumshambulia. Ukiona kiongozi yeyeto yule anaetaka kuongoza nchi kwa kuteka ile mihimili mingine miwili jua kuna kitu.
 
Kwa hiyo mtoa hoja unataka kutuambia Magufuli anaongea tu bila vitendo?
Hadi sasa mmi binafsi sijaona kama kuna hata nusu ya yale tutalajiayo,, kuwa ameafanya naona bado anabagua watu wa kushughulikia,,,
 
Back
Top Bottom