Kauli za Rais Magufuli zinajichanganya, lazima kuna tatizo mahali

Jana tulimsikia Rais wetu akieleza mambo mbali mbali katika nchi. Hata hivyo kupitia hutuba yake hiyo, kama kawaida imeleta maswali mengi kuliko majibu.

Suala la nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma

Rais wetu baada ya miaka miwili bila nyongeza anakuja kusema kuwa hataongeza mpaka kuongezeke uzalishaji jana tarehe 3 oktoba, 2017. watu wanauliza ni uzalishaji upi huo? jee alikusudia kila mfanyakazi azalishe ndio aongezwe mshahara au alikusudia uzalishaji wa mapato kitaifa? Kwa nini iwe baada ya karibu miaka miwili? Jee sheria na miongozo ya kiutumishi inakubaliamna na alichokisema?

Mwanzoni serikali ilisema kuwa inahakiki watumishi hewa na kumekuwa na danadana nyingi. Kujichanganya huku ni kwa sababu gani lazima kuna tatizo mahali.

Suala la vyeti feki na Makonda.

Hapa napo kauli zimejichanganya, tumeshangaa kusema wanaolalamika leo mitandaoni ni wale waliofukuzwa kazi kwa vyeti feki lakini hapo hapo akamsifu makonda anayetuhumiwa kuwa na vyeti feki na majina feki. alienda mbali eti hata kama asingejuwa kusoma ilimradi amedili na madawa ya kulevya ingetosha. Hapa kuna undumi la kuwili. Kwani hao waliokuwa na vyeti feki hawakufanya wajibu wao vizuri? Iweje Makonda pekee apewe kinga hizi ?

Watu wanashindwa kujuwa Rais anasimamia nini vyeti feki au kulinda maswahiba ? Katika hali hii lazima kuna tatizo.

Mwisho.

Sisi wengine tunaamini kuwa taasisi ya urais ni nyeti sana, maneno huumba na huumbuwa. Tulitamani rais wetu awe mfano kwa kila jambo. Kwenye haya mambo walau mawili rais wetu anajichanganya sana. Tunahitaji atuoneshe njia badala ya kutupoteza. Naamini kwa kauli za jana zitashusha morali ya kazi kwa wafanyakazi maana kulikosekana walau lugha ya matumaini. Uzalishaji upi unawahusu watoa huduma kwenye ofisi za umma? Jee mpaka lini na kwa kipimo kipi kitawahusu hawa wafanyakazi?

Tunakuomba rais wetu utuoneshe njia.


Kishada.
Albadili inafanya kazi
 
Waliosomea Management wanafahamu vizuri namna ya handle Rasilimali watu. ukiwavuruga watakuvuruga tu hata kama ukiwa kama simba. Ninamkumbuka sana Mkapa alikuwa anasimama majukwaani na kusema, Namnukuu " hakuna nyongeza ya mishahara mpaka mniambie mmefanya nini" (lengo lake lilikuwa kuwaficha wafanya biashara wasipandishe bei ya bidhaa kwa wananchi kwa sababu ya kupanda kwa mshahara) kwa kweli tulimuelewa Rais Mkapa. Sasa huyu wa sasa haeleweki kabisa Wafanyakazi wa Umma waongeze uzalishajiiiii wapi? Kwa hiyo hawa Askali wetu Polisi wazalishe nini, Wanajeshi wetu wazalishe nini, Mahakimu wetu na wafanyakazi wa Mahakama wazalishe nini?. Ninaona Rushwa ikiongezeka sana, na matukio ya wizi na uporaji ukiongezeka kwa kauli hii ya mkuu wa nchi. ( Ni ya kukatisha tamaa kabisa). Sijui wapi tulikosea hapo hapo bila ya kufikiria alichosema sentensi mbili tatu zilizopita, namnukuu " Serikali yangu imeweza kuvuka malengo kwa kukusanya zaidi kuliko kutoka Bill 800-900 mpaka Trillion 1.3. kwa mwezi" Sasa anataka tufike wapi?

Mimi Ninashauli tu. Tunaomba waliokaribu na Rais wetu wamshauri awe anasema yale yaliyoandikwa kwenye karatasi lakini kutoa tu maneno ambayo yanajipinga yenyewe kwa yenyewe Tunashangaa sana, Tunajiuliza hivi kweli kuna umakini katika kufanya kazi za nchi au kuna tatizo la kusahau katika viongozi wetu.
 
Sasa hivi tutaanza kufukuzana na magari ya Ugawaji kununua unga wa muhogo kwa vidaftari tena.
 
Na kuna watu walikuwa wanashangilia mfano aliuliza kwani nyinyi wenyeviti mmesoma?watu wakashangilia,siongezi mishahara!! Watu wakashangilia watanzania bwana tunafurahisha sana
Kamera zinamulika acha kushangilia utumbuliwe
 
Jemedari makini huwa anawapa moyo sana wapiganaji hata kama mambo hayaendi kama alivyopanga. Kutokuwapa matumaini kunaweza kuwavunja morali na wakashindwa vita.
 
Nafikiri hakujichanganya bali alikuwa anajaribu kuweka taswira halisi ya KIUCHUMI kabla ya kuongeza chochote.
Kuhusu RC. Makonda nafikiri kwa kifupi alikuwa akisema anapenda mtu AFANYAYE kazi.
Na hivyo kusema kuwa MASOMO mengi bila UZALISHAJI basi ni heri ASIYESOMA sana na anaweza kutoa MATOKEO. Kuliko kigezo cha elimu.
Ndugu zetu 12000 hakukuwa na wazalishaji na wazalendo?
 
Mkuu bendera ya Japan ikoje?
_20171004_120805.JPG
 
Nimefikilia kiuwendawazimu Sana kuhusu hawa watu wa kanda ya ziwa kuhusu hii sigara kubwa

Note msininukuu vibaya sijasema ya kuwa anavuta.
 
Ndio eti anajiita raisi wa wanyonge!!!! Mbali zaidi tuna miaka 7 long way to go
 
Back
Top Bottom